Bomu la ajira

Bomu la ajira

technically

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
13,634
Reaction score
58,270
Unatoa elimu Bure kuanzia darasa la kwanza mpaka form four...

Unatoa mkopo chuo kikuu miaka mitatu..

Unamwandaa kijana awe mwalimu na sio fani nyingine yeyote....

Kijana anamaliza degree hana kazi yupo mtaani unategemea akafanye kazi gani?.....

Si ni bora wangeandaliwa walimu wachache wanaoweza kuajiriwa kirahisi?.....

Tukiongea tunaambiwa wapiga dili hasa mtu kusoma kutoka darasa la kwanza mpaka chuo kikuu unafikiri anakuwa kapoteza kiasi gani cha pesa za serikali na za wazazi je izo pesa zinarudi vipi kama ni jobless?..

Tufike wakati tuwe na uchungu kwa vijana wanaosoma kwa shida kiukweli ni mateso ..

Serikali itoe ajira watu warudishe mikopo walipe kodi wengine wasome kama hatutoi ajira maana yake kuna muda utafika hata pesa ya kukopesha wanafunzi itakosa...

Serikali imetengeneza walimu walio mtaani 91,000 na mwezi wa saba wengine wanamaliza wewe unatoa ajira 4500 ambao hata 10% haifiki ..

Halafu wanafunzi hawana walimu uko shuleni wanakaa chini .

Walimu waliopo hawalipwi vizuri tuwe na uchungu jamani mambo haya ndio mambo ya msingi tuwe na hofu ya Mungu.

Akiba ya pesa tunaambiwa ipo si tuwape wadogo zetu ma watoto wetu kazi ?

Kodi sasa hivi si inalipwa kwa wakati sasa shida nini kuwapa kazi wadogo zetu na watoto wetu...?

Hata mkisema mimi sio mzalendo au mimi ni mpiga dili sawa tu nimeshazoea ila nitaongea ukweli mpaka naenda kaburini...

20190328_074435.jpeg
 
Ndugu kuna shule unakuta ina waalimu wawili au wanne tu... Na hii ni kwa shule ya msingi na sekondari pia. Unabaki unajiuliza hivi waalimu waliohitimu ambao kila siku tunapishana nao mtaani kwa nini wasiajiriwe kwenda kusaidia maeneo yenye upungufu? Unakosa jibu.. Kila siku wahitimu wanajazana mtaani, hakuna ajira, ni wachache tu wanaoweza kujiajiri au kuajiriwa na sekta binafsi... Wengine wote wanategemea ajira serikalini. Hali ni ngumu sana huku mtaani sio jambo la kusema taratibu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo la wasomi Wengi wanachugua chagua sana kazi mbona wengine tushafanya hadi kazi za kujitolea ili kuonesha uwepo ukikaa nyumbani ukasubiri ajira trust me utafika mwaka wa kustaafu na bado hujaajiriwa
 
Serikali ya awamu ya tano haipambani na tatizo la ajira nchini ndio maana Magufuli huwezi kumsikia akizungumzia tatizo hilo.

Awamu hii haipambani na tatizo la umasikini nchini ndio maana huwezi kumsikia Magufuli akizungumzia ni kwa kiasi gani amepunguza tatizo la umasikini nchini.

Hazungumzii uboreshaji wa kilimo nchini.

Hazungumzii matatizo ya uhaba wa walimu nchini.

Magufuli yeye hupenda mambo ya kiki au drama, maana utasikia amekamata vichwa chwa treni havina mwenyewe, mara tutaongea na mwenyewe tuvinunue (asiyekuwapo kwa mujibu wa Magufuli), hahahaha hivi ndivyo hupenda Watanzania kuliwalisha matongo pori.

Tukaambiwa alikamata magari ya kifahari ambayo hayana kibali ya kuingia nchini, kumbe yalikuwa na vibali vyote vya kuingia nchini.

Magufuli kama kiongozi aache porojo ajikite kuwaeleza Watanzania taifa linaelekea wapi kiuchumi, kisiasa, kidplomasia, mapinduzi ya kilimo, n.k
 
Unatoa elimu Bure kuanzia darasa la kwanza mpaka form four...

Unatoa mkopo chuo kikuu miaka mitatu..

Unamwandaa kijana awe mwalimu na sio fani nyingine yeyote....

Kijana anamaliza degree hana kazi yupo mtaani unategemea akafanye kazi gani?.....

Si ni bora wangeandaliwa walimu wachache wanaoweza kuajiriwa kirahisi?.....

Tukiongea tunaambiwa wapiga dili hasa mtu kusoma kutoka darasa la kwanza mpaka chuo kikuu unafikiri anakuwa kapoteza kiasi gani cha pesa za serikali na za wazazi je izo pesa zinarudi vipi kama ni jobless?..

Tufike wakati tuwe na uchungu kwa vijana wanaosoma kwa shida kiukweli ni mateso ..

