Bomu linalomwandama Magufuli | Page 5 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bomu linalomwandama Magufuli

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by EasyFit, Sep 19, 2015.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2015
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,263
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Habari hii ilichapishwa kwenye gazeti la RAI miaka michache iliyopita ikisomeka...

  Huyu Ndiye Pombe Magufuli:

  - Wasema nyumba 8,000 kauza kwa mkono wake mwenyewe
  - Apuuza maonyo ya wataalamu- Mafaili ya Sundi na Musa aliyabeba kwapani

  ALIYEKUWA Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, katika Serikali ya awamu ya tatu, aliteka madaraka na kuwa mwenyekiti wa zoezi la kuuza nyumba za serikali ambazo hadi sasa, zimeshauzwa 8,288 imefahamika.

  Habari zilizopatikana ndani ya wakala wa Majengo ya Serikali (TBA), zimethibitishia Rai wiki hii kwamba Magufuli alihakikisha anashiriki kama Mwenyekiti katika zoezi zima la kuuza nyumba, ambalo kimsingi lilistahili kusimamiwa na Mtendaji Mkuu wa TBA.

  Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari ndani ya TBA, Magufuli alifanya kila aina ya ‘fujo’ katika zoezi la kuuza nyumba hizo, wakati mwingine akibatilisha maamuzi yaliyofanywa na Kamati ya TBA ya kuuza nyumba hizo, akiwapangia watu nyumba kwa utashi wake na wakati mwingine akiwakemea wale wote waliomshauri kinyume na matakwa.

  Ni chini ya utaratibu huo, habari zinaeleza kwamba Magufuli, aliyabeba yeye mwenyewe mafaili ya ndugu zake; Musa Magufuli ambaye ni mdogo wake, na Sundi Malomo ambaye ni mzazi mwenzake na kuwalazimisha watendaji wa TBA wafuate matakwa yake katika kuwapatia nyumba ndugu zake hao.

  Habari hizo zinaeleza kwamba awali Mtendaji Mkuu wa TBA alimshauri Magufuli kwamba suala la mauzo ya nyumba kwa ndugu zake ni kinyume cha utaratibu. Hata hivyo, imeelezwa kwamba Magufuli alilazimisha huku akisema mdogo wake hana tatizo kwa sababu alikuwa tayari mfanyakazi wa Serikali.

  Musa aliajiriwa kwa mkataba wa miezi mitatu, baada ya mwezi mmoja akauziwa nyumba na baada ya miezi miwili akaacha kazi.

  “Kwa upande wa Sundi, kwanza ilikuwa Sundi auziwe nyumba moja kwa moja. Lakini Magufuli alipoonywa akashtuka na kusema suala hilo aachiwe yeye mwenyewe. Na ndipo akaibuka na jina la Stanley Manongi kwamba ndiye mnunuzi halisi na baba yake Sundi,” vinasema vyanzo hivyo vya habari, vingine ambavyo vilishiriki moja kwa moja katika mchakato wa uuzaji nyumba hizo.

  Habari hizo zinaendelea kueleza kwamba baadaye, Sundi alishtuka akitilia shaka uaminifu wa Manongi, kwamba angeweza kumdhulumu nyumba hiyo.

  “Ndipo Magufuli aliibuka na mpango wa Sundi kuwa mtoto wa Manongi na mrithi wake na kisha kwa kuhakikisha kwamba hakuna dhuluma yoyote, mtoto wa Sundi naye akarithishwa na kama mrithi wa pili,” chanzo hicho cha habari kinaeleza.

  Chini ya sheria ya Executive Agency Act No. 30 ya mwaka 1997, TBA ilipewa madaraka yote ya kuuza nyumba za Serikali, kujenga nyumba mpya, kuzikarabati zilizopo pamoja na kugawa nyumba za madaraja A, B na C kwa wafanyakazi wa Serikali.

  Sheria hiyo inaipa mamlaka ya kipekee ya kufanya shughuli zote bila kuingiliwa na chombo chochote.

  Chini ya sheria hiyo, Waziri anaruhusiwa kuteua wajumbe wa bodi ya ushauri watakaomshauri Katibu Mkuu wa Wizara juu ya namna nzuri ya TBA kusimamia mamlaka yake.

  Hadi Machi mwaka huu, wajumbe hao walikuwa ni J. Kijazi, E. Lipambila, E. Lugwisha, Msangi, E. Mwakalinga, D. Kisasi, P. Ncheye, F. Werema na A. Bukuku.

  Hata hivyo, sheria haitoi nafasi yoyote kwa Waziri kusimamia shughuli za uuzwaji au upangaji wa nyumba za serikali.

  Mtendaji Mkuu wa TBA Togolayi Makumba Kimweri, alipoulizwa kupitia kwa Katibu Muhtasi wake, alimwambia mwandishi wa Rai aandike maswali kisha asubiri kuruhusiwa kuingia ndani ya ofisi.

  Hata hivyo, baada ya kusubiri kwa muda wa saa moja, mwandishi alipokwenda kuuliza akaambiwa kwamba Kimweri tayari alikwishaondoka ofisini kupitia mlango wa nyuma na asingeweza kurudi ofisini.

  Lakini baadhi ya wafanyakazi wa TBA wameiambia Rai kwamba kinachoandikwa kwenye magazeti kuhusu ushiriki wa Magufuli kuuza nyumba za Serikali ni kidogo mno kuliko hali halisi.

  Kama ilivyokuwa kwa mdogo wake Musa, waziri Magufuli alishinikiza mtoto wa dada yake anayeitwa James Doto Mgosha auziwe nyumba za serikali kwa kumtengenezea ajira ya muda mfupi katika TANROADS.

  Tofauti na Musa, Doto ameuziwa nyumba hiyo kwa jina la mtu mwingine lakini anaishi katika nyumba hiyo, namba 64 iliyopo Kinondoni Flats.

  Habari kutoka TBA zinaonyesha jina la mtu mwingine (tunalihifadhi) kuwa ndiye aliyeuziwa nyumba hiyo mtu huyo alipata kupitia utaratibu wa Magufuli kupeleka jina lake kwenye wakala wa majengo na kulazimisha apewe nyumba.

  Alipoulizwa kwa njia ya simu, Doto alisema suala la ajira na nyumba waulizwe waliomwajiri na kumpa nyumba. Akakata simu.

  Mfanyakazi mwingine alieleza Rai kwamba msichana mwingine (jina tunalihifadhi) akiwa na miezi minne tu kazini alipelekwa na Magufuli katika Wakala wa Majengo akilazimisha auziwe nyumba hata kabla ya kuthibitishwa kazini. Nyumba hiyo iko Block A, Ocean Road.

  Hata hivyo, habari hizo zinaeleza kwamba msichana huyo ambaye hadi sasa anaishi na wazazi wake, ameipangisha nyumba hiyo kwa mfanyakazi mmoja wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa na analipwa kwa dola za kimarekani.

  “Kuuza nyumba za serikali sawa, lakini kweli katika mtindo huu? Sisi tunaoshiriki kuzikagua na kuziratibu tukiomba hatupati, lakini wengine wanaingia serikalini miezi miwili wanapata nyumba. Na wengine hata si wafanyakazi, wanapata, hii si sahihi, alilalamika mfanyakazi mmoja aliyeandikia Rai kwa njia ya barua pepe.

  Hadi Machi mwaka huu Wakala wa Majengo wa Serikali (TBA) walishauza nyumba 8,288 ambazo hata hivyo zilitakiwa kuuzwa kwa watumishi wa serikali.

  Katika mauzo hayo, Serikali ilitarajia kupata jumla ya shilingi 60,016,556,439.00. Hata hivyo hadi sasa Serikali imepata shilingi 22,684,108,115.08.

  Kwa sasa, Serikali imebakiwa na nyumba 1,098 zinazosimamiwa na TBA. Kati ya hizo, nyumba 692 zimetengwa kwa wafanyakazi wa Serikali, nyumba 675 kama tied quarters, nyumba 111 zinatumika kama Rest House za Serikali, wakati nyumba 40 zinatumika kama state lodges. Nyumba 24 zinatumika kama ofisi na nyingine 29 ni kama karakana na bohari.

  SALVA RWEYEMAMU
  RAI
   
 2. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #81
  Sep 20, 2015
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,510
  Likes Received: 7,587
  Trophy Points: 280
  Siyo kweli,kipindi hicho Salva alikuwa kambi ya JK ikisimamiwa na Lowasa,hivyo yote hii ilikuwa ni kumzuia Magufuli kugombea uraisi baada ya JK.
   
 3. JT2014

  JT2014 JF-Expert Member

  #82
  Sep 20, 2015
  Joined: Jan 18, 2014
  Messages: 1,867
  Likes Received: 1,053
  Trophy Points: 280
  Oooh,kumbe ndo maana mamisab wake anagoma kuambatana naye kwenye kampeni!!!
   
 4. rais15

  rais15 JF-Expert Member

  #83
  Sep 20, 2015
  Joined: Jul 11, 2015
  Messages: 339
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Acha uongo na hujui ulisemalo
   
 5. M

  MONTESQUIEU JF-Expert Member

  #84
  Sep 20, 2015
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 847
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hakuna msafi TZ serikali ijitahidi tu kusimamia uchaguzi uwe wa wazi na kweli. EL OR mAGUFURI MMOJA WAO ATAKUWA RAIS WETU NA WOTE WAMEKUWA KWENYE SERIKALI HIYO HIYO. WA TZ WENGI NI WAPIGA DEAL TU
   
 6. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #85
  Sep 20, 2015
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  mhh

  kazi kweli kweli
   
 7. salimkabora

  salimkabora JF-Expert Member

  #86
  Sep 20, 2015
  Joined: Nov 10, 2012
  Messages: 2,451
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  ESCROW vipi hahusiki manake kuna orodha ya majina imefichwa; pembe za ndovu je, na masuala ya kuuza unga hayumo manake mkulu kaficha majina. Innji hii bhana wengine wanasakamwa kwa mambo ya kubambikiwa wakati madoni yenyewe kabisa wanalindwa kwa gharama zote
   
 8. Mack Wild

  Mack Wild JF-Expert Member

  #87
  Sep 20, 2015
  Joined: Apr 25, 2013
  Messages: 4,718
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  Atakuwa raisi chumbani kwako Tena kitandani ila si Tanzania
   
 9. Mack Wild

  Mack Wild JF-Expert Member

  #88
  Sep 20, 2015
  Joined: Apr 25, 2013
  Messages: 4,718
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Ablessed

  Ablessed JF-Expert Member

  #89
  Sep 20, 2015
  Joined: Mar 19, 2013
  Messages: 4,624
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kweli mkuu inaumiza sana tukiweka pembeni ushabiki wa siasa. Itakua kuna mengi yanaendelea humo ndani hebu jiulize ikiwa haya tusomayo humu ni ya kweli basi yule mama anavumilia mengi. Halafu nina wasi wasi na kauli zake za kibabe kama anaweza kuwaambia wananchi maneno yenye ukakasi je kwa mkewe si balaa
   
 11. kimsboy

  kimsboy JF-Expert Member

  #90
  Mar 2, 2018
  Joined: Oct 17, 2016
  Messages: 2,732
  Likes Received: 2,529
  Trophy Points: 280
   
 12. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #91
  Mar 5, 2018
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,263
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hivi Salva Rweyemamu aliyekuwa afisa habari ikulu yuko wapi?
   
 13. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #92
  Mar 5, 2018
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,263
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hivi Salva Rweyemamu aliyekuwa afisa habari ikulu yuko wapi?
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...