Bongo Fleva tulipotoka na tunapoelekea

Mawawa

Senior Member
May 2, 2020
130
250
Kwa miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia wimbi kubwa la wasanii wakifanya vizuri hasa kwenye soko la ndani. Wapo waliokuja wakajaribu bahati zao wakatoa hit song mbili tatu wakapotea. Wapo waliokomaa na gemu mpaka sasa tuna enjoy kazi zao hawa tunawaita wakongwe

TULIPOTOKA. Miaka ya nyuma kabla ya hichi kizazi cha kina mondi, kiba etc hakijaja muziki wetu ulikuwa na ushindani wa hali juu, kwa upande wangu kile ndiyo kizazi bora cha muziki wa bongo fleva mpaka nitakapo ingia kaburini. Wale ndio walitengeneza ramani nzuri ya muziki wetu matunda wanafaidi hawa wa sasa

TULIPO. kwa sasa ni dhahiri muziki wetu umepoteza dira haujulikani unaelekea wapi, ni kweli wasanii wazuri wapo tena wengi tu..je! Shida ni nini mbona hawafiki kule tunapo pataka?

KINACHO UWA MUZIKI WETU.
1. MEDIA.Hakuna asiye jua kuwa media zina mchango mkubwa sana kwenye mziki wetu, achilia mbali mitandao ya kijamii. Ni ajabu kusikia eti media ina bifu na msanii hapa ndio tumejiloga wenyewe. TUBADILIKE.

2. TEAMS. Hapa ndio tumejichimbia kaburi kabisa, hapa namaanisha team wasafi, kiba na sasa ivi imeibuka team konde. Hata ikitoke msanii labda kutoka konde anawania tuzo fulani basi hatopata sapoti kutoka team wasafi, hizi team zimepandikiza chuki ya hatari mioyoni mwetu na ndio zimegawa hata media. TUBADILIKE.

MWISHO. Kama tutaungana pamoja kama wadau na kuweka pembeni utimu nauwona muziki wetu mbali sana vipaji tunavyo vingi sana tatizo ni umimi.

Ahsanteni.
 
May 16, 2020
88
125

Nigeria waliamua kuipeleka Afrobeats Marekani na wameanza kufanikiwa(Wizkid,Davido,Burna Boy ni mfano)
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
27,998
2,000
Je! Sisi tutumie njia zipi ili tuweze kufanikiwa kama wenzetu.
Njia tayari zipo ila tunatakiwa kuwa na genre yetu ambayo ndio kwanza tumekazana kuichakachua. Huwezi sema unaipeleka bongo flava Marekani wakati ikiwa typically ina vionjo vya Nigerian beats.

Bongo flava ilikuwa ina taste ya pekee kabla haijaanza kuchanganywa na manyimbo ya south africa na kisha Nigeria.

Ile bongo flava halisi iko kwa wakongwe kina P-Funk ndio walitakiwa wasambaze Original production kits kwa ma producer wapya kwa ajili ya kutengeneza nyimbo zenye vionjo halisi.

Tukiweza kuipenyeza mainstream kupitia platform mbali mbali kama akina Spotify, iTunes, Deezer, Youtube n.k naamini tutafika mbali zaidi.
 
Nimekubali ushauri mzuri
 
nguvu

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
9,154

Juu umesema inabidi tuwe na genre yetu halafu hapohapo unasifia bongo fleva ya zamani, ila nikwambie bongo fleva ya zamani ilikuwa hip hop na r&b ambazo chumbuko lake ni marekani
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
27,998
2,000
Juu umesema inabidi tuwe na genre yetu halafu hapohapo unasifia bongo fleva ya zamani, ila nikwambie bongo fleva ya zamani ilikuwa hip hop na r&b ambazo chumbuko lake ni marekani
kwahio unaona bongo fleva ya leo iko sawa kuliko ya early 2k? kila mtu ana sikio lake ila mi naona bongo fleva ya zamani iko so original. Nyimbo pia zilikuwa zinaongelea vitu vya kueleweka haijalishi ni za ku party au story au ushauri flani.

Sasa bongo fleva ya sahizi ninys kusample nyimbo za Nigeria. Davido katoa IF Diamond kai sample ikawa Eneka.

Burna boy katoa nyimbo yake Diamond kai sample kuwa Baba Lao. Inshort mziki umekuwa wa kuchakachua sana. Bongo fleva halisi iko kwa ma producer wachache sana kwa leo nyimbo ziko za kufanana fanana mno
 
nguvu

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
9,154
2,000
kwahio unaona bongo fleva ya leo iko sawa kuliko ya early 2k?
Hapana, ya zamani ilikuwa tamu ila genre haikuwa yetu tulitoa USA, angalia alipoanzia jaydee, uniq sisters, sister p, gangwe mobb, university conner, sgf, mabaga fresh halafu uone kama haikuwa USA genre, mi naona tumetoka USA tumekuja Afrika lakini bado hatuko kwenye vyetu
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
27,998
2,000
Hapana, ya zamani ilikuwa tamu ila genre haikuwa yetu tulitoa USA, angalia alipoanzia jaydee, uniq sisters, sister p, gangwe mobb, university conner, sgf, mabaga fresh halafu uone kama haikuwa USA genre, mi naona tumetoka USA tumekuja Afrika lakini bado hatuko kwenye vyetu
Ila mziki ulikuwa mzuri mkuu, sio sawa na sasa! Kwa graph naona ni kama mziki wetu unaenda shimoni na hakuna wa kuzuia hilo. Umebakia ushabiki wa kitimu tu hamna la maana. kila kinachotoka wasafi ndio kinaonekana bora, kuna watu wengine wanaimba vizuri zaidi ila ndio kama hawaeleweki.
 
el_magnefico

JF-Expert Member
Nov 6, 2015
442
1,000
kwahio unaona bongo fleva ya leo iko sawa kuliko ya early 2k? kila mtu ana sikio lake ila mi naona bongo fleva ya zamani iko so original. Nyimbo pia zilikuwa zinaongelea vitu vya kueleweka haijalishi ni za ku party au story au ushauri flani.

Sasa bongo fleva ya sahizi ninys kusample nyimbo za Nigeria. Davido katoa IF Diamond kai sample ikawa Eneka.

Burna boy katoa nyimbo yake Diamond kai sample kuwa Baba Lao. Inshort mziki umekuwa wa kuchakachua sana. Bongo fleva halisi iko kwa ma producer wachache sana kwa leo nyimbo ziko za kufanana fanana mno
Sijui unamaanisha muziki wa zamani ulikuwa mzuri sababu watu walitumia nguvu sana lakini sasa mambo yamebadilika unaweza wewe usiwe shabiki wa muziki wa sasa ila mashabiki wengine wakawepo.
Na inawezekana ukawepo utata kuwa bongo fleva haswa na ipi!!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom