Bomu linalomwandama Magufuli | Page 4 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bomu linalomwandama Magufuli

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by EasyFit, Sep 19, 2015.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2015
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,263
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Habari hii ilichapishwa kwenye gazeti la RAI miaka michache iliyopita ikisomeka...

  Huyu Ndiye Pombe Magufuli:

  - Wasema nyumba 8,000 kauza kwa mkono wake mwenyewe
  - Apuuza maonyo ya wataalamu- Mafaili ya Sundi na Musa aliyabeba kwapani

  ALIYEKUWA Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, katika Serikali ya awamu ya tatu, aliteka madaraka na kuwa mwenyekiti wa zoezi la kuuza nyumba za serikali ambazo hadi sasa, zimeshauzwa 8,288 imefahamika.

  Habari zilizopatikana ndani ya wakala wa Majengo ya Serikali (TBA), zimethibitishia Rai wiki hii kwamba Magufuli alihakikisha anashiriki kama Mwenyekiti katika zoezi zima la kuuza nyumba, ambalo kimsingi lilistahili kusimamiwa na Mtendaji Mkuu wa TBA.

  Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari ndani ya TBA, Magufuli alifanya kila aina ya ‘fujo’ katika zoezi la kuuza nyumba hizo, wakati mwingine akibatilisha maamuzi yaliyofanywa na Kamati ya TBA ya kuuza nyumba hizo, akiwapangia watu nyumba kwa utashi wake na wakati mwingine akiwakemea wale wote waliomshauri kinyume na matakwa.

  Ni chini ya utaratibu huo, habari zinaeleza kwamba Magufuli, aliyabeba yeye mwenyewe mafaili ya ndugu zake; Musa Magufuli ambaye ni mdogo wake, na Sundi Malomo ambaye ni mzazi mwenzake na kuwalazimisha watendaji wa TBA wafuate matakwa yake katika kuwapatia nyumba ndugu zake hao.

  Habari hizo zinaeleza kwamba awali Mtendaji Mkuu wa TBA alimshauri Magufuli kwamba suala la mauzo ya nyumba kwa ndugu zake ni kinyume cha utaratibu. Hata hivyo, imeelezwa kwamba Magufuli alilazimisha huku akisema mdogo wake hana tatizo kwa sababu alikuwa tayari mfanyakazi wa Serikali.

  Musa aliajiriwa kwa mkataba wa miezi mitatu, baada ya mwezi mmoja akauziwa nyumba na baada ya miezi miwili akaacha kazi.

  “Kwa upande wa Sundi, kwanza ilikuwa Sundi auziwe nyumba moja kwa moja. Lakini Magufuli alipoonywa akashtuka na kusema suala hilo aachiwe yeye mwenyewe. Na ndipo akaibuka na jina la Stanley Manongi kwamba ndiye mnunuzi halisi na baba yake Sundi,” vinasema vyanzo hivyo vya habari, vingine ambavyo vilishiriki moja kwa moja katika mchakato wa uuzaji nyumba hizo.

  Habari hizo zinaendelea kueleza kwamba baadaye, Sundi alishtuka akitilia shaka uaminifu wa Manongi, kwamba angeweza kumdhulumu nyumba hiyo.

  “Ndipo Magufuli aliibuka na mpango wa Sundi kuwa mtoto wa Manongi na mrithi wake na kisha kwa kuhakikisha kwamba hakuna dhuluma yoyote, mtoto wa Sundi naye akarithishwa na kama mrithi wa pili,” chanzo hicho cha habari kinaeleza.

  Chini ya sheria ya Executive Agency Act No. 30 ya mwaka 1997, TBA ilipewa madaraka yote ya kuuza nyumba za Serikali, kujenga nyumba mpya, kuzikarabati zilizopo pamoja na kugawa nyumba za madaraja A, B na C kwa wafanyakazi wa Serikali.

  Sheria hiyo inaipa mamlaka ya kipekee ya kufanya shughuli zote bila kuingiliwa na chombo chochote.

  Chini ya sheria hiyo, Waziri anaruhusiwa kuteua wajumbe wa bodi ya ushauri watakaomshauri Katibu Mkuu wa Wizara juu ya namna nzuri ya TBA kusimamia mamlaka yake.

  Hadi Machi mwaka huu, wajumbe hao walikuwa ni J. Kijazi, E. Lipambila, E. Lugwisha, Msangi, E. Mwakalinga, D. Kisasi, P. Ncheye, F. Werema na A. Bukuku.

  Hata hivyo, sheria haitoi nafasi yoyote kwa Waziri kusimamia shughuli za uuzwaji au upangaji wa nyumba za serikali.

  Mtendaji Mkuu wa TBA Togolayi Makumba Kimweri, alipoulizwa kupitia kwa Katibu Muhtasi wake, alimwambia mwandishi wa Rai aandike maswali kisha asubiri kuruhusiwa kuingia ndani ya ofisi.

