Bomu linalomwandama Magufuli | Page 3 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bomu linalomwandama Magufuli

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by EasyFit, Sep 19, 2015.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2015
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,263
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Habari hii ilichapishwa kwenye gazeti la RAI miaka michache iliyopita ikisomeka...

  Huyu Ndiye Pombe Magufuli:

  - Wasema nyumba 8,000 kauza kwa mkono wake mwenyewe
  - Apuuza maonyo ya wataalamu- Mafaili ya Sundi na Musa aliyabeba kwapani

  ALIYEKUWA Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, katika Serikali ya awamu ya tatu, aliteka madaraka na kuwa mwenyekiti wa zoezi la kuuza nyumba za serikali ambazo hadi sasa, zimeshauzwa 8,288 imefahamika.

  Habari zilizopatikana ndani ya wakala wa Majengo ya Serikali (TBA), zimethibitishia Rai wiki hii kwamba Magufuli alihakikisha anashiriki kama Mwenyekiti katika zoezi zima la kuuza nyumba, ambalo kimsingi lilistahili kusimamiwa na Mtendaji Mkuu wa TBA.

  Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari ndani ya TBA, Magufuli alifanya kila aina ya ‘fujo’ katika zoezi la kuuza nyumba hizo, wakati mwingine akibatilisha maamuzi yaliyofanywa na Kamati ya TBA ya kuuza nyumba hizo, akiwapangia watu nyumba kwa utashi wake na wakati mwingine akiwakemea wale wote waliomshauri kinyume na matakwa.

  Ni chini ya utaratibu huo, habari zinaeleza kwamba Magufuli, aliyabeba yeye mwenyewe mafaili ya ndugu zake; Musa Magufuli ambaye ni mdogo wake, na Sundi Malomo ambaye ni mzazi mwenzake na kuwalazimisha watendaji wa TBA wafuate matakwa yake katika kuwapatia nyumba ndugu zake hao.

  Habari hizo zinaeleza kwamba awali Mtendaji Mkuu wa TBA alimshauri Magufuli kwamba suala la mauzo ya nyumba kwa ndugu zake ni kinyume cha utaratibu. Hata hivyo, imeelezwa kwamba Magufuli alilazimisha huku akisema mdogo wake hana tatizo kwa sababu alikuwa tayari mfanyakazi wa Serikali.

  Musa aliajiriwa kwa mkataba wa miezi mitatu, baada ya mwezi mmoja akauziwa nyumba na baada ya miezi miwili akaacha kazi.

  “Kwa upande wa Sundi, kwanza ilikuwa Sundi auziwe nyumba moja kwa moja. Lakini Magufuli alipoonywa akashtuka na kusema suala hilo aachiwe yeye mwenyewe. Na ndipo akaibuka na jina la Stanley Manongi kwamba ndiye mnunuzi halisi na baba yake Sundi,” vinasema vyanzo hivyo vya habari, vingine ambavyo vilishiriki moja kwa moja katika mchakato wa uuzaji nyumba hizo.

  Habari hizo zinaendelea kueleza kwamba baadaye, Sundi alishtuka akitilia shaka uaminifu wa Manongi, kwamba angeweza kumdhulumu nyumba hiyo.

  “Ndipo Magufuli aliibuka na mpango wa Sundi kuwa mtoto wa Manongi na mrithi wake na kisha kwa kuhakikisha kwamba hakuna dhuluma yoyote, mtoto wa Sundi naye akarithishwa na kama mrithi wa pili,” chanzo hicho cha habari kinaeleza.

  Chini ya sheria ya Executive Agency Act No. 30 ya mwaka 1997, TBA ilipewa madaraka yote ya kuuza nyumba za Serikali, kujenga nyumba mpya, kuzikarabati zilizopo pamoja na kugawa nyumba za madaraja A, B na C kwa wafanyakazi wa Serikali.

  Sheria hiyo inaipa mamlaka ya kipekee ya kufanya shughuli zote bila kuingiliwa na chombo chochote.

  Chini ya sheria hiyo, Waziri anaruhusiwa kuteua wajumbe wa bodi ya ushauri watakaomshauri Katibu Mkuu wa Wizara juu ya namna nzuri ya TBA kusimamia mamlaka yake.

  Hadi Machi mwaka huu, wajumbe hao walikuwa ni J. Kijazi, E. Lipambila, E. Lugwisha, Msangi, E. Mwakalinga, D. Kisasi, P. Ncheye, F. Werema na A. Bukuku.

  Hata hivyo, sheria haitoi nafasi yoyote kwa Waziri kusimamia shughuli za uuzwaji au upangaji wa nyumba za serikali.

  Mtendaji Mkuu wa TBA Togolayi Makumba Kimweri, alipoulizwa kupitia kwa Katibu Muhtasi wake, alimwambia mwandishi wa Rai aandike maswali kisha asubiri kuruhusiwa kuingia ndani ya ofisi.

