Bomu linalomwandama Magufuli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bomu linalomwandama Magufuli

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by EasyFit, Sep 19, 2015.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2015
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,263
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Habari hii ilichapishwa kwenye gazeti la RAI miaka michache iliyopita ikisomeka...

  Huyu Ndiye Pombe Magufuli:

  - Wasema nyumba 8,000 kauza kwa mkono wake mwenyewe
  - Apuuza maonyo ya wataalamu- Mafaili ya Sundi na Musa aliyabeba kwapani

  ALIYEKUWA Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, katika Serikali ya awamu ya tatu, aliteka madaraka na kuwa mwenyekiti wa zoezi la kuuza nyumba za serikali ambazo hadi sasa, zimeshauzwa 8,288 imefahamika.

  Habari zilizopatikana ndani ya wakala wa Majengo ya Serikali (TBA), zimethibitishia Rai wiki hii kwamba Magufuli alihakikisha anashiriki kama Mwenyekiti katika zoezi zima la kuuza nyumba, ambalo kimsingi lilistahili kusimamiwa na Mtendaji Mkuu wa TBA.

  Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari ndani ya TBA, Magufuli alifanya kila aina ya ‘fujo’ katika zoezi la kuuza nyumba hizo, wakati mwingine akibatilisha maamuzi yaliyofanywa na Kamati ya TBA ya kuuza nyumba hizo, akiwapangia watu nyumba kwa utashi wake na wakati mwingine akiwakemea wale wote waliomshauri kinyume na matakwa.

  Ni chini ya utaratibu huo, habari zinaeleza kwamba Magufuli, aliyabeba yeye mwenyewe mafaili ya ndugu zake; Musa Magufuli ambaye ni mdogo wake, na Sundi Malomo ambaye ni mzazi mwenzake na kuwalazimisha watendaji wa TBA wafuate matakwa yake katika kuwapatia nyumba ndugu zake hao.

  Habari hizo zinaeleza kwamba awali Mtendaji Mkuu wa TBA alimshauri Magufuli kwamba suala la mauzo ya nyumba kwa ndugu zake ni kinyume cha utaratibu. Hata hivyo, imeelezwa kwamba Magufuli alilazimisha huku akisema mdogo wake hana tatizo kwa sababu alikuwa tayari mfanyakazi wa Serikali.

  Musa aliajiriwa kwa mkataba wa miezi mitatu, baada ya mwezi mmoja akauziwa nyumba na baada ya miezi miwili akaacha kazi.

  “Kwa upande wa Sundi, kwanza ilikuwa Sundi auziwe nyumba moja kwa moja. Lakini Magufuli alipoonywa akashtuka na kusema suala hilo aachiwe yeye mwenyewe. Na ndipo akaibuka na jina la Stanley Manongi kwamba ndiye mnunuzi halisi na baba yake Sundi,” vinasema vyanzo hivyo vya habari, vingine ambavyo vilishiriki moja kwa moja katika mchakato wa uuzaji nyumba hizo.

  Habari hizo zinaendelea kueleza kwamba baadaye, Sundi alishtuka akitilia shaka uaminifu wa Manongi, kwamba angeweza kumdhulumu nyumba hiyo.

  “Ndipo Magufuli aliibuka na mpango wa Sundi kuwa mtoto wa Manongi na mrithi wake na kisha kwa kuhakikisha kwamba hakuna dhuluma yoyote, mtoto wa Sundi naye akarithishwa na kama mrithi wa pili,” chanzo hicho cha habari kinaeleza.

  Chini ya sheria ya Executive Agency Act No. 30 ya mwaka 1997, TBA ilipewa madaraka yote ya kuuza nyumba za Serikali, kujenga nyumba mpya, kuzikarabati zilizopo pamoja na kugawa nyumba za madaraja A, B na C kwa wafanyakazi wa Serikali.

  Sheria hiyo inaipa mamlaka ya kipekee ya kufanya shughuli zote bila kuingiliwa na chombo chochote.

  Chini ya sheria hiyo, Waziri anaruhusiwa kuteua wajumbe wa bodi ya ushauri watakaomshauri Katibu Mkuu wa Wizara juu ya namna nzuri ya TBA kusimamia mamlaka yake.

  Hadi Machi mwaka huu, wajumbe hao walikuwa ni J. Kijazi, E. Lipambila, E. Lugwisha, Msangi, E. Mwakalinga, D. Kisasi, P. Ncheye, F. Werema na A. Bukuku.

  Hata hivyo, sheria haitoi nafasi yoyote kwa Waziri kusimamia shughuli za uuzwaji au upangaji wa nyumba za serikali.

