Secret Star
JF-Expert Member
- Jul 1, 2011
- 1,724
- 1,646
Leo nilikuwa napitapita Kariakoo katika maduka ya movies na series za nje hasa za Kikorea, Hollywood Bollywood, China na hata Nigeria, ila cha ajabu nikakutana na hali ya kushangaza kabisa pale. Maduka yote yanayouza movies hizo nikakuta yamefungwa tofauti na siku za nyuma,kwamba kila siku yalikuwa wazi, nikajaribu kudadisi nikaja kupata sababu kuwa ni Bongo Movies ndio waliofanya maduka yale yafungwe kwa maandamano wakidai kuwa Filamu zao zimekuwa haziuziki sokoni na kuwa zinazouzika sana ni hizo za nje tu.
Hivyo wanahitaji soko la filamu za nje lifungwe, ili wao watuuzie hizo filamu zao! Nikashangaa! Ina maana hawa jamaa wameiga ile action ya Magufuli ya kufunga masoko ya nje ya viwanda vya sukari, ili kuvipa mwanya viwanda vya ndani viuze! Nikashangaa ina maana na hizi movie, za nje nazo ni majipu!Hivi inawezekana kweli?
Leo Mheshimiwa akasimama na kutoa rai kuwa nyimbo zote za nje ya nchi zifungiwe kupigwa Tanzania ili hawa kina Diamond wapate mwanya wa kutuuzia zao humu vizuri.Kivipi kama wanatuimbia Pumba? Wana Bongo movie iweje waanze kubana soko la kazi za wenzao wa nje zisiuzwe Tanzania na movies zao zenyewe ni aibu kwa asilimia nyingi tu!Itawezekanaje suala la kubana uingizaji wa kazi kutoka nje kuingia Tanzania hadi kwenye Burudani?
Wakati watu tulionao humu uwezo wao bado ni local!Njia nzuri ni wao kupinga wizi wa kazi zao na kupanga mipango mahususi itakayowawezesha wao kushindana na hilo soko na si kupinga uuzaji wa kazi za wenzao ili watuuzie zao huko ni kukimbia ushindani.