  Hata hivyo, baada ya kusubiri kwa muda wa saa moja, mwandishi alipokwenda kuuliza akaambiwa kwamba Kimweri tayari alikwishaondoka ofisini kupitia mlango wa nyuma na asingeweza kurudi ofisini.

  Lakini baadhi ya wafanyakazi wa TBA wameiambia Rai kwamba kinachoandikwa kwenye magazeti kuhusu ushiriki wa Magufuli kuuza nyumba za Serikali ni kidogo mno kuliko hali halisi.

  Kama ilivyokuwa kwa mdogo wake Musa, waziri Magufuli alishinikiza mtoto wa dada yake anayeitwa James Doto Mgosha auziwe nyumba za serikali kwa kumtengenezea ajira ya muda mfupi katika TANROADS.

  Tofauti na Musa, Doto ameuziwa nyumba hiyo kwa jina la mtu mwingine lakini anaishi katika nyumba hiyo, namba 64 iliyopo Kinondoni Flats.

  Habari kutoka TBA zinaonyesha jina la mtu mwingine (tunalihifadhi) kuwa ndiye aliyeuziwa nyumba hiyo mtu huyo alipata kupitia utaratibu wa Magufuli kupeleka jina lake kwenye wakala wa majengo na kulazimisha apewe nyumba.

  Alipoulizwa kwa njia ya simu, Doto alisema suala la ajira na nyumba waulizwe waliomwajiri na kumpa nyumba. Akakata simu.

  Mfanyakazi mwingine alieleza Rai kwamba msichana mwingine (jina tunalihifadhi) akiwa na miezi minne tu kazini alipelekwa na Magufuli katika Wakala wa Majengo akilazimisha auziwe nyumba hata kabla ya kuthibitishwa kazini. Nyumba hiyo iko Block A, Ocean Road.

  Hata hivyo, habari hizo zinaeleza kwamba msichana huyo ambaye hadi sasa anaishi na wazazi wake, ameipangisha nyumba hiyo kwa mfanyakazi mmoja wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa na analipwa kwa dola za kimarekani.

  “Kuuza nyumba za serikali sawa, lakini kweli katika mtindo huu? Sisi tunaoshiriki kuzikagua na kuziratibu tukiomba hatupati, lakini wengine wanaingia serikalini miezi miwili wanapata nyumba. Na wengine hata si wafanyakazi, wanapata, hii si sahihi, alilalamika mfanyakazi mmoja aliyeandikia Rai kwa njia ya barua pepe.

  Hadi Machi mwaka huu Wakala wa Majengo wa Serikali (TBA) walishauza nyumba 8,288 ambazo hata hivyo zilitakiwa kuuzwa kwa watumishi wa serikali.

  Katika mauzo hayo, Serikali ilitarajia kupata jumla ya shilingi 60,016,556,439.00. Hata hivyo hadi sasa Serikali imepata shilingi 22,684,108,115.08.

  Kwa sasa, Serikali imebakiwa na nyumba 1,098 zinazosimamiwa na TBA. Kati ya hizo, nyumba 692 zimetengwa kwa wafanyakazi wa Serikali, nyumba 675 kama tied quarters, nyumba 111 zinatumika kama Rest House za Serikali, wakati nyumba 40 zinatumika kama state lodges. Nyumba 24 zinatumika kama ofisi na nyingine 29 ni kama karakana na bohari.

  SALVA RWEYEMAMU
  RAI
   
 2. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #41
  Sep 20, 2015
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,994
  Likes Received: 451
  Trophy Points: 180
  Kebby's ni hotel ipo Mwenge karibu na kituo cha Bamaga, ni hotel ya hawala yake Magufuli anayeitwa Kabula dada (Kb) au Kebby. Inasemekana ni nguvu za mzee.
   
 3. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #42
  Sep 20, 2015
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,924
  Trophy Points: 280
  Huyu Magufuli sina hakika kama atafikisha kura milioni tatu
   
 4. hazole1

  hazole1 JF-Expert Member

  #43
  Sep 20, 2015
  Joined: Jan 3, 2015
  Messages: 4,129
  Likes Received: 3,349
  Trophy Points: 280
  Kama mke wake tu hamkubari na ninahisi mke wa makufuri lazima kura atampa lowassa na ukienda huko kwao ndio hawamuelewi kabisa je hizo kura milion 3 atazipata wapi?
   