  Mtendaji Mkuu wa TBA Togolayi Makumba Kimweri, alipoulizwa kupitia kwa Katibu Muhtasi wake, alimwambia mwandishi wa Rai aandike maswali kisha asubiri kuruhusiwa kuingia ndani ya ofisi.

  Hata hivyo, baada ya kusubiri kwa muda wa saa moja, mwandishi alipokwenda kuuliza akaambiwa kwamba Kimweri tayari alikwishaondoka ofisini kupitia mlango wa nyuma na asingeweza kurudi ofisini.

  Lakini baadhi ya wafanyakazi wa TBA wameiambia Rai kwamba kinachoandikwa kwenye magazeti kuhusu ushiriki wa Magufuli kuuza nyumba za Serikali ni kidogo mno kuliko hali halisi.

  Kama ilivyokuwa kwa mdogo wake Musa, waziri Magufuli alishinikiza mtoto wa dada yake anayeitwa James Doto Mgosha auziwe nyumba za serikali kwa kumtengenezea ajira ya muda mfupi katika TANROADS.

  Tofauti na Musa, Doto ameuziwa nyumba hiyo kwa jina la mtu mwingine lakini anaishi katika nyumba hiyo, namba 64 iliyopo Kinondoni Flats.

  Habari kutoka TBA zinaonyesha jina la mtu mwingine (tunalihifadhi) kuwa ndiye aliyeuziwa nyumba hiyo mtu huyo alipata kupitia utaratibu wa Magufuli kupeleka jina lake kwenye wakala wa majengo na kulazimisha apewe nyumba.

  Alipoulizwa kwa njia ya simu, Doto alisema suala la ajira na nyumba waulizwe waliomwajiri na kumpa nyumba. Akakata simu.

  Mfanyakazi mwingine alieleza Rai kwamba msichana mwingine (jina tunalihifadhi) akiwa na miezi minne tu kazini alipelekwa na Magufuli katika Wakala wa Majengo akilazimisha auziwe nyumba hata kabla ya kuthibitishwa kazini. Nyumba hiyo iko Block A, Ocean Road.

  Hata hivyo, habari hizo zinaeleza kwamba msichana huyo ambaye hadi sasa anaishi na wazazi wake, ameipangisha nyumba hiyo kwa mfanyakazi mmoja wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa na analipwa kwa dola za kimarekani.

  “Kuuza nyumba za serikali sawa, lakini kweli katika mtindo huu? Sisi tunaoshiriki kuzikagua na kuziratibu tukiomba hatupati, lakini wengine wanaingia serikalini miezi miwili wanapata nyumba. Na wengine hata si wafanyakazi, wanapata, hii si sahihi, alilalamika mfanyakazi mmoja aliyeandikia Rai kwa njia ya barua pepe.

  Hadi Machi mwaka huu Wakala wa Majengo wa Serikali (TBA) walishauza nyumba 8,288 ambazo hata hivyo zilitakiwa kuuzwa kwa watumishi wa serikali.

  Katika mauzo hayo, Serikali ilitarajia kupata jumla ya shilingi 60,016,556,439.00. Hata hivyo hadi sasa Serikali imepata shilingi 22,684,108,115.08.

  Kwa sasa, Serikali imebakiwa na nyumba 1,098 zinazosimamiwa na TBA. Kati ya hizo, nyumba 692 zimetengwa kwa wafanyakazi wa Serikali, nyumba 675 kama tied quarters, nyumba 111 zinatumika kama Rest House za Serikali, wakati nyumba 40 zinatumika kama state lodges. Nyumba 24 zinatumika kama ofisi na nyingine 29 ni kama karakana na bohari.

  SALVA RWEYEMAMU
  RAI
   
 2. n

  neneso Member

  #2
  Sep 19, 2015
  Joined: Nov 7, 2014
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii nayo si ya kunyamazia
   
 3. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2015
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,211
  Likes Received: 603
  Trophy Points: 280
  Hii itafutwa muda mfupi ujao
   
 4. Kitaturu

  Kitaturu JF-Expert Member

  #4
  Sep 19, 2015
  Joined: Apr 13, 2013
  Messages: 4,103
  Likes Received: 2,255
  Trophy Points: 280
  Hii ni makala ya huyu huyu Salva Rweyemamu aliyeko ikulu leo kama Afisa habari?

  Lakini ukimwambia atoe msimamo wake wa hiki alichokiandika zaidi ya miaka 10 iliyopita, ataruka kimanga balaa!!

  Madaraka na hela ni noma sana, unaweza kumkana hata mama yako!!
   
 5. wirewizard1

  wirewizard1 Senior Member

  #5
  Sep 19, 2015
  Joined: Jun 28, 2015
  Messages: 151
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Habari kama hizi ndg zetu wana CCM ...Hawazitaki kuziona..!!!@Tusubiri octoba 25....?
   
 6. kson m

  kson m JF-Expert Member

  #6
  Sep 19, 2015
  Joined: Jan 24, 2014
  Messages: 5,511
  Likes Received: 1,696
  Trophy Points: 280
  Uharamia mchana kweupe!!!
   
 7. fundi25

  fundi25 JF-Expert Member

  #7
  Sep 19, 2015
  Joined: Apr 16, 2013
  Messages: 5,839
  Likes Received: 2,836
  Trophy Points: 280
  Ccm inanuka
   
 8. D

  David Elia Senior Member

  #8
  Sep 19, 2015
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Magufuli kaooza!!!!! Rais wa Kuwait ni Gadaffi.....what? Mwizi no 1
   
 9. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #9
  Sep 19, 2015
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,445
  Likes Received: 349
  Trophy Points: 180
  Alisema Saddam
   
 10. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #10
  Sep 19, 2015
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,707
  Likes Received: 5,590
  Trophy Points: 280


  Alisema Saddam ni wa Libya, akasema tena hapana, ni wa KUWAIT... eeehh.. Saddam wa KUWAIT mnajua...? Ghadaffi je wa IRAQ je mmemsikia..? na Salva Kiir wa Ethiopia je..? eeeh na Mohammed Morsi wa SOMALIA... sasa msicheze na Amani... pia mnamjua Kabila wa Burundi... kuweni makini na Amani...!!!

  Yaani....

  😨😨😨😨😨😨😨😷😷😷😷😠😠😠
   
 11. kivava

  kivava JF-Expert Member

  #11
  Sep 19, 2015
  Joined: Apr 2, 2013
  Messages: 5,519
  Likes Received: 4,201
  Trophy Points: 280
  Ahaa....kumbe ana nyumba ndogo,atakuwa..rais....
   
 12. a

  analaizi JF-Expert Member

  #12
  Sep 19, 2015
  Joined: Mar 8, 2014
  Messages: 1,351
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hivii ule uzi wenye email iliyotumwa kwa Dr ambao umetembea leo umeliwa na kirusi gani!
   
 13. MTENGETI

  MTENGETI JF-Expert Member

  #13
  Sep 19, 2015
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,365
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Mwenye kipande cha hilo gazet tukutane pm! Kama vip nitamtoa vizur tu. Nina kaz nacho siku mavimwana au sadam wa kuwait akiingia klm vitamhusu
   
 14. k

  kasinge JF-Expert Member

  #14
  Sep 19, 2015
  Joined: May 22, 2011
  Messages: 1,262
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Ngoja niikopi kwanza, kwa records.
   
 15. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #15
  Sep 19, 2015
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,510
  Likes Received: 7,586
  Trophy Points: 280
  Magufuli kama unasoma hapa,kamuombe mkeo msamaha,hata mimi niliekuwa kambi yako mdogo mdogo.Yaani laana ya mke wako inakufuata.Ukweli popularity yako inapungua kila kukicha
   
 16. Maarifa

  Maarifa JF-Expert Member

  #16
  Sep 19, 2015
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 2,975
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Je zimeuzwa kwa hasara? Je serikali ilikuwa wapi kuzikarabati? Je ni lazima serikali kuwa ma nyumba lukuki bila repair? Mie shida si magufuli. Shida ni mfumo wa uzandiki wa ccm. Haifai
   
 17. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #17
  Sep 19, 2015
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,263
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Jiulize pia waliouziwa walikuwa na sifa?
   
 18. Kayoka

  Kayoka JF-Expert Member

  #18
  Sep 19, 2015
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,470
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Natamani nipate nafasi, jukwaa na wasaa sijui nitapata wapi. Nataka kuwaeleza UKWELI kama huu wale NZI wa kijani na madoadoa ya NJANO walioko huko chooni na wanaoamshabikia na kumsujudia KINYESI cha maharage ya SOYA toka huko kaskazini magharibi mwa TAWALANYIKA kuwa hafai hata kidogo licha ya kuahidi neema tele kwa MENDE wake, yeye mwenyewe na washirika wake.
  *MABADILIKO*
   
 19. Cham Bee

  Cham Bee JF-Expert Member

  #19
  Sep 19, 2015
  Joined: Feb 10, 2015
  Messages: 3,401
  Likes Received: 1,444
  Trophy Points: 280
  jeuri+pumba+majivuno=jpm
   
 20. M

  MTENDAHAKI JF-Expert Member

  #20
  Sep 19, 2015
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,007
  Likes Received: 947
  Trophy Points: 280
  Kama mbowe alivyoikana falsafa ya kupambana na ufisadi na kumkumbatia fisadi papa
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...