baz kaiza
JF-Expert Member
- Jan 27, 2015
- 11,576
- 12,290
Eti Nape ni waziri,
Unategemea nini kutoka kwa zwazwa kama huyu?
Mwenyewe nilishangaa kumuona Nape eti waziri nchi hii kila kitu kinawezekana
Eti Nape ni waziri,
Unategemea nini kutoka kwa zwazwa kama huyu?
Mkuu hili ni janga,hawa jamaa wanakera sana kwenye maadili.Kama bongo move wanataka kukamata soko waangalie zaidi mila na desturi za kitanzania,waache kuiga tamaduni za nje ili kujitofautisha,tamaduni zetu zinaweza kukamata soko(create own style)
Yah na watanzania wameshawachoka ndugu zetu sijui itabidi watumie njia gani!ila ukweli Watanzania ni rahisi saana kuwateka kwenye sanaa ila ni ngum sana kuwarudishwa wakikupotezea.
Na mimi haliniathiri hata kidogo,waandamane hadi kwa maguPole zenu mnaonunua movies K/Koo..
Wenzenu nikiwemo mimi napakua series zangu za kikorea mwenyewe.
Hivyo hilo suala halitoniathiri hata chembe.
Leo nilikuwa napitapita Kariakoo katika maduka ya movies na series za nje hasa za Kikorea, Hollywood Bollywood, China na hata Nigeria, ila cha ajabu nikakutana na hali ya kushangaza kabisa pale. Maduka yote yanayouza movies hizo nikakuta yamefungwa tofauti na siku za nyuma,kwamba kila siku yalikuwa wazi, nikajaribu kudadisi nikaja kupata sababu kuwa ni Bongo Movies ndio waliofanya maduka yale yafungwe kwa maandamano wakidai kuwa Filamu zao zimekuwa haziuziki sokoni na kuwa zinazouzika sana ni hizo za nje tu.
Hivyo wanahitaji soko la filamu za nje lifungwe, ili wao watuuzie hizo filamu zao! Nikashangaa! Ina maana hawa jamaa wameiga ile action ya Magufuli ya kufunga masoko ya nje ya viwanda vya sukari, ili kuvipa mwanya viwanda vya ndani viuze! Nikashangaa ina maana na hizi movie, za nje nazo ni majipu!Hivi inawezekana kweli?
Leo Mheshimiwa akasimama na kutoa rai kuwa nyimbo zote za nje ya nchi zifungiwe kupigwa Tanzania ili hawa kina Diamond wapate mwanya wa kutuuzia zao humu vizuri.Kivipi kama wanatuimbia Pumba? Wana Bongo movie iweje waanze kubana soko la kazi za wenzao wa nje zisiuzwe Tanzania na movies zao zenyewe ni aibu kwa asilimia nyingi tu!Itawezekanaje suala la kubana uingizaji wa kazi kutoka nje kuingia Tanzania hadi kwenye Burudani?
Wakati watu tulionao humu uwezo wao bado ni local!Njia nzuri ni wao kupinga wizi wa kazi zao na kupanga mipango mahususi itakayowawezesha wao kushindana na hilo soko na si kupinga uuzaji wa kazi za wenzao ili watuuzie zao huko ni kukimbia ushindani.
Ndugu yangu mimi si mnafiki na sijasema kiupendeleo ila nawakosoa sababu wanakosea na ndio maana mwisho wa thread yangu nimesema wazi kuwa suala ambalo ndugu zetu wanapaswa kufanya na kulihangaikia ni juu ya kupinga piracy ya kazi zao, maana inajulikana wazi kuwa wanaibiwa mno!Kuna wakti unaweza ukaleta uzi humu jamvini ukaonekana ni kituko au hujui chochote ni vyema kabla hujaaweka andiko ulitathimini kwa kina ili usindike kinafiki au kishabiki, hizo cd za nje zimechangia nn kwenye uchumi wa taifa lako? kwa kiasi gani kazi za wasanii wetu zinachezwa au kuuzwa nje ya nchi kama zao kwetu?fikiria umekesha studio au location umetoa hela kibao kufanikisha kazi yako harafu mjinga mjinga fulani hv yuko sebuleni kwake na machine yake ya kudurufu anatandika copy zako tu kirahisi rahisi tu utazani zake, jifunze kuheshimu kazi za wengine kumb, hapo ndipo wanapopatia mkate wa sku, tufanye kazi vya bure vimeisha.
