Bongo- Ivi N' Kwanini?!

Kana-Ka-Nsungu

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,257
353
Ni vijiswali tu ambavyo huwa najiuliza mara kwa mara na labda na wewe una vyako, unaruhusiwa kuviongeza hapa chini:

Hivi n' kwanini..............

-Mtu anatumia simu ya blackberry kwa kupiga na kupokea tu na hajui kutumia function nyingine yoyote?

-Mtu siku zote anakunywa safari lakini akizifumania anahamia kwenye Heinneken?

-Mtu unaishi Temeke lakini kila siku unashinda Masaki na Oysterbay?

-Mtu ukiwa hata mwendawazimu lakini unaongea kiingereza watu wanafikiri umesoma sana?

-Mtu ukiwa unaishi 'majuu' watu wanadhani una mihela ya kumwaga?

-Mtu anaona kula chips kuku kila siku ni ufahari?

-Mtu usipomnunulia kadi ya valentine demu wako anakumwaga?

-Mtu ni Rais na kila mwezi akiongea na wananchi haongelei yale watu wanayotaka kumskia akiyaongelea?

-Mtu umetuhumiwa kutenda kosa, hakuna hata ushahidi, lakini polisi wakija kukukamata lazima wakupige kwanza na ulale ndani?

-Mtu unaendesha gari lako, traffic lights zinafanya kazi, lakini polisi ndo anaongoza magari?

Hivi n'kwanini jamani????
 
mimi wapenzi wangu siwanunulii kadi ya valentine na hawaniulizi,na wananipenda ajabu,
 
ni kwa sababu hii ni nchi ambamo watu hawafuati sheria, serikali legelege, viongozi wezi wanachaguliwa kuongoza taifa na asasi zake.
 
Watu wa Nchi hii wanapenda sifa saaana,unakuta mtu ananunua kitu kwa hela nyingi sana halafu hakitumii ipasavyo!!
 
-Hivi n'kwanini mwanaume akifuga rasta anaonekana ni muhuni?
-Hivi n'kwanini wanaume hawapendi kutoka sehemu mbalimbali za starerehe na wapenzi/wake zao?
-Hi n'kwanini wanaume hawaachi hela ya mboga nyumbani lakini wakiwa kwenye mabaa kuchoma kuku na mbuzi hawaoni uvivu?
 
-Mtu anakojoa katikati ya jiji wakati vyoo vipo!
-Mtu anatupa taka popote katikati ya jiji wakati mabini yapo!
-Umeme umekatika most of the time lakini bill ikija inatisha!
-Bomba halijawahi toa maji tangu limewekwa lakini bill zinakuja kila mwezi!
-Uki top up simu yako then ukajitusu kupiga kwenye mtandao mwingine umekwisha!

Hivi n'kwanini jamani??????
 
-mtu anakojoa katikati ya jiji wakati vyoo vipo!
-mtu anatupa taka popote katikati ya jiji wakati mabini yapo!
-umeme umekatika most of the time lakini bill ikija inatisha!
-bomba halijawahi toa maji tangu limewekwa lakini bill zinakuja kila mwezi!
-uki top up simu yako then ukajitusu kupiga kwenye mtandao mwingine umekwisha!

Hivi n'kwanini jamani??????


mi nafikiri we unapitia mid life crisis.
 
Hivi n'kwanini........

Abiria wa mabasi yaendayo mikoani wanakuwa wakali iwapo dereve anaenda kwa mwendo wa taratibu na salama? Akienda kwa kasi na akaovertake basi jingine utawaona wanakenua meno yao na wengine kushangilia!!Lakini ajali ikitokea kila mtu anamlaumu dereva?

Hawa madereva nao, safari hata ya Dar- Tunduma, dereve huyohuyo mmoja zaidi ya masaa kumi na hata hapumziki, na ukikagua leseni yake unagundua kuwa ni feki lakini bado anaruhusiwa na mamlaka husika acheze bahati nasibu za maisha ya watu zaidi ya 60? Kwa mtaji huu ajali zitaacha kumaliza kweli?

Hivi n'kwanini jamani????
 
Hivi n'kwanini watu wengi hawakumbuki birthdays za ndugu zao ie. mama, kaka, dada, etc lakini wanakumbuka zile za wapenzi wao? Na ikitokea ukasahau ya mpenzi basi inakuwa ni tafrani kwelikweli!
Hivi n'kwanini?
 
Hivi kwa nini polisi wanakuchukua kwa maelezo kwamba ukaisaidie polisi kutokana ishu ambayo wanadhani unaifahamu, halafu badala ya kukuweka kwenye mazingira mazuri ya kutoa msaada, wanakutupa selo?

Hivi kusaidia polisi ni kosa?
 
Hivi ni kwanini mtu akiwa na mkewe kwenye gari hakuna vicheko, lakini akiwa na nyumba ndogo...ni tihii...tehee....tuk..tuk...tuk!!!
 
mtu anajenga choo, mbele ya mlango wako ukilalamika anasema ni kiwanja chake ana haki ya kujenga anachotaka

watu kila siku wanalalamika daladala zinajaza abiria kama makopa kwenye gunia, lakini wakiona daladala imejaa wanazidi tu kujisunda ndani hukku wakimlaumu konda

watu wanalalamika kila siku rushwa na kujuana kumekithiri maofisini, lakini wakifika ofisi za serikali badala ya kupanga foleni wahudumiwe, wanawatafuta wawajuao au wanaangaza angaza wapi pa kupenyeza rupia wakisababisha waliowahi kwenye foleni wasubiri mda mrefu zaidi

ive n'kwanini?!
 
Hivi n'kwanini mtu umepata ajali mbaya, watu wakikumbiza hospitali-wauguzi wanakataa kukupatia matibabu eti hadi uwe na PF3? na ukienda huko polisi kufuata hiyo PF3 polisi wanakuzungusha hadi utoe chochote ndo uipate? Kwanini in emergencies watu wasitibiwe bila hayo makaratasi, uhai wa mtu si muhimu kuliko paper work?
Hivi n'kwanini jamani????
 
Back
Top Bottom