Serikali itoe ajira watu warudishe mikopo walipe kodi wengine wasome kama hatutoi ajira maana yake kuna muda utafika hata pesa ya kukopesha wanafunzi itakosa...

Serikali imetengeneza walimu walio mtaani 91,000 na mwezi wa saba wengine wanamaliza wewe unatoa ajira 4500 ambao hata 10% haifiki ..

Halafu wanafunzi hawana walimu uko shuleni wanakaa chini .

Walimu waliopo hawalipwi vizuri tuwe na uchungu jamani mambo haya ndio mambo ya msingi tuwe na hofu ya Mungu.

Akiba ya pesa tunaambiwa ipo si tuwape wadogo zetu ma watoto wetu kazi ?

Kodi sasa hivi si inalipwa kwa wakati sasa shida nini kuwapa kazi wadogo zetu na watoto wetu...?

Hata mkisema mimi sio mzalendo au mimi ni mpiga dili sawa tu nimeshazoea ila nitaongea ukweli mpaka naenda kaburini...

View attachment 1056404
Hapo tu ndo nimeona JPM hamna kabisa aisee....yaan unakamua watu mpak machinga na mikopo juu ili ufanikishe miradi ambayo ni secondary na sio primary....hli la vijana kusota mtaa nalifahamu kabisa kuna vijana mtaani mpak wanatia huruma aisee..wamemaliza degree za ualimu wapo tuu na ni watoto wa maskini kwel kweli, bora hata sie tuliopata channel za harakat za mtaa na degree zetu za tourism....
 
Jiwe angetakiwa afanye kama waliomtangulia. Kila mwisho wa mwezi, Rais anazungumza na Taifa kupitia Tv na redio. Kipind kile nakumbuka tunafatlia kipind kupitia ITV kila saa 3 usiku. Angefanya hivy angalau angeongeza agenda za kushughulika nazo vizur ili mwsh wa mwez aongeleee na kila kipande cha maisha ya watu kingeguswa na siyo kukaa anavyokaaa tu saiv akijisikia kuwa kweny magazet,anajiachia tuu
 
G

We hataki kabsa hyo kitu ninyi watoto wa cku hz mnahoji kila kitu na yy hataki kuhojiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unatoa elimu Bure kuanzia darasa la kwanza mpaka form four...

Unatoa mkopo chuo kikuu miaka mitatu..

Unamwandaa kijana awe mwalimu na sio fani nyingine yeyote....

Kijana anamaliza degree hana kazi yupo mtaani unategemea akafanye kazi gani?.....

Si ni bora wangeandaliwa walimu wachache wanaoweza kuajiriwa kirahisi?.....

Tukiongea tunaambiwa wapiga dili hasa mtu kusoma kutoka darasa la kwanza mpaka chuo kikuu unafikiri anakuwa kapoteza kiasi gani cha pesa za serikali na za wazazi je izo pesa zinarudi vipi kama ni jobless?..

Tufike wakati tuwe na uchungu kwa vijana wanaosoma kwa shida kiukweli ni mateso ..

Serikali itoe ajira watu warudishe mikopo walipe kodi wengine wasome kama hatutoi ajira maana yake kuna muda utafika hata pesa ya kukopesha wanafunzi itakosa...

Serikali imetengeneza walimu walio mtaani 91,000 na mwezi wa saba wengine wanamaliza wewe unatoa ajira 4500 ambao hata 10% haifiki ..

Halafu wanafunzi hawana walimu uko shuleni wanakaa chini .

Walimu waliopo hawalipwi vizuri tuwe na uchungu jamani mambo haya ndio mambo ya msingi tuwe na hofu ya Mungu.

Akiba ya pesa tunaambiwa ipo si tuwape wadogo zetu ma watoto wetu kazi ?

Kodi sasa hivi si inalipwa kwa wakati sasa shida nini kuwapa kazi wadogo zetu na watoto wetu...?

Hata mkisema mimi sio mzalendo au mimi ni mpiga dili sawa tu nimeshazoea ila nitaongea ukweli mpaka naenda kaburini...

View attachment 1056404
Ajira sio bomu kwa muono wangu, ila "uipotezea" na kuchukulia poa nguvu kazi ya vijana na akili zao kuzalisha ili kukuza uchumi ni hasara kubwa.

Kiuhalisia Serikali haina nafasi nyingi sana za ajira ukilinganisha na Sekta binafsi mbayo ina fursa ya kukua kila siku. Na tukumbuke Sekta binafsi ndiyo ilipelekea kuanzishwa kwa NPF ambayo baadae ikaja kuwa NSSF, taasisi ambayo inakuwa kutokana na makato ya 10% toka kwa mishahara ya wafanyakazi na 10% toka kwa muajiri.

Wizara ya fedha ingekuwa na watu wanaofikiri nje ya box inge-facilitate soft loans iki kukuza industrial farming, hii ingekuza, agro-processing ambayo iki-peak sekta wezeshi za huduma kama Elimu, Uhasibu, Masoko, Afya, Usafirishaji, Mabenki, Bima, Sheria, zinawachukua wasomi wetu.

Bahati mbaya, kuna watu ambao huwa hawataki kusikiza mawazo mbadala. Wapo confined kwenye what is named policies and regulations.
Policies zetu nyingi ni za miaka ya 90. Leo miaka zaidi ya 20 bado tunatumia policies ambazo haziko compatible na uchumi wa karne ya 21.
Ubaya kuna watu walisomaga wakapata PhD miaka ya 90 ndiyo hao wanajiona wanajua kila kitu.
Anyway tuendelee kuvuta subra, maana ndicho tumekuwa tukiaminishwa, wakati wenzetu muda kwao ni fursa ya kutengeneza hela na kukuza uchumi.
Kuna Mtanzania ninamfahamu, aliwahi kupeleka business model ya kiwanda kwa "wakubwa" ambapo FURSA hiyo ingeweza kutoa ajira zaidi ya 100 kwa mkupuo na kila mwaka kulikuwa na room ya expansion . Washua wa serikalini walimpotezea kana kwamba that could not happen
 
Ajenda yake kuu ni kusomesha watu no ili apate Furaha.Mambo yasiyo na kiki yaani yasiyo ya macamera mfano kuongeza ajira,kuinua Kilimo, nk hayana nafasi kwake,yye ni makatazo,fungia,kamata,tunga Sheria komozi za kunyoosha watu mda wake utaaisha na atowamaliza,hadi sasa kaua shughuli laki 3 zilizoajiri Jumla ya watu Milioni 2 wako nje ya ajira sababu ya matamko,makatazo,chuki kwa matajiri waliofanikiwa.Ajatengeneza ajira mpya zaidi ya kuzibomoa kuzipunguza hata zilizopo kwa kuleta itikadi zilizofail duniani kote za kijamaa monopoly of business kwenye ulimwengu wa sasa uliobadilika kwa kila kitu.Kwake ttzo la ajira litazidi na ndilo Bomu apambane nalo kwani limemjengea chuki kwa wasio na ajira.
 
Unatoa elimu Bure kuanzia darasa la kwanza mpaka form four...

Unatoa mkopo chuo kikuu miaka mitatu..

Unamwandaa kijana awe mwalimu na sio fani nyingine yeyote....

Kijana anamaliza degree hana kazi yupo mtaani unategemea akafanye kazi gani?.....

Si ni bora wangeandaliwa walimu wachache wanaoweza kuajiriwa kirahisi?.....

Tukiongea tunaambiwa wapiga dili hasa mtu kusoma kutoka darasa la kwanza mpaka chuo kikuu unafikiri anakuwa kapoteza kiasi gani cha pesa za serikali na za wazazi je izo pesa zinarudi vipi kama ni jobless?..

Tufike wakati tuwe na uchungu kwa vijana wanaosoma kwa shida kiukweli ni mateso ..

Serikali itoe ajira watu warudishe mikopo walipe kodi wengine wasome kama hatutoi ajira maana yake kuna muda utafika hata pesa ya kukopesha wanafunzi itakosa...

Serikali imetengeneza walimu walio mtaani 91,000 na mwezi wa saba wengine wanamaliza wewe unatoa ajira 4500 ambao hata 10% haifiki ..

Halafu wanafunzi hawana walimu uko shuleni wanakaa chini .

Walimu waliopo hawalipwi vizuri tuwe na uchungu jamani mambo haya ndio mambo ya msingi tuwe na hofu ya Mungu.

Akiba ya pesa tunaambiwa ipo si tuwape wadogo zetu ma watoto wetu kazi ?

Kodi sasa hivi si inalipwa kwa wakati sasa shida nini kuwapa kazi wadogo zetu na watoto wetu...?

Hata mkisema mimi sio mzalendo au mimi ni mpiga dili sawa tu nimeshazoea ila nitaongea ukweli mpaka naenda kaburini...

View attachment 1056404
Tatizo watanzania wengi tena waliotumia kodi za wananchi na kupata elimu hawana maono na nchi yao, wanaongoza nchi inayolea watanzania wenzao bila hata kutafakari . Ajira hakuna, secta binafsi zinazotemewa na walalaoi wengi( shule ,vyuo na viwanda) vinafungwa , bei ya vifaa vya ujenzi znapanda, wafanyakazi hawaongezewi mishahara, walimu hawapandi madaraja, Halafu mtu kirahc tu anaama chama kuunga juhudi na akijua kabsa kabsa kodi za wananch wlalahoi znaenda kutumika kwa Mara ya pili bila sababu ya msingi, Mtu anaandaa maandamano kumpongeza ununuzi wa ndege hata hajui hatapanda lini. MUNGU SAIDIA TANZANIA MY COUNTRY.
 
Back
Top Bottom