Bongo movie bila mabasi ya mikoani ingeshakufa

Bongo movie bila mabasi ya mikoani ingeshakufa

Kuna movie moja ina part nne zaidi ya four hours ni bongo muvi tu inachosha sana

Dreams never end by fear
 
Mkuu, nimeitikia wito baada ya kusikia ukiniita.

Kiukweli Bongo Movies na tasnia nzima ya filamu ipo 'Babeli', hili la kutumia mabasi ya mikoani kama mambo mengine hayajawekwa sawa haliwezi kusaidia chochote. Kuna matatizo makubwa mno yanayotakiwa kwanza kushughulikiwa. Hapa chini naweka makala niliyoandika jana na imetoka kwenye gazeti la SpotiLeo la leo Jumapili:


Tasnia ya filamu Tanzania ni sawa na soka bila refa!

Na BISHOP HILUKA

HADI leo sijajua ni ‘impact’ gani iliachwa na maandamano ya mwezi Aprili mwaka huu ya wasanii wa filamu walioandamana kushinikiza kusitishwa kwa uuzwaji wa filamu kutoka nje ya nchi kwa madai zinaharibu soko la ndani! Athari pekee niliyoishuhudia ni ufa uliojitokeza kati ya wasanii waliounga mkono maandamano na waliopinga, kiasi cha kuibua mihemko iliyosababisha kutishiana maisha na kutukanana matusi ya nguoni.

Kwa sasa Sekta ya filamu Tanzania ipo ‘Babeli’ ingawa ilifikia hatua ya kutingisha Afrika. Sidhani kama kuna mtu atabisha kuwa filamu za kibongo ‘hazikutesa’ Afrika Mashariki na nchi za Maziwa Makuu. Filamu hizi zilisaidia kwa kiwango fulani kuitangaza Tanzania na kuwatangaza wasanii wa nchi hii. Sinema hizi ziliuzwa kwa wingi mitaani, watu walizichangamkia; wanawake na vijana ndio wakiwa wateja wakubwa wa sinema hizi.

Uchumi wa soko huria la filamu ulichangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa sinema za Kiswahili. Ilikuwa ukipita mitaa ya jiji la Dar es Salaam au katika miji mikubwa unaona mabanda ya kuoneshea video yametapakaa kila kona. Pia unakutana na wauzaji wa filamu wakitembeza barabarani.

Na kwa tuliopata bahati ya kutembelea nchi jirani za Kenya, DR Congo, Rwanda, Burundi na kadhalika, tunathibitisha kuwa filamu hizi zilitesa sana maeneo hayo. Lakini sasa hali imebadilika!

Inawezekana filamu zinazotoka nje ya nchi zimechangia kuharibu soko la filamu za ndani, lakini kabla wasanii hawajaandamana kushinikiza kusitishwa kwa uuzwaji wa filamu kutoka nje ya nchi walipaswa kutoa kwanza boriti kwenye macho yao ndipo watazame kibanzi kwenye macho ya wengine.

Utoaji wa filamu zetu ndio umelifikisha soko la filamu hapa, maana ulikuwa ni kama soka bila refa, mkutano bila mwenyekiti, darasa bila mwalimu, au nyumba (familia) bila mzazi…

Wasanii waliwaamini sana wafanyabiashara, waliahidiwa milioni kadhaa kwa sinema; watengenezaji sinema wakawa wanalipua kazi; waigizaji hawalipwi vizuri; utengenezaji sinema ukafanywa haraka haraka. Sinema zikatengenezwa kwa siku tatu hadi wiki moja, na ndani ya mwezi mmoja tu ziko sokoni. Haraka haraka…

Wasanii wa filamu wakaigiza bila script wala mazoezi, baadhi ya watengenezaji filamu wakatumia mwanya huo kula uroda na wasichana warembo (na Umiss ukawa kigezo kikubwa cha kupata nafasi ya kucheza filamu, haijalishi ana kipaji cha kuigiza au la), baadaye wasanii wetu wakaanza kujilinganisha na Wanaijeria!