  Hata hivyo, baada ya kusubiri kwa muda wa saa moja, mwandishi alipokwenda kuuliza akaambiwa kwamba Kimweri tayari alikwishaondoka ofisini kupitia mlango wa nyuma na asingeweza kurudi ofisini.

  Lakini baadhi ya wafanyakazi wa TBA wameiambia Rai kwamba kinachoandikwa kwenye magazeti kuhusu ushiriki wa Magufuli kuuza nyumba za Serikali ni kidogo mno kuliko hali halisi.

  Kama ilivyokuwa kwa mdogo wake Musa, waziri Magufuli alishinikiza mtoto wa dada yake anayeitwa James Doto Mgosha auziwe nyumba za serikali kwa kumtengenezea ajira ya muda mfupi katika TANROADS.

  Tofauti na Musa, Doto ameuziwa nyumba hiyo kwa jina la mtu mwingine lakini anaishi katika nyumba hiyo, namba 64 iliyopo Kinondoni Flats.

  Habari kutoka TBA zinaonyesha jina la mtu mwingine (tunalihifadhi) kuwa ndiye aliyeuziwa nyumba hiyo mtu huyo alipata kupitia utaratibu wa Magufuli kupeleka jina lake kwenye wakala wa majengo na kulazimisha apewe nyumba.

  Alipoulizwa kwa njia ya simu, Doto alisema suala la ajira na nyumba waulizwe waliomwajiri na kumpa nyumba. Akakata simu.

  Mfanyakazi mwingine alieleza Rai kwamba msichana mwingine (jina tunalihifadhi) akiwa na miezi minne tu kazini alipelekwa na Magufuli katika Wakala wa Majengo akilazimisha auziwe nyumba hata kabla ya kuthibitishwa kazini. Nyumba hiyo iko Block A, Ocean Road.

  Hata hivyo, habari hizo zinaeleza kwamba msichana huyo ambaye hadi sasa anaishi na wazazi wake, ameipangisha nyumba hiyo kwa mfanyakazi mmoja wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa na analipwa kwa dola za kimarekani.

  “Kuuza nyumba za serikali sawa, lakini kweli katika mtindo huu? Sisi tunaoshiriki kuzikagua na kuziratibu tukiomba hatupati, lakini wengine wanaingia serikalini miezi miwili wanapata nyumba. Na wengine hata si wafanyakazi, wanapata, hii si sahihi, alilalamika mfanyakazi mmoja aliyeandikia Rai kwa njia ya barua pepe.

  Hadi Machi mwaka huu Wakala wa Majengo wa Serikali (TBA) walishauza nyumba 8,288 ambazo hata hivyo zilitakiwa kuuzwa kwa watumishi wa serikali.

  Katika mauzo hayo, Serikali ilitarajia kupata jumla ya shilingi 60,016,556,439.00. Hata hivyo hadi sasa Serikali imepata shilingi 22,684,108,115.08.

  Kwa sasa, Serikali imebakiwa na nyumba 1,098 zinazosimamiwa na TBA. Kati ya hizo, nyumba 692 zimetengwa kwa wafanyakazi wa Serikali, nyumba 675 kama tied quarters, nyumba 111 zinatumika kama Rest House za Serikali, wakati nyumba 40 zinatumika kama state lodges. Nyumba 24 zinatumika kama ofisi na nyingine 29 ni kama karakana na bohari.

  SALVA RWEYEMAMU
  RAI
   
 2. james katto

  james katto JF-Expert Member

  #61
  Sep 20, 2015
  Joined: Sep 1, 2013
  Messages: 384
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Mzinzi koma kumnyoshea kidole Mwizi!
   
 3. C

  CHAZA JF-Expert Member

  #62
  Sep 20, 2015
  Joined: Dec 21, 2012
  Messages: 6,793
  Likes Received: 2,256
  Trophy Points: 280
  Simiyu yao, Dada FF, Jingalao, Lizabon et al wamekimbia. Uzuri wa hii makala iliandikwa na mtu ambaye kwa sasa ni mtu mwandamizi tena yuko ofisi kubwa kabisa-Ikulu! I salute you Max Mello kuanzisha Jamii Forums ambapo data kama hizi huwez kuzipata popote mwanzoni nje ya JF!
   
 4. w

  w.senteuh Senior Member

  #63
  Sep 20, 2015
  Joined: Sep 8, 2015
  Messages: 102
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  jamani ndo maana mkapa kawaita mapumbavu na malofa!!!mwandishi silva rweyimamu!!kurugenz ya habar ikulu!!!nyumba zilizobaki ni 1098,,someni!!692,675,111,40,29 !!!!majanga mbona zinafika 1500!!!facke source!!!!!!!!!mara kebb'ys!!!tulieni dawa ifanye kazi kwani hamjui hesabu na mnakurupuka!!!magufuli ndiye rais wa tanzania 2015-2020!!
   
