Bongo movie aibu tena

Bongo movie aibu tena

Watanzania tumelala sana !
kila kitu cha nje tunakiogopa kwa kuhofia ushindani hata kwenye sukari sikwambii magari..
tutafungia kila kitu cha nje na mwishoe tutashindwa kuingia kwenye masoko ya biashara ya kimataifa..
tutaishia kufanya biashara kati ya ngosha na mkwere.
 
Movie zao siyo nzuri hazina hata uhalisia nani azinunue???? Hata wakifunga tutadownload tuuu
 
Mamlaka ya kufunga maduka wanayo? Au ndio hearsay tu. Nina wasiwasi na hii thread huenda ikawa ni uzushi tu.
 
Bado nina wasiwasi na utashi wa baadhi ya viongozi wa awamu hii, na nilihisi hili baada tu ya kutangaza baraza la mawaziri na utendaji wao usio na dira. Mwisho watasema ni marufuku kuangalia mipira ya nje.

Wakukurupuka style.....

Kazi ipo divai mpya viriba vya zamani...
 
Mimi movie za kibongo huwa siangaliagi kabisa manake hazina mvuto hata kidogo movie nzur labda ni siri ya mtungi ndo huwa naifatilia kidogo Ile series imenipa ushawishi kwa mbali.
 
Nikweli Tanzania haina kiwango cha kuingiza na kuimba so waangalie tu kaz zao zisipate kuibiwa
 
Watapata wapi changamoto zitakazowawezesha kuboresha kazi zao? Vifungiwe basi hata vitabu vya hadithi za nje maana kuna wakati watu hufanya editing ya story au movies za zamani na kudai wametunga.
Imani yangu ni kuwa ushindani hupelekea kuzalisha bidhaa bora ili kuendana na kasi ya soko.
 
Mamlaka ya kufunga maduka wanayo? Au ndio hearsay tu. Nina wasiwasi na hii thread huenda ikawa ni uzushi tu.
NI KWELI MKUU NIMESIKIA KWENYE REDIO HALAFU HAO WA KWNYE MADUKA YA MUVI ZA KIKOREA MBONA LESENI ZA BIASHARA WANAZO KWANINI WAZUILIWE
 
Hivyo wanahitaji soko la filamu za nje lifungwe, ili wao watuuzie hizo filamu zao! Nikashangaa! Ina maana hawa jamaa wameiga ile action ya Magufuli ya kufunga masoko ya nje ya viwanda vya sukari, ili kuvipa mwanya viwanda vya ndani viuze! Nikashangaa ina maana na hizi movie, za nje nazo ni majipu!Hivi inawezekana kweli?


Walianza na Bunge kutokuwa live, sasa dalili ndizo hizo za kupangiwa aina ya burudani...., let us wait
 
Jaman muv za kibongo....nikikumbuka yule jambaz aliemvamia iren kisha akavua viatu ndo akaingia ndan sion sababu ya kulazmisha tuzinunue
 
WAACHANE NA MAMBO YA PART ONE NA TWO AMBAPO UKIANGALIA MOVIE INAMATANGAZO KAMA ISHIRIN ALAFU MOVIE YENYEWE UNAANGALIA DAKIKA 15 IMEISHA ALAFU HAINA MVUTO UKIONA KASHA TU BAAS UMESHAJUA MOVIE IMECHEZWAJE TUPO KOREA BANA VITU VYA UKWEL MKIWEZA KUIGIZA HIVYO NA ZIWE NDEFU TUTANUNUA
 
THT, Bolingo movi, Clouds, COSOTA, ....naona kuna vitu havipo sawa up-stairs... Missing a target!
 
!
!
Mimi naiona fursa sasa hapa kwa wauzaji wa filam za nje. Kinachitakiwa sasa ni kuinvest katika ujuzi wa kudownload na black market. Kimsingi mimi kama mdau wa muvie sinunui cover kwa hiyo hata kwenye flash tu naibeba naenda nayo. Au tutumiane kwenye telegram. Haitahitaji kibanda kikubwa ni wewe laptop yako modem ya halotel labda na simu tu. Selikali kwa maana ya cosota na tra unawazunguka tu kama huna akili nzuri. Wakijifanya wehu ni bora tukawa wehu mara mbili zaidi.

Haulijui soko la movie la Tanzania wstu wanaangalia cover la movie ndo anashawishika kununua movie
 
Leo nilikuwa napitapita Kariakoo katika maduka ya movies na series za nje hasa za Kikorea, Hollywood Bollywood, China na hata Nigeria, ila cha ajabu nikakutana na hali ya kushangaza kabisa pale. Maduka yote yanayouza movies hizo nikakuta yamefungwa tofauti na siku za nyuma,kwamba kila siku yalikuwa wazi, nikajaribu kudadisi nikaja kupata sababu kuwa ni Bongo Movies ndio waliofanya maduka yale yafungwe kwa maandamano wakidai kuwa Filamu zao zimekuwa haziuziki sokoni na kuwa zinazouzika sana ni hizo za nje tu.

Hivyo wanahitaji soko la filamu za nje lifungwe, ili wao watuuzie hizo filamu zao! Nikashangaa! Ina maana hawa jamaa wameiga ile action ya Magufuli ya kufunga masoko ya nje ya viwanda vya sukari, ili kuvipa mwanya viwanda vya ndani viuze! Nikashangaa ina maana na hizi movie, za nje nazo ni majipu!Hivi inawezekana kweli?

Leo Mheshimiwa akasimama na kutoa rai kuwa nyimbo zote za nje ya nchi zifungiwe kupigwa Tanzania ili hawa kina Diamond wapate mwanya wa kutuuzia zao humu vizuri.Kivipi kama wanatuimbia Pumba? Wana Bongo movie iweje waanze kubana soko la kazi za wenzao wa nje zisiuzwe Tanzania na movies zao zenyewe ni aibu kwa asilimia nyingi tu!Itawezekanaje suala la kubana uingizaji wa kazi kutoka nje kuingia Tanzania hadi kwenye Burudani?

Wakati watu tulionao humu uwezo wao bado ni local!Njia nzuri ni wao kupinga wizi wa kazi zao na kupanga mipango mahususi itakayowawezesha wao kushindana na hilo soko na si kupinga uuzaji wa kazi za wenzao ili watuuzie zao huko ni kukimbia ushindani.
Usiongee kitu usichokijua....
 
Sababu za kufunga ni kwamba hazina stika za TRA (hawalipi kodi) na hii ni mpaka kwa baadhi ya muvi za kibongo zimekutwa hazina stika pia.
 
Nachoweza angalia bongo movie ni upande. Wa comedy tu hizo filamu siziwez,nadhan maji wanayokunywa kUwafanya wawe weupe Sasa yamekimbilia kwenye ubongo yanawavuruga,watawezeje kupambana na kaz za nnje wakat film. Zao no kutuonyesha mapaja na kuonyesha magar. Na majumba,yan tangu kanumba aondoke wana bongo movie wamekuwa kama meli ilozimika baharin inapelekwa tu na upepo,hivi wanaweza act kama movie za nnje ,huku ni kutotutendea haki wapenzi wa movie tz,alozifunga afikirie tena mahamuz yake
 
Back
Top Bottom