Bongo movie aibu tena

Bongo movie aibu tena

wamesha kunywa maji ya ray yale na viroba hao kwani lazima kuangalia movie zao za kutuanikia mapaja nje wakitaka vya nje vifungwe wasivae nguo za nje wavae kama mpoto ivi kwa mfano movie za hawa dada zetu wakaa uchi nani anazitaka wajipange aisee atununui ng'o
 
basiii waruhusu tuangalie bunge live,maana tunakoendea huko ni kubaya zaidi movie zenyewe za bongo hazina mvuto
 
Ninacho kulaumu kwenye hii thread ni wewe kupotosha na kusababisha kila mtu anaye changia hii thread kudhani serikali inazuia uingizwaji wa movie za nje kitu ambacho sicho kabisa!

Serikali inacho hitaji ni kufuatwa utaratibu wa uuzwaji wa na sio movie za nje maana hata movie za ndani zisizo na vibali au sticker zimekamatwa..!
Na hiki ndicho kitu halisi, na ni jambo jema sana, lakin naona watu fulan kwa manufaa yao wenyewe wadanganya watu wazima ,na kuifanya ionekane kwamba serikali inachofanya si sahihihi.

Ni udanganyifu, na asilimia 90 ya wachangiaji wamechangia ktk uelewa ulio potoka,

Mods fungia huu uzi au uwekwe sawa
 
Tatizo ni huyo dikteta hapo magogoni yeye akiamua kila mtu anakurupuka hata majadiliano hakuna.
Haya yanatokea kwa msukumo wa wauza papa Wa bongo movie. Soko lao ni kubwa sana ila linaangushwa na vibanda vya kukodisha bongo movies uswahilini. Yaani movie mpya ikitoka tu fasta watu wanaenda kuikodi vibandani. Yaani mtu ameona movie zote za bongo movie lakini zote hajanunua hata moja.

Watafute suluhisho LA matatizo yao wasije kuwa kama bongo flava walilia studio wakapewa lakini bado wanalia.

Wasitujengee chuki sisi hatuna tatizo nao wasitulazimishe tuuze kazi zao kwani hao wanaowauzia wanatosha sana tu.
 
Leo nilikuwa napitapita Kariakoo katika maduka ya movies na series za nje hasa za Kikorea, Hollywood Bollywood, China na hata Nigeria, ila cha ajabu nikakutana na hali ya kushangaza kabisa pale. Maduka yote yanayouza movies hizo nikakuta yamefungwa tofauti na siku za nyuma,kwamba kila siku yalikuwa wazi, nikajaribu kudadisi nikaja kupata sababu kuwa ni Bongo Movies ndio waliofanya maduka yale yafungwe kwa maandamano wakidai kuwa Filamu zao zimekuwa haziuziki sokoni na kuwa zinazouzika sana ni hizo za nje tu.

Hivyo wanahitaji soko la filamu za nje lifungwe, ili wao watuuzie hizo filamu zao! Nikashangaa! Ina maana hawa jamaa wameiga ile action ya Magufuli ya kufunga masoko ya nje ya viwanda vya sukari, ili kuvipa mwanya viwanda vya ndani viuze! Nikashangaa ina maana na hizi movie, za nje nazo ni majipu!Hivi inawezekana kweli?

Leo Mheshimiwa akasimama na kutoa rai kuwa nyimbo zote za nje ya nchi zifungiwe kupigwa Tanzania ili hawa kina Diamond wapate mwanya wa kutuuzia zao humu vizuri.Kivipi kama wanatuimbia Pumba? Wana Bongo movie iweje waanze kubana soko la kazi za wenzao wa nje zisiuzwe Tanzania na movies zao zenyewe ni aibu kwa asilimia nyingi tu!Itawezekanaje suala la kubana uingizaji wa kazi kutoka nje kuingia Tanzania hadi kwenye Burudani?

Wakati watu tulionao humu uwezo wao bado ni local!Njia nzuri ni wao kupinga wizi wa kazi zao na kupanga mipango mahususi itakayowawezesha wao kushindana na hilo soko na si kupinga uuzaji wa kazi za wenzao ili watuuzie zao huko ni kukimbia ushindani.


Kwa kuchangia kidogo hapo, mi nafikili hakuna ubaya kwenye hilo, kilicho muhimu kwetu ni kutengeneza filamu zenye ubora wa hali ya juu ili tuweze kupata kipato ambacho kitatufanya tuweze kushindana na hao wa mbele. Na nafikiri hiyo ndiyo sababu kubwa ya kuzuia filamu za mbele zisiingie kwa wingi mdau.
 
Back
Top Bottom