Bomb Attack on Opposition Party Casts Shadow over Local Elections in Tanzania

Hii ni social forum ya kila mtu na kila kitu kila wakati. Kama mnakerwa nendeni Michuzi au FB
Mkuu, hakika kama kuna watu wanakereka basi nyie machadema ndo mnaongoza. Mpaka mnatoa majina ya ajabu na uzushi kibao. Tupambane kwa hoja maana nyie mkizidiwa mnakimbilia kutoa matusi tu. uwezo wenu wa kufikiri ni mdogo
 
Ahsante kwa kioja badala ya hoja
 
images
images
​
​
MATUKIO ya utekaji, kupiga na hata kuuawa kwa viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani, hususan CHADEMA, yamechukua sura mpya baada ya shirika moja la Kijerumani kutoa ripoti iliyoanika hadharani ukatili huo. Ripoti hiyo ambayo inadaiwa kusambazwa ndani na nje ya nchi, imeshutumu vikali matukio hiyo, huku ikisukuma lawama kwa vyombo vya dola kwa kushindwa kuchukua hatua madhubuti dhidi ya watu wanaodaiwa kuhusika na ukatili huo.

Shirika la Konrad Adenauer Stiftung la Ujerumani linalojihusisha na utafiti wa siasa nchini limetoa ripoti hiyo, huku likitahadharisha kuwepo kwa uwezekano mkubwa zaidi wa vitendo vya kikatili kwa viongozi wa vyama vya upinzani, wanaharakati na wakosoaji wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete kadiri chaguzi zinavyