Wakazi Kurasini wagoma kuhama
na Deogratius Temba
Walisema mwaka 2006, wakati tathmini ilipofanyika mfuko mmoja wa saruji ulikuwa unauzwa sh 5,000, lakini sasa hivi ni kati ya sh 10,000 na 12,000, hivyo wangepaswa kuongezewa fedha, ili zikidhi gharama za wakati huu na mabadiliko ya gharama za vifaa vya ujenzi.
Pia wakazi hao walilalamikia kauli ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Chiligati, kuwa wakazi hao walilipwa sh milioni 20 kila mmoja kama fidia.
Walisema kauli hiyo ya Chiligati si ya kweli, kwani kuna watu waliolipwa mpaka sh milioni 1.5 kwa gharama zote
.
Source: Tanzania Daima
Waliobomolewa nyumba Kurasini wadai waziri amesema uongo
Na Furaha Kijingo
WAKAZI waKurasini Zam Cargo, Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam wamesikitishwa na kauli iliyotolewa bungeni na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Chiligati, kwamba kila mmoja amelipwa fidia zaidi ya Sh100m ili kupisha ujenzi wa bandari katika eneo hilo.
Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti wakazi hao walisema kauli ya waziri ni ya uongo kwani hakuna mtu aliyelipwa kiasi cha fedha hizo kati yao na kudai kuwa walizolipwa hazilingani na gharama za ujenzi na hata hadhi ya nyumba zao. Mkazi wa eneo hilo, Shen Azad Shen(63) alisema, waziri amedanganywa kabisa na kuongeza: "Amekubali kupokea uongo huo, fedha walizosema tumelipwa si kweli, mi nimelipwa Sh16 milioni na nyumba yangu ina zaidi ya thamani ya Sh50 milioni. Kwanini Waziri anadanganywa na anakubali, halafu anakurupuka na kuongea kwa uhakika bungeni?
Shen alisema hata madai ya kuwa kesi yao inayohusu mgogoro huo wameshindwa si ya kweli kwani bado itasikilizwa tena Oktoba16, mwaka huu katika Mahakama Kuu ya Ardhi.
Naye Abdallah Pogola Abdallah(54) alisema alilipwa ni Sh10 milioni na hata alipojaribu kufuatilia wizarani alipewa mchanganuo mzima wa jinsi atakavyolipwa inaonyesha kwamba alitakiwa kulipwa Sh24 milioni. Naye Mary Kiula alisema kuwa bomoabomoa hiyo haijawatendea haki ikilinganishwa na thamani ya nyumba zao nakudai kwamba kitendo cha askari kwenda na mbwa kuwaondoa kinaashiria kwambawaliobomolewa walikuwa wanadai haki.
''Mimi na wanangu sasa tunakwenda kukaa kwa mdogo wangu, fedha niliyolipwa haitoshi, nilipowauliza walijibu,' si ulipenda mwenyewe kujenga nyumba ya gharama,'' alilalamika Kiula.
Source : Mwananchi
-Inaonekana mawaziri wetu hawachambui vizuri taarifa wanazopelekewa, ambayo kwa kiasi fulani inaichafua serikali na pole pole inajenga watu kuichukia serikali.
-Kuna tuhuma nyingi sana hapo ardhi kuwa kwenye matukio kama haya watendaji wa wizara ya ardhi wanatumia kujitajirisha ....mfano hapo juu evaluation in 24M unlipwa 10M ....nyingine zinakwenda wapi?
-Evaluation zinafanywa leo unalipwa baada ya miaka miwili mpaka mitano ....nadhani hapo kuna jambo la kuwakosea haki wananchi.