Mel James
JF-Expert Member
- Jun 23, 2015
- 367
- 299
Habari ya jion wakuu! Poleni na miangaiko ya leo. Nimeona niaandike habari hii maana binafsi ni mpenzi wa safari sana hasa wikiend uwa napendelea kusafiri. Mabasi mengi ya mikoan wanapendelea sana kuweka hii miziki ya bongo flavior sijui fleva.
Kwa upande wangu sikatai miziki isiwekwe hasa hii ya nyumbani lakini nawaomba sana wenye mabasi kuwa makini. Bongo fleva nyingi wanaimba matusi tena makubwa na hata uchezaji mwingine kwa kweli sio vizuri kuangalia mbele ya wazazi au watoto. Kwenye mabasi yenu watu wanasafiri na watoto wao wengine wazazi wao.
Unaweza kukaa kwenye siti na mzee mtu mzima kama mzazi wako ila unaona aibu hata kuangalia nyimbo mnazoweka. Mamlaka husika za usafiri tunaomba muingilie kati hili swala. Angalau wekeni miziki basi yenye staha kidogo hata kama wanaimba mapenzi ila wametofautiana level ya maneno hata video zao.
Wenye mabasi pia kuweni waungwana hasa makonda na madereva wekeni nyimbo ambazo hata nyie mnaweza kuangalia na watoto wenu au wazazi wenu nyumbani. Asanteni.