Sikatai na wala hakuna atakayebisha kuwa sinema za Nigeria zilitingisha katika nchi yetu, zilileta athari kubwa na kubadilisha tamaduni za Nigeria na Afrika. Sekta ya filamu ya Nigeria imesaidia kuleta mageuzi na kuhifadhi utamaduni wa Kiafrika pamoja na kuwepo nguvu za utandawazi.

Sikatai na wala hakuna atakayebisha kuwa sinema za Nigeria zinatumia lugha za asili za Nigeria kusimulia habari za Afrika. Ni kweli kuwa lugha na utamaduni wa watu ni muhimu katika utambulisho wao na matarajio yao kwa ajili ya kujitawala.

Aidha, sikatai na wala hakuna atakayebisha kuwa sinema za Nigeria zinaelezea maisha ya jadi, mchanganyiko na ya kisasa ya watu wa Nigeria. Lakini kwanini wasanii wetu walizitumia kama kipimo chao cha filamu? Kwanini waliamua kufuata nyayo za Wanaijeria katika kuzalisha sinema za Tanzania? Matokeo yake wakajikuta wameacha kusimulia hadithi zetu na kusimulia za Wanaijeria.

Sinema zetu zikawa zinasimulia uchawi, mapenzi au mikasa ya kijamii kama wanaijeria. Wasanii wetu wakawa wanaiga hadithi za Wanaijeria na namna yao ya uchezaji. Kwanini Watanzania wasizione sinema za Nigeria zinafaa kuliko za kwetu?

Sasa wasanii wanalalamika kuwa Watanzania hatununui sinema zinazotolewa na Watanzania wenzetu. Kwa kuwa sinema za nje zimejaa, zinauzwa bei chee na hazilipi kodi. Wanaweza kuwa sahihi. Lakini, wakumbuke ni Watanzania haohao walioacha kuangalia sinema za nje na kuzipokea sinema za ndani, na sasa wameamua kurudi kuangalia sinema za nje. Kisa? Haziwavutii tena na zinatengenezwa kwa kulipuliwa.

Lakini nimekuwa najiuliza, kwanini hata zile zinazotengenezwa vizuri bado hazinunuliwi? Kwanini hazifurahiwi? Kwanini hazitolewi maoni na hazitangazwi? Tunachokiweza ni kuziponda tu!

Na wasanii wasilalamike tu bali wakumbushane kwamba sinema ni sanaa inayochukua muda. Hawawezi kutengeneza sinema ikakamilika ndani ya wiki au mwezi mmoja tu. Wajipe muda katika kuifanya kazi kwa ufanisi zaidi. Wasiangalie kufanya kazi haraka haraka ili wapate pesa na kutatua matatizo yao. Wakumbuke kuwa ukitoa kazi nzuri yenye ubora hukaa na huuzika miaka nenda miaka rudi, tofauti na kazi ambazo baada ya wiki mbili zinakuwa hazina tena soko.

Wakumbushane kujipa muda katika uandaaji wa filamu: Mwezi mmoja wa mikutano kupanga mambo (wapi itapigwa picha, nani atafanya nini, waigizaji watatoka wapi, watafanya nini), mwezi mwingine kupanga usanii (mazoezi ya waigizaji, mazingira yao), mwezi mwingine wa kupiga picha. Baada ya miezi mitatu, mingine miwili ya kuhariri na kusahihisha makosa.

Kisha kifuate kipindi cha kuitangaza kusudi iuzwe. Ukichunguza sana utagundua kuwa sinema haiwezi kumalizika chini ya miezi sita kwa mazingira ya Tanzania. Ndiyo maana wenzetu wanatoa sinema moja tu kwa mwaka lakini pesa wanazopata wanakula kwa miaka kibao. Sisi tulikuwa tunatoa sinema kila mwezi lakini pesa yake ni ya kujikimu tu.