Hakika!acheni kupotosha bongo movie hawana uwezo wa kuzuia maduka ya kuuza dvd za nje yafungwe kama kweli wanataka waende mlimani city na majumba mengine ya sinema, kilichosababishwa yafungwe ni kudaiwa kuweka sitika za cosota na TRa kama taratibu zinavyoelezwa
Wamefungiwa kwakuwa wameshindwa kufata utaratibu hakuna mtu aliye zuiwa kuingiza movie nje bali unachotakiwa ili ufanye biashara ya kuuza lazima uwe na vibali pia na sticker za TRAWatanzania tumelala sana !
kila kitu cha nje tunakiogopa kwa kuhofia ushindani hata kwenye sukari sikwambii magari..
tutafungia kila kitu cha nje na mwishoe tutashindwa kuingia kwenye masoko ya biashara ya kimataifa..
tutaishia kufanya biashara kati ya ngosha na mkwere.
Movie zao siyo nzuri hazina hata uhalisia nani azinunue???? Hata wakifunga tutadownload tuuu
Mamlaka ya kufunga maduka wanayo? Au ndio hearsay tu. Nina wasiwasi na hii thread huenda ikawa ni uzushi tu.
Wafunge hata torrent sites kama wanaweza ***** zao%
Mimi movie za kibongo huwa siangaliagi kabisa manake hazina mvuto hata kidogo movie nzur labda ni siri ya mtungi ndo huwa naifatilia kidogo Ile series imenipa ushawishi kwa mbali.
Nikweli Tanzania haina kiwango cha kuingiza na kuimba so waangalie tu kaz zao zisipate kuibiwa
Move za kibongo sizielewi kabisa Na uwaga siziangalii
Nina kasema wamefungia filamu za nje kuingizwa nchini? Kinachotakiwa ni wao kufata utaratibu wa kuuza filamu lazima wapitie TRA na Cosota....Watapata wapi changamoto zitakazowawezesha kuboresha kazi zao? Vifungiwe basi hata vitabu vya hadithi za nje maana kuna wakati watu hufanya editing ya story au movies za zamani na kudai wametunga.
Imani yangu ni kuwa ushindani hupelekea kuzalisha bidhaa bora ili kuendana na kasi ya soko.
mmmmmmh!! TRA wafanye kazi yao ila bila utaratibu itakuwa nuksi tu! halafu waigizaji wa bongo movies waache kuigiza chini ya viwango uwezo wanao ila hawana wataalum wanaojua movie ni nn..ndo maana wote wanaiga kujichubu..kuongea sauti ambazo si zao..kingereza kibovu..maudhui ndo hovyo kabisa aibuuuu...bongo movies zote zifungiwe ili wajue wanaharibu waje upya kivingine twaweza elewa!..
Ninacho kulaumu kwenye hii thread ni wewe kupotosha na kusababisha kila mtu anaye changia hii thread kudhani serikali inazuia uingizwaji wa movie za nje kitu ambacho sicho kabisa!Secret Star kwanini unasema uongo? Swala hili halikuanza awamu ya Magufuli bali lilianza kitambo na wauzaji wanajua fika kuwa wanatakiwa kuwa na vibali kutoka COSOTA ili waweze kuuza movie za nje humu nchini?COSOTA na TRA wanashirikiana kuhakikisha kila wanao uza movie kutoka nje wana vibali na pia ni movie original na si fake!
Ukiingiza mzigo wa movie kutoka nje kabla ya kuanza kuuza unatakiwa kupata kibali kutoka COSOTA na mzigo wako uta hakikiwa na pia utabandikwa sticker za TRA.
Lengo ni jema tuu kwa kuwa litasaidia kuondoa movie zisizo kidhi viwango na ambazo hazina vibali na zile fake(CD)....!
Wauzaji wanacho lalamikia ni masharti ya kupata leseni ya kuuza movie za nje maana wengi wao walikuwa wanauza tuu bila vibali au kukaguliwa na wengi wao mizigo yao imekamatwa....