 5. mwengeso

  mwengeso JF-Expert Member

  #64
  Sep 20, 2015
  Joined: Nov 27, 2014
  Messages: 5,039
  Likes Received: 2,730
  Trophy Points: 280
  Kwa maelezo yako, ni vyema hayo hayo yaweendee waliohama CCM baada ya kukatwa. Ho pia walikuwa na madaraka huko, yawezekanaje leo watuongopee wanaweza kuleta mabadiliko. Mtu makini, ili aaminike, ni vyema akafanya mabadiliko kwake kwanza. Hutegemei kujenga nyumbani kwa mwenzio unaacha kwako hakuko shwari.

  TAFAKARI CHUKUA HATUA.
   
 6. Jp Omuga

  Jp Omuga JF-Expert Member

  #65
  Sep 20, 2015
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 2,784
  Likes Received: 942
  Trophy Points: 280
 7. J

  Jozi 1 JF-Expert Member

  #66
  Sep 20, 2015
  Joined: Aug 16, 2015
  Messages: 5,053
  Likes Received: 2,294
  Trophy Points: 280
  I must say this sounds comical ha ha ha ha ha
   
 8. m

  mtoto wa maskini JF-Expert Member

  #67
  Sep 20, 2015
  Joined: Jun 28, 2013
  Messages: 1,154
  Likes Received: 550
  Trophy Points: 280
  Too late maana kaisha........
   
 9. Mb-one

  Mb-one JF-Expert Member

  #68
  Sep 20, 2015
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 609
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 80
  utatushushia credit wana ukawa...maCCM hawachelewi kusemaa tunazushaa, si unajua wanatafuta kick tu kdgoo
   
 10. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #69
  Sep 20, 2015
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,982
  Likes Received: 1,861
  Trophy Points: 280
  Huyu si mgombea urais ni mgombea ujambazi aisee
   
 11. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #70
  Sep 20, 2015
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,510
  Likes Received: 7,587
  Trophy Points: 280
  Mimi ni team Magufuli,ila ninayosoma humu kuhusu alivyomfanyia mke wake,incase ni ya kweli ,yanaumiza sana.Mimi mtu asiyemjali mke wa ujana wake na akaweza jali mahawara zake huwa namuwekea wasiwasi sana katika kufaa kwake kuwa kiongozi.Ndo maana nasema kama ni kweli Magufuli atengeneze na mkewe,na kama leo nisipomwona huyu mama kwenye mkutano wa Magufuli huko Chato basi nitaconclude kuwa Magufuli hatashinda Uraisi.Ila mama Magufuli akionekana leo kule Chato basi Magufuli ni Rais na anasubiri kuapishwa tu.
   
 12. a

  asakuta same JF-Expert Member

  #71
  Sep 20, 2015
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 15,040
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 0
 13. m

  makoko jumanne JF-Expert Member

  #72
  Sep 20, 2015
  Joined: Apr 20, 2015
  Messages: 584
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Hapa kazi tu,Magufuli hoyeeeee
   
 14. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #73
  Sep 20, 2015
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  makufuli na ccm ni janga la kitaifa
   
 15. hunchback

  hunchback JF-Expert Member

  #74
  Sep 20, 2015
  Joined: Nov 10, 2014
  Messages: 598
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45

  Attached Files:

 16. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #75
  Sep 20, 2015
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  ccm ni janga la kitaifa

  kama kipindupindu, ebola na dengue
   
 17. s

  sensor JF-Expert Member

  #76
  Sep 20, 2015
  Joined: Jan 27, 2015
  Messages: 2,472
  Likes Received: 837
  Trophy Points: 280
  Hii makala ni mojawapo ya zilizomfanya apewe shavu magogoni ili kumfunga mdomo
   
 18. Jp Omuga

  Jp Omuga JF-Expert Member

  #77
  Sep 20, 2015
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 2,784
  Likes Received: 942
  Trophy Points: 280
  Utofauti unaosema upo kwenye habari..
  Kuhusu habari ya Magufuli ccm imeilipa CNN hela nyingi sana ili waondoe habari hiyo na picha zake zote... You will find it no where...!!
   
 19. S

  Swat JF-Expert Member

  #78
  Sep 20, 2015
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 4,191
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Habari ya kale sana hii na iloshatolewa majibu. Tunaomba mlete vitu vya motomoto
   
 20. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #79
  Sep 20, 2015
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 12,852
  Likes Received: 17,426
  Trophy Points: 280
  Richmond ya juzi?
  Basi tuambie aliyebeba viroba vya Escrow ni nani hii bado motomoto.
   
 21. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #80
  Sep 20, 2015
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Makufuli na ccm ni janga la kitaifa

  kama kipindupindu, ebola na dengue
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...