Kwa hoja hii, nakaribisha mjadala.

Mkuu inabidi hii nakala uwatumie wabongo movie wote including producers iwe kama Jarida naamini itawachallenge na kuleta mapinduzi.
 
Tatizo watanzania upole au sijui niseme woga ndio umetuzidi
Hakuna wa kulalamika mtu mpaka kichwa kinauma uko kimya tu
Kwa kweli sheria ingetoka wizarani kuwa ni marufuku kelele kwenye public transport

Dereva inatakiwa awe makini ajue kinachoendelea kwenye gari.
Kama kitu kimeharibika au exhaust imevunjika yeye anaenda tu ndio maana na ajali zinatokea kwa sababu hizo
Waziri husika angeambiwa

Mbona wakija Ulaya wanaona wenye heshima why kwetu na wanalifumbia macho?
Unapanda bus Ulaya au train wameandika kabisa heshimu aliekaa karibu yako punguza sauti ya simu yako kama ni mziki.
Yaani hadi raha unauchapa na usingizi bila buqhudha kabisa.
Huku kwetu wengine wanaingia na kuanza kuuza visabuni yaani ni kero tupu
Mkuu upo Ulaya au Tanzania?Maana unanichanganya.Mara "wakija" Ulaya,mara "huku"kwetu Tanzania.Umesahau ulipo au ni matumizi tu ya lugha yetu adhimu ya kiswahili yanakuchanganya?
 
Mkuu upo Ulaya au Tanzania?Maana unanichanganya.Mara "wakija" Ulaya,mara "huku"kwetu Tanzania.Umesahau ulipo au ni matumizi tu ya lugha yetu adhimu ya kiswahili yanakuchanganya?
Hahaha nimeipenda hiyo
Ni lugha adhimu, nipo kote
 
Siku hizi nimepata dawa yao:
Kwanza nna headphones kubwa zinaziba masikio hata muungurumo wa gari huwa siusikii.
Pili nikijua kesho nasafiri huwa nachelewa kurudi home mpaka saa 2200 au 2300 nikifika naanza kujiandaa kwa kupanga nini naondoka nacho.

**Nikimaliza kupanga labda ni saa 7/8usiku naanza kujiandaa kwa kuosha mwili, lengo la hii ni kutopata usingizi ili kwenye basi nakuwa full mbonji, aka kulala.

mshana jr
CHUKUA HII IKO POA.
 
Hahahahah ......kuna kampuni zinajitambua. Mwaka juzi mwishoni nikiwa natokea Mbeya kuelekea Dodoma ndani ya Swahili coach, ilikuwa ni mwendo wa hot world movies tu ikiwemo MAD MAX FURY ROAD enzi hizo bado mpyampya. I really enjoyed the journey

Sent from my SM-J710H using JamiiForums mobile app
 
Hawa jamaa kiukweli wabadilike kabisa. Huwezi ondoa bus tuu stand unaanza tafta flash ya mibongo movie. Kingine hata movie hizo walau zingekuwa na tamaduni zetu. Tamaduni zote za ulaya. Mambo yote ya nchi za watu. Unawekewa The God must be Crazy leooo!?!? Hawa jamaa wanakera sana. Laiti nchi hii ingekuwa na route za ndege mikoa yote mabasi naiman yangesubiri hasa wakati huu wa 80km/h as a speed limit. Mtu unashindwa kutafakali maisha yako. Masaa nane au sita ni mengi sana. Mm nawasihi waache kabisa kuweka mamuvi yao yanakera sana. Utaskiaaaa Ankooooo beny maraa Dokiiiiii. Mandaziii kabisa
 
Siku hizi hata housemaids wamehamia ufilipino, hawataki mchezo japo years back ndo walikua wateja wao wakuu

Do a little thing with the great love ~ Mother Theresa
Na Telemundo aisee....yan kutwaa, sio kama zamani full kumtaja kanumba tu
 
Back
Top Bottom