Bomu linalomwandama Magufuli

Magufuli kama unasoma hapa,kamuombe mkeo msamaha,hata mimi niliekuwa kambi yako mdogo mdogo.Yaani laana ya mke wako inakufuata.Ukweli popularity yako inapungua kila kukicha

Victoire kula likes zangu kibao kwa mara ya kwanza.
 
Ingekuwa vizuri habari hii ikachipishwa front page kuwakumbusha watanzania maana walishasahau. Kama iliandikwa na Salva Rweyemamu mwandishi wa habari wa rais kwa sasa, basi ni credible. Ichapishwe tena. Nawasilisha

Naunga mkono hoja.
 
Hii habari ni mbaya sana kwa Magufuli. Sasa ikiwa hivyo Waziri tu akiwa Raisi si itakuwa balaa?
 
Ukweli wa mambo Watanzania mara hii tunahitaji mabadiliko na tunayataka nje ya Ccm. Ukawa ndio suluhisho japo kuna kasoro kubwa ya vyama hivi vyote. Mgombea walomteua Lowassa ni tested leader anaweza ila kuna tatizo la afya yake. Amekua hawezi kuongea na kuzungumza kwa ufasaha. Lakini kwa vile tunataka mabadiliko tutampigia debe.

Ccm nao kama chama kina kasoro lukuki na kimeendelea kua chama kinachomilikiwa na kikundi maslahi sasa hivi. Ni wazi huwezi kupata ubunge bila ya pesa..ni kweli hili asije mtu kubisha , wakati wa uteuzi pesa zilitumika na ubabe.

Nao kwa ursis wakatupatia Magufuli. Mie nasema Magufuli hana sifa hata moja ya kuongoza nchii hii. Yeye mwenyewe hakutarajia kuwa atapita . Na ukweli alipita kutokana na wajumbe wa Nec kupiga kura za hasira baada ya Lowassa kukatwa. Wenyewe walimuandaa Membe . Walimueka Foreign miaka 10 ili aive kumtayarisha kuchukua nchi. Membe na mwembe zake lakini anazo sifa za kuwa rais.lakini mambo hayakua kama walivo tarajia akabwagwa chini. Turufu ikabaki kwa Makamba naye ni kijana ambaye angekua Bora zaidi..ni mwelewa. Lakini kura za maruhani zika mdondosha.

Hivyo sisi wapiga kura tumepata wagombea wawili tuchague. Mmoja , Magufuli not presidential material , not fit kuwa rais , hana sifa hata moja, he is not well informed person , sote tunakumbuka Mambo ya Saddam Na Kuwait. Huko mbele kwenye kuzisimamia sera za uchumi , mambo ya nje, uhusiano na mazungumzo na wafadhili hatujui itakuwaje...lakini huyu in short is not a presidential material. Akipita kuchaguliwa ccm wajitayarishe miaka mitano wachague mgombea mwengine nchi haiwezi ku afford kuongozwa kwa kurudi kinyume nyume.

Upande wa ukawa nao Lowassa ni tested leader, amekua waziri mkuu miaka 2. Rekodi iko wazi alimsaidia sana RAis akiwa W/Mkuu . Aliandamwa na kashfa lakini hizi si kigezo sana kwani kwa sasa kupata mr msafi ni kazi kweli kweli. Yeye anatatizo la afya na vyama hivi vya ukawa bado havina strtegies ya kujiimarisha kiuongozi . Miaka mitano hii wangetumia nguvu nyingi sana kushawishi watanzania wasomi na mashuhuri wawaunge mkono na kuingia ndani ya hivi vyama ili kubadilisha sura ya uongozi lakini walitidhika kuwa bile vile tangia uvhaguzi ulopita. Hakuna mabadiliko ya safu zao.hawana mipango thabit.

Sasa watanzania tumepewa choice hizi mbili tuchaguwe..na kwa hakuna budi lazima tuchague basi tuchague tu mabadiliko...tutafanyaje ?
 
Ukweli JPM sio kabisa..mkuu hii news ishatembea hata moderator akiifuta sio issue....huyu jamaa mtemi ukisikia hotuba zake ni mikwara kibao..sasa wtz tujiulize hv kwani ukiwa ktk baraza la mawaziri huwezi toa ushaufi wa maendeleo kwa mawazifi wenzio? Ye kila kitu anashangaa na kusema atawashughulikia akipata kura..alikua ansubiri apate uraisi ndio arekebishe mambo...huo ni ubinafsi...
 
Hizo pesa ambazo hazionekani kama bilion 38 inamaana makufuri ameisha idhulumu serikari muogope sana mtu hadi anaidhulumu serikali je mwananchi wa kawaida itakuwaje
 
Magufuli kama unasoma hapa,kamuombe mkeo msamaha,hata mimi niliekuwa kambi yako mdogo mdogo.Yaani laana ya mke wako inakufuata.Ukweli popularity yako inapungua kila kukicha

Bifu la mke hata siyo la Sundi ,itakuwa ni la Kabula wa Keby's.
 
