bomb neutralizers

bomb neutralizers

ymollel

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2012
Posts
3,095
Reaction score
2,294
naomba kueleweshwa kutoka kwa wale wataalamu wa mambo ya milipuko. kuna kitu kinaitwa bomb neutralizer ila sijui kama ni kifaa au nacho ni mlipuko. kifaa hiki kinatumiwa kulipua bomu kwa kulifuata kabla halijashuka ardhini. nimesikia hata israel wanavitumia kwa sasa.

SWALI LANGU:
1.je? hiki kitu kinafanyaje kazi.
2. je kinaweza kutumika zaidi ya mara moja au kikishatumia mara moja ndio basi?
3. je? ni kifaa cha electronic
4. je? kinaongozwa au kinauwezo wa kujiongoza chenyewe
5. je? kikitumwa angani na kama hakuna bomu kitarudi kizima iki kitumike tena au ndio mwisho wake.

asanteni wataalamu
 
ngoja waje.. na mimi pia ningependa kufahamu kutengeneza bomu la mkono, yani grenade. plz wakuu tupeni maujanja ya mabomu hapa
 
Utakuwa unaongelea anti-missile defence systems kama Iron Dome ya Israel au Patriot System ya Wamarekani iliyotumika Gulf war kutungua Scud za Sadam Hussein.
Haya ni makombora ambayo kazi yake ni kutungua makombora mengine, inatumia rada kugundua na kulitrack kombora la adui kisha inapima kombora hilo litakuwa wapi baada ya muda fulani kwa kuangalia spidi na trajectory ya hilo kombora, kisha inarusha kombora lake lenyewe ambalo kazi yake ni kwenda kulipuka mpele ya kombora la adui na hivyo kuliharibu. Kombora haliwezi kutumika zaidi ya mara moja na likikosa target yake linajilipua lenyewe kuondoa hatari ya kudondoka na kuleta uharibifu.
Cheki Iron Dome - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Check video ya how iron dom work hapa,ukitaka practical zaidi inabidi uende Israel hasa kipindi hiki ukajionee mwenyewe.Kumbuka hii ni technologia ya kijeshi so usitegemee kila details itapatikana kirahisi kama ingekuwa hivyo hata nchi zingine wangetengeneza.Fuatilia habari za mashariki ya kati utajua mengi.
 
Hizo teknolojia zinaweza kuwashusha wanaoruka na ungo?
 
Ni ngumu sana maana hawa jamaa hawaonekani kwenye rada.
Naamini ukiwa na radar iliyotengenezwa kwa technologia kama wanayotumia kuruka utawapata,hujawahi kushuhudia walionaswa na kuanguka kisa walipita kwenye anga la wenzao bila taarifa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom