Bomoa bomoa usiku wa manane

Inkoskaz

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
6,350
1,500
Nakwazika kidogo ama sina ufahamu sana katika hili ndio maana nimejitosa humu kwa magwiji wa sheria nipate mwanga zaidi
Nikiwa katika pitapita zangu za misele ya friday night around saa sita usiku maeneo ya Tazara Veternary nimeshuhudia gari Canter ya manispaa Temeke ikiambatana na Landcruiser pickup ya manispaa piazikiwa na mgambo wenye nyundo na mitarimbo na Auxiliary police wenye bunduki wakishushwa katika bar moja na kuanza kuivunja huku wakitoa vitisho na bila kujali wateja waliokuwepo na hata mali mbalimbali wakiziharibu,sijui uhalali wa uwepo wa hiyo bar lakini maswali yangu machache yafuatayo yakipata ufafanuzi nitashukuru sana

1.Je zoezi la bomoabomoa kufanyilka usiku mkubwa ni halali,hata kama kuna amri ya mahakama ndio utekelezaji wake uwe usiku mkubwa,kama ni halali kwanini lifanyike muda huo?

2.zoezi hilo kufanyika bila taarifa kwa uongozi wa mtaa au mjumbe wa shina, polisi wala ushiriki wao ni sahihi?

3.Zoezi kusimamiwa na Raia mwenye kuhusishwa na dispute haileti picha ya rushwa

4.uvunjaji umefanyika ndani ya compound ya nyumba za Tazara,mbona hakukuwa na uwakilishi wala usimamizi kutoka menejimenti ya Tazara? Na hapo mamlaka ya manispaa inaingiaje katika eneo ambalo tayari ni milki ya Tazara?

5.La mwisho,eneo hilo lina baa nyingine zimezagaa,vibanda vya biashara na mifugo na yadi za magari ambazo ni hakika nadhani hazipo kisheria,swali linakuja kuwa mbona kama ni operesheni ya kuondoa aina hizo za structures mbona halikugusa bar nyingine za jirani zilizokuwa zinaendelea na biashara na structures nyingine?

tuelimishane kwa hayo
 
Top Bottom