Habari hii ilichapishwa kwenye gazeti la RAI miaka michache iliyopita ikisomeka...

Huyu Ndiye Pombe Magufuli:

- Wasema nyumba 8,000 kauza kwa mkono wake mwenyewe
- Apuuza maonyo ya wataalamu- Mafaili ya Sundi na Musa aliyabeba kwapani

ALIYEKUWA Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, katika Serikali ya awamu ya tatu, aliteka madaraka na kuwa mwenyekiti wa zoezi la kuuza nyumba za serikali ambazo hadi sasa, zimeshauzwa 8,288 imefahamika.

Habari zilizopatikana ndani ya wakala wa Majengo ya Serikali (TBA), zimethibitishia Rai wiki hii kwamba Magufuli alihakikisha anashiriki kama Mwenyekiti katika zoezi zima la kuuza nyumba, ambalo kimsingi lilistahili kusimamiwa na Mtendaji Mkuu wa TBA.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari ndani ya TBA, Magufuli alifanya kila aina ya ‘fujo’ katika zoezi la kuuza nyumba hizo, wakati mwingine akibatilisha maamuzi yaliyofanywa na Kamati ya TBA ya kuuza nyumba hizo, akiwapangia watu nyumba kwa utashi wake na wakati mwingine akiwakemea wale wote waliomshauri kinyume na matakwa.

Ni chini ya utaratibu huo, habari zinaeleza kwamba Magufuli, aliyabeba yeye mwenyewe mafaili ya ndugu zake; Musa Magufuli ambaye ni mdogo wake, na Sundi Malomo ambaye ni mzazi mwenzake na kuwalazimisha watendaji wa TBA wafuate matakwa yake katika kuwapatia nyumba ndugu zake hao.

Habari hizo zinaeleza kwamba awali Mtendaji Mkuu wa TBA alimshauri Magufuli kwamba suala la mauzo ya nyumba kwa ndugu zake ni kinyume cha utaratibu. Hata hivyo, imeelezwa kwamba Magufuli alilazimisha huku akisema mdogo wake hana tatizo kwa sababu alikuwa tayari mfanyakazi wa Serikali.

Musa aliajiriwa kwa mkataba wa miezi mitatu, baada ya mwezi mmoja akauziwa nyumba na baada ya miezi miwili akaacha kazi.

“Kwa upande wa Sundi, kwanza ilikuwa Sundi auziwe nyumba moja kwa moja. Lakini Magufuli alipoonywa akashtuka na kusema suala hilo aachiwe yeye mwenyewe. Na ndipo akaibuka na jina la Stanley Manongi kwamba ndiye mnunuzi halisi na baba yake Sundi,” vinasema vyanzo hivyo vya habari, vingine ambavyo vilishiriki moja kwa moja katika mchakato wa uuzaji nyumba hizo.

Habari hizo zinaendelea kueleza kwamba baadaye, Sundi alishtuka akitilia shaka uaminifu wa Manongi, kwamba angeweza kumdhulumu nyumba hiyo.

“Ndipo Magufuli aliibuka na mpango wa Sundi kuwa mtoto wa Manongi na mrithi wake na kisha kwa kuhakikisha kwamba hakuna dhuluma yoyote, mtoto wa Sundi naye akarithishwa na kama mrithi wa pili,” chanzo hicho cha habari kinaeleza.

Chini ya sheria ya Executive Agency Act No. 30 ya mwaka 1997, TBA ilipewa madaraka yote ya kuuza nyumba za Serikali, kujenga nyumba mpya, kuzikarabati zilizopo pamoja na kugawa nyumba za madaraja A, B na C kwa wafanyakazi wa Serikali.

Sheria hiyo inaipa mamlaka ya kipekee ya kufanya shughuli zote bila kuingiliwa na chombo chochote.

Chini ya sheria hiyo, Waziri anaruhusiwa kuteua wajumbe wa bodi ya ushauri watakaomshauri Katibu Mkuu wa Wizara juu ya namna nzuri ya TBA kusimamia mamlaka yake.

Hadi Machi mwaka huu, wajumbe hao walikuwa ni J. Kijazi, E. Lipambila, E. Lugwisha, Msangi, E. Mwakalinga, D. Kisasi, P. Ncheye, F. Werema na A. Bukuku.

Hata hivyo, sheria haitoi nafasi yoyote kwa Waziri kusimamia shughuli za uuzwaji au upangaji wa nyumba za serikali.

Mtendaji Mkuu wa TBA Togolayi Makumba Kimweri, alipoulizwa kupitia kwa Katibu Muhtasi wake, alimwambia mwandishi wa Rai aandike maswali kisha asubiri kuruhusiwa kuingia ndani ya ofisi.

Hata hivyo, baada ya kusubiri kwa muda wa saa moja, mwandishi alipokwenda kuuliza akaambiwa kwamba Kimweri tayari alikwishaondoka ofisini kupitia mlango wa nyuma na asingeweza kurudi ofisini.

