Bomoa bomoa iliishia wapi?

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,115
3,863
Kama kuna watu bado wanaamini serikali hii itafanya kazi na kuwaletea watanzania maendeleo nawashangaa sana. Tujiulize ile bomoa bomoa iliyokuwa inaendelea iliishia wapi? Nyumba zilizojengwa holela ziliisha? Au bomoa bomoa ndiyo ilikuwa holela? Kama ilikuwa holela waliobomolewa watalipwa fidia?

Nakumbuka niliona siku moja Jiji la Mwanza wakisema watavunja nyumba 1000. Leo hata moja haijavunjwa! Watu wa NEMC walikuwa wanatafuta sifa kwa vile wanamjua rais anapenda bomoa bomoa? Au aliagiza mwenyewe?
 
Walikuwa wanaogopa kuwaudhi wapiga kura wa zanzibar, maadamu sasa wamepata ushindi wa kishindo cha tsunami wataanza tena kuvunja
 
Nyumba za kubomoa zimekwisha. Zingine hazipo ndani ya hifadhi ya barabara dude.
Waliojenda mabondeni wote wamejiondoa wenyewe, mfano jangwani, buguruni(kando ya mto msimbazi n.k)
Hakuna nyumba tena ndani ya hifadhi ya barabara.
Unazoziona sio nyumba hizo, mawenge yako tu mkuu.
 
Mtatetea sana ila sisi kazi yetu kuwakumbusha kimoja kimoja
 
Nyumba za mbondeni na ndani ya hifadhi ya barabara hazipo tena mkuu. Angalia Jangwani na buguruni (kando ya mto msimbazi) zote zimebomolewa. Unazoziona ni mawenge yako tu mkuu.
 
Mbona hujauliza kuhusu ile kesi ilofunguliwa kuzuia mchakato wa bomoa bomoa?? Na kama unaamini hakutakua na maisha bora katika serikali hii basi hamia hata Rwanda ambako wana maendeleo!! Unashindwa kuwaza kwamba hata Roma haikujengwa kwa siku moja!!!
 
Mtatetea sana ila sisi kazi yetu kuwakumbusha kimoja kimoja
Read between the line. Sorry lakini kwa kukupoteza. Serikali ya CCM ina makengeza.
Kama upo dar maeneo ya mbezi luis, kuna kighorofa karibu kabisa na stendi mpya ya Mbezi lkn haijawekwa X. Nyumba ya jirani yake iliyoko mbali kidogo na hiyo stand imewekwa X, kisa huyo mwenye kigorofa ni afisa upelelezi mstaafu.
 
Mbona hujauliza kuhusu ile kesi ilofunguliwa kuzuia mchakato wa bomoa bomoa?? Na kama unaamini hakutakua na maisha bora katika serikali hii basi hamia hata Rwanda ambako wana maendeleo!! Unashindwa kuwaza kwamba hata Roma haikujengwa kwa siku moja!!!
Kesi ilihusu sehemu moja ya bonde la Msimbazi. Kubali tu kwa wazee wa kukurupuka walishutuka
 
Binafsi ningemshauri mstahiki Meya wa Jiji apitie upya tathmini ya lile zoezi lilivyofanyika. Lengo sio kutafuta mchawi, hapana lengo liwe ni jinsi ya kuliboresha ili kuondoa kadhia ya wakazi wa mabondeni. Anaweza kuangalia jinsi ya kuwaondoa hawa wakazi wa mabondeni kiustaarabu na bila kusumbuana kwa kuangalia utu na sio kudhalilishana kama ilivyokuwa hapo awali.
Kama kuna eneo lenye kero kwa wakazi wa Dar ambalo litampa credit mojawapo ni hili la wakazi wa mabondeni. Tusilichukulie kama ni jambo la kisiasa, hili jambo liangalie jinsi ya kuokoa maisha ya wakazi wa mabondeni. Mvua zikinyesha ndugu zetu hawa wanataabika sana na mara nyingine hukubwa na vifo. Namuomba mstahiki Meya aangalie jinsi ya kulitatua hili jambo tusisubiri maafa kwa hawa ndugu zetu.
 
Maamuzi ya kukurupuka ndivyo yalivyo lakini kwa jinsi ninavomjua mkuu wa kaya mkiendelea kumchokoza ataifufua na atabomoa kwelikweli maana hapendi kuonekana alikosea.
 
Njoo uku mbezi beach nyumba ziliwekwa x ndo kwanza wenye nyumba wanapiga rang nyingne kuashilia kwamba hatuna wacwac na maisha yanaendelea swadacta
 
Njoo uku mbezi beach nyumba ziliwekwa x ndo kwanza wenye nyumba wanapiga rang nyingne kuashilia kwamba hatuna wacwac na maisha yanaendelea swadacta
Umenikumbusha mkwara eti watabomoa hotel zote za ufukweni zilizojengwa ndani ya mita 60. Nchi hii bwana!
 
Nyumba za kubomoa zimekwisha. Zingine hazipo ndani ya hifadhi ya barabara dude.
Waliojenda mabondeni wote wamejiondoa wenyewe, mfano jangwani, buguruni(kando ya mto msimbazi n.k)
Hakuna nyumba tena ndani ya hifadhi ya barabara.
Unazoziona sio nyumba hizo, mawenge yako tu mkuu.
Bomoa Bomoa, hazijaisha bado zipo nyumba nyingi zilizojengwa mabondeni, zilizotiwa X sehemu nyingi tu, ila sema wamejifahamu kuwa zoezi zima la bomoabomoa lilikua limefanywa kimakosa, huwezi wabomolea watu nyumba bila kuwapa kiwanja na muda kidogo, wajitayarishe kujenga japo vibanda katika maeneo yao mapya.

kinachoshangaza ni kwamba kama ni makosa na hatari kujenga mabondeni kwasababu ya mafuriko, pia ni hatari kwa moto nyumba nyingi za gorofa mjini, zilizojengwa bila kuacha chochoro pembeni kama sheria inavyotaka, badala yake kujengwa viduka au vioski vinavyotakiwa kuachwa wazi ili kuepusha moto kusambaa kwenda nyumba nyengine panapotokea ajali ya moto kuwaka, kutumika kama fire exit na pia kuwapa urahihisi wazima moto kufanya kazi yao panapo tokea moto katika hizo nyumba.

pia kuna nyumba nyingi za gorofa mjini zimejengwa chini ya viwango na pia hazina certificate ya kuthibitishwa na wahandisi wa serikali/manispaa kuwa zimemaliza ujenzi kwa mujibu wa ramani zilizowasishwa manispaa, na zipo salama kuweza kukaliwa au kufanywa biashara katika hayo majengo lakini yanafumbiwa macho, zikiachwa watu kuishi, kukodishwa kama makazi au kufanyiwa biashara bila kuguswa.

Kama wa wabondeni wamefanya makosa kujenga, inafaa na hawa wa mjini wenye magorofa wachunguzwe, kwani nao pia ujenzi wao unahatarisha maisha ya wananchi na mali zao, na ujenzi kama huu kuachwa kuendelea ni wazi mji wetu utajengwa nyumba ambazo ni hatari kwa makazi na biashara.
 
Back
Top Bottom