Bomoabomoa itakavyoyumbisha taasisi za kifedha

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,169
Reaction score
48,451
Jana nilipokuwa naangalia kwenye mitandao ya kijamii niliona picha mbali mbali za bomoabomoa ya nyumba inayoendelea Dar es salaam. Pamoja na huzuni, hasira, navilio vilivyokuwa vimetawala zoezi hilo, mimi kwa mtizamo wangu nimeona kwamba zoezi lenyewe litaziathiri sana taasisi za kifedha na uchumi wa nchi kwa ujumla.

Kati ya nyumba zilizobomolewa miongoni mwake kuna nyumba ambazo ziliwekwa dhamana kwa mikopo pia kuna nyumba ambazo zilitumika kama ni anwani za wakopaji. Na kwenye maeneo hayo pia kuna nyumba zilizokuwa zinatumika kama nyumba za biashara zilizotathiminiwa kupata kigezo cha kukopeshwa.

Nyumba za aina hiyo zinapobomolewa zinaleta sintofahamu kubwa sana kwa taasisi za kifedha. Kwa mfano nyumba iliyowekwa dhamana na mkopaji imebomolewa na nyumba iliyotumika kama anwani ya mkopaji nayo imebolewa, na eneo ilikokuwa inafanyika biashara iliyokopeshwa nayo imebomolewa. Hapa taasisi ya kifedha iliyokopesha inawezaje kulipwa?

Halafu eneo lote linalobomolewa, serikali imewahi kujua ni biashara ya thamani kiasi gani ilikuwa inafanyika kwenye eneo hilo? Leo wote waliokuwa wanawazuia bidhaa wafanyabiashra wa eneo hilo wamepoteza wateja na waliokuwa wateja nao wamepoteza mitaji. Ni kwa kiasi gani biashara iliyopootezwa kwenye eneo hilo italeta athari kwenye uchumi wa Dar es salaam na Taifa kwa ujumla?

Wafanyakazi wa serikali ambao watakuwa wanashughulika na matokeo ya ubomoaji huo,ni kwa kiasi gani watashusha ufanisi wao kazini na pia wanawezaje kuhimili makato ya mikopo yao waliyokopa ili kuendeshea shughuli za kujiongezea kipato kwenye maeneo nyumba zilikobomolewa?
 
kweli mkuu ukumbi wa harusi kama kilato pale kimara ni uwekezaji mkubwa sana... kitendo cha kuubomoa kama ana loan bank anaweza asilipe na usimfanye chochote maana dhamana imevunjwa... au mama kapinga pale
Halafu ukiangali kwa undani ni kama dhuluma fulani hivi. Hawa watu wanaoambiwa hawakuwa pale kihalali, ni wao walikuwa wanalipa kodi, wanakata leseni za biashara na kulipa tozo mbali mbali za kibiashara na wengine Kampuni zao zimesajiliwa Brela kwa kutumia eneo hilo hilo ambalo leo wanaambiwa hawako kihalali. Ina maana serikali ilikuwa inajishughulisha na wafanyabiashara haramu?
 
sidhani kama bima watakubali kulipa. hasa huko benki kwenye mikopo
 
Hao waliovunjiwa wana hati za viwanja husika?
Swali la msingi kabisa. mimi tangu mwaka 1998 nafuatilia kupimiwa na kupewa hati ya kiwanja changu na mpaka leo sijafanikiwa. Lakini serikali yenyewe inayatambua maeneo yaliyopimwa na yasiyopimwa kisheria.

Hapo kinachobomolewa si ardhi ambayo haijapimwa bali yanabomolewa majengo ambayo yako kisheria na ndiyo maana kwenye maeneo yaliyobomolewa nyumba kuna serikali za mitaa!
 
Jana nilipokuwa naangalia kwenye mitandao ya kijamii niliona picha mbali mbali za bomoabomoa ya nyumba inayoendelea Dar es salaam. Pamoja na huzuni, hasira, navilio vilivyokuwa vimetawala zoezi hilo, mimi kwa mtizamo wangu nimeona kwamba zoezi lenyewe litaziathiri sana taasisi za kifedha na uchumi wa nchi kwa ujumla.

Kati ya nyumba zilizobomolewa miongoni mwake kuna nyumba ambazo ziliwekwa dhamana kwa mikopo pia kuna nyumba ambazo zilitumika kama ni anwani za wakopaji. Na kwenye maeneo hayo pia kuna nyumba zilizokuwa zinatumika kama nyumba za biashara zilizotathiminiwa kupata kigezo cha kukopeshwa.

Nyumba za aina hiyo zinapobomolewa zinaleta sintofahamu kubwa sana kwa taasisi za kifedha. Kwa mfano nyumba iliyowekwa dhamana na mkopaji imebomolewa na nyumba iliyotumika kama anwani ya mkopaji nayo imebolewa, na eneo ilikokuwa inafanyika biashara iliyokopeshwa nayo imebomolewa. Hapa taasisi ya kifedha iliyokopesha inawezaje kulipwa?

Halafu eneo lote linalobomolewa, serikali imewahi kujua ni biashara ya thamani kiasi gani ilikuwa inafanyika kwenye eneo hilo? Leo wote waliokuwa wanawazuia bidhaa wafanyabiashra wa eneo hilo wamepoteza wateja na waliokuwa wateja nao wamepoteza mitaji. Ni kwa kiasi gani biashara iliyopootezwa kwenye eneo hilo italeta athari kwenye uchumi wa Dar es salaam na Taifa kwa ujumla?

Wafanyakazi wa serikali ambao watakuwa wanashughulika na matokeo ya ubomoaji huo,ni kwa kiasi gani watashusha ufanisi wao kazini na pia wanawezaje kuhimili makato ya mikopo yao waliyokopa ili kuendeshea shughuli za kujiongezea kipato kwenye maeneo nyumba zilikobomolewa?
Maendeleo hayaji bila bomoa bomoa. Si nyumba tu, hata misingi ya utu inabidi ibomolewe. Hujaona watu wa jinsia moja wanaoana, tena cha ajabu wengine ni wachungaji wa kondoo wanaoana na kondoo zao.

Misingi ya utu inabomolewa na kanisa linabariki kwa kuwa wameendelea itakuwa serikali kubomoa nyumba kupisha highways? Fikiri.
 
Kwa kweli Mkuu, suala la kumrudisha mtu nyuma kimaendeleo ni ukatili wa hali ya juu sana. Tunahumia sisi lkn wengine wasioijua hata bei ya kiberiti wanafanya wanavyojiskia. It pains!!!!!
Uzuri wasimamizi wakuu wa huo ubomoaji huwa hawaishi kwenye nyumba zao binafsi!
 
Back
Top Bottom