figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,720
- 55,843
BOMOABOMOA DAR: Ubomoaji nyumba zilizojengwa bila kufuata utaratibu na zile zilizopo mabondeni, waanza tena Suna Kinondoni leo, huku uamuzi wa kesi ya kupinga zoezi hilo ukitarajiwa kutolewa leo.
Sakata la bomoabomoa kwa wakazi wa mabondeni lilichukua sura mpya baada ya mbunge wa Kinondoni (CUF), Maulid Mtulia kufungua kesi katika Mahakama kuu ya Ardhi kupinga ubomoaji wa nyumba bila kutoa njia mbadala za makazi. Lakini hilo hawajali, wanaendelea na ubomoaji.
Kesi hiyo jana iliahirishwa. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba alisema hadi jana walikuwa hawajapokea zuio lolote la mahakama, hivyo operesheni hiyo itaendelea.