Lakini baadhi ya wafanyakazi wa TBA wameiambia Rai kwamba kinachoandikwa kwenye magazeti kuhusu ushiriki wa Magufuli kuuza nyumba za Serikali ni kidogo mno kuliko hali halisi.

Kama ilivyokuwa kwa mdogo wake Musa, waziri Magufuli alishinikiza mtoto wa dada yake anayeitwa James Doto Mgosha auziwe nyumba za serikali kwa kumtengenezea ajira ya muda mfupi katika TANROADS.

Tofauti na Musa, Doto ameuziwa nyumba hiyo kwa jina la mtu mwingine lakini anaishi katika nyumba hiyo, namba 64 iliyopo Kinondoni Flats.

Habari kutoka TBA zinaonyesha jina la mtu mwingine (tunalihifadhi) kuwa ndiye aliyeuziwa nyumba hiyo mtu huyo alipata kupitia utaratibu wa Magufuli kupeleka jina lake kwenye wakala wa majengo na kulazimisha apewe nyumba.

Alipoulizwa kwa njia ya simu, Doto alisema suala la ajira na nyumba waulizwe waliomwajiri na kumpa nyumba. Akakata simu.

Mfanyakazi mwingine alieleza Rai kwamba msichana mwingine (jina tunalihifadhi) akiwa na miezi minne tu kazini alipelekwa na Magufuli katika Wakala wa Majengo akilazimisha auziwe nyumba hata kabla ya kuthibitishwa kazini. Nyumba hiyo iko Block A, Ocean Road.

Hata hivyo, habari hizo zinaeleza kwamba msichana huyo ambaye hadi sasa anaishi na wazazi wake, ameipangisha nyumba hiyo kwa mfanyakazi mmoja wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa na analipwa kwa dola za kimarekani.

“Kuuza nyumba za serikali sawa, lakini kweli katika mtindo huu? Sisi tunaoshiriki kuzikagua na kuziratibu tukiomba hatupati, lakini wengine wanaingia serikalini miezi miwili wanapata nyumba. Na wengine hata si wafanyakazi, wanapata, hii si sahihi, alilalamika mfanyakazi mmoja aliyeandikia Rai kwa njia ya barua pepe.

Hadi Machi mwaka huu Wakala wa Majengo wa Serikali (TBA) walishauza nyumba 8,288 ambazo hata hivyo zilitakiwa kuuzwa kwa watumishi wa serikali.

Katika mauzo hayo, Serikali ilitarajia kupata jumla ya shilingi 60,016,556,439.00. Hata hivyo hadi sasa Serikali imepata shilingi 22,684,108,115.08.

Kwa sasa, Serikali imebakiwa na nyumba 1,098 zinazosimamiwa na TBA. Kati ya hizo, nyumba 692 zimetengwa kwa wafanyakazi wa Serikali, nyumba 675 kama tied quarters, nyumba 111 zinatumika kama Rest House za Serikali, wakati nyumba 40 zinatumika kama state lodges. Nyumba 24 zinatumika kama ofisi na nyingine 29 ni kama karakana na bohari.

SALVA RWEYEMAMU
RAI

niliwahi kusema, hao mafisadi atakaowaundia mahakama ni wa kuanzia lini? juzi, jana, leo au kesho? kwa hali kama hii, yeye ataipa ruhusa hiyo serikali yake imfungulie mashitaka? je salva atatoa ushahidi upande upi? huyu jamaa anafanana na kk yake yule wa upumabavu na ulofa na umbumbumbu!. Munafiki dawa yake ni kumwanika hadharani! wamezoea ubabe!
 
Angalia clip ya sumaye kajibu hilo swali alilouliza mbatia tafuteni kila kashafa ila edo ni kiboko wa kashfa
 
Mods wataitoa.Tuisevu wakikata tuiweke kwenye Whattsup groups

Hifadhi na udhibitisho wake kabisa.
ImageUploadedByJamiiForums1442695623.265516.jpg

Kwa hisani ya Chakaza Library
 
Last edited by a moderator:
Ukweli JPM sio kabisa..mkuu hii news ishatembea hata moderator akiifuta sio issue....huyu jamaa mtemi ukisikia hotuba zake ni mikwara kibao..sasa wtz tujiulize hv kwani ukiwa ktk baraza la mawaziri huwezi toa ushaufi wa maendeleo kwa mawazifi wenzio? Ye kila kitu anashangaa na kusema atawashughulikia akipata kura..alikua ansubiri apate uraisi ndio arekebishe mambo...huo ni ubinafsi...
Mkuu inashangaza sana
 
Kweli ''uchafu'' wa CCM ni mfumo, hivyo katu haitatokea kiongozi mwana-CCM akibaki ndani ya CCM kuwa msafi lazima mfumo utambadilisha na kuwa kama wengine ndani ya CCM. Ndiyo maana mekuwa vigumu sana CCM kupambana na ufisadi, kutumia madaraka (ofisi/vyeo/dhamana) vibaya, kulindana, kutoa ahadi bila utekelezaji ..... n.k.
 
Back
Top Bottom