 5. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #44
  Sep 20, 2015
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 12,036
  Likes Received: 3,872
  Trophy Points: 280
  Naunga mkonyo hoja. Kura zikitosha ichapishwe haraka sn ili watz wasiendelee kupotoshwa
   
 6. l

  lugaluga Senior Member

  #45
  Sep 20, 2015
  Joined: Mar 30, 2015
  Messages: 108
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  tukutane tarehe 26-10
   
 7. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #46
  Sep 20, 2015
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 12,036
  Likes Received: 3,872
  Trophy Points: 280
  Ndio maana magufuli hana confidence kabisa kwa sababu ya matatizo makuu manne
  1. Mke wake kumsusa
  2. Ufisadi aliofanya kwenye uuzaji wa nyumba
  ,3. Kushindwa kesi ya Samaki wa magufuli na kuliingizia taifa hasara kubwa
  4. Kumpa kimada wake nyumba ya serikali
   
 8. a

  asakuta same JF-Expert Member

  #47
  Sep 20, 2015
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 15,040
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 0
  Sundi ndiye yule kimada aliyezaa naye mtoto Jerry ambaye alimuhonga nyumba ya Serikali enzi hizo za kuuza nyumba za Serikali....

  Kabula wa Keby's ni kimada wake wa sasa aliyemjengea Keby's hotel pale maeneo ya Mwenge.

  Kwa hali hiyo kweli wife haimuumi!?

  Jangwani yenyewe alisahau kumtambulisha mkewe halali Janeth, mpaka dakika za mwisho alipokumbushwa na JK.
  Kwa udhalilishwaji huo , huyo mama ajipumzikie tu.
   
 9. a

  asakuta same JF-Expert Member

  #48
  Sep 20, 2015
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 15,040
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 0
  Nimeshaiweka vizuri wakati namjibu Victoire
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. hazole1

  hazole1 JF-Expert Member

  #49
  Sep 20, 2015
  Joined: Jan 3, 2015
  Messages: 4,129
  Likes Received: 3,349
  Trophy Points: 280
  Ivi yule bwana mkubwa kama amepita mote humo atakuwa amekosa kakichwani kweli na inaoneka yule mzee anapenda sana chini hadi hadi anahonga nyumba serikali.
   
 11. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #50
  Sep 20, 2015
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 12,036
  Likes Received: 3,872
  Trophy Points: 280
  Kweli ccm ni ileile na wanaccm ni walewale. mkapa alimhonga mramba wizara ya fedha. Mwenzake kikwete alikuwa anahonga wilaya na mikoa sasa km akiwa waziri alikuwa anahonga nyumba za serikali je akiwa rais atahonga nn?
  Tafakari chukua hatua weka ccm mbalo na watz.
   
 12. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #51
  Sep 20, 2015
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,994
  Likes Received: 451
  Trophy Points: 180
  Ataanza kuhonga nyumba za ikulu ndogo za wilaya.
   
 13. C

  CHAZA JF-Expert Member

  #52
  Sep 20, 2015
  Joined: Dec 21, 2012
  Messages: 6,793
  Likes Received: 2,256
  Trophy Points: 280
  Nani kaandika, mbona jina ni la Boss wa Kurugenzi kuu ya Habari State house au jina limefanana!?
   
 14. T

  Twilightstar Senior Member

  #53
  Sep 20, 2015
  Joined: Mar 29, 2015
  Messages: 192
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Magufuli hafai kuwa Rais wetu, atawagawa hata watanzania kwa ndugu zake. Wapiga kura wanatakiwa watahadharishwe.
   
 15. C

  CHAZA JF-Expert Member

  #54
  Sep 20, 2015
  Joined: Dec 21, 2012
  Messages: 6,793
  Likes Received: 2,256
  Trophy Points: 280
  Hiyo ya nne umma haua uthibitisho ila hizo tatu za kwanza zinajulikana na Watanzania walio wengi!
   
 16. kamandawasua

  kamandawasua JF-Expert Member

  #55
  Sep 20, 2015
  Joined: Jun 6, 2013
  Messages: 290
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ndo SISIEMU
   
 17. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #56
  Sep 20, 2015
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,994
  Likes Received: 451
  Trophy Points: 180
  Aliandika enzi hizo kabla ya kulambishwa asali ya ukurugenzi nafikiri leo akiiona makala hii anaweza kuikana.
   
 18. m

  majeshi 1981 JF-Expert Member

  #57
  Sep 20, 2015
  Joined: Dec 7, 2013
  Messages: 1,856
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 180
  magufuli ni zaidi ya majanga
   
 19. M

  Manyunchwi JF-Expert Member

  #58
  Sep 20, 2015
  Joined: May 11, 2013
  Messages: 427
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  wazinzi wanapigiwaga kura ya ndiyo? unahonga hawara nyumba ya serikali!
   
 20. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #59
  Sep 20, 2015
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 145
  Uzi upo tangu jana lakini wale jamaa zetu wa it wanachungulua tu wasepa hakuna anaye tetea mhhh imewakuna njooni kina
  jinga lao
  moto chin
  liz
  ritz
  vip mpo kwenye sabato au leo kanisani tutawasubiri kesho
   
 21. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #60
  Sep 20, 2015
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 12,036
  Likes Received: 3,872
  Trophy Points: 280
  Na hapa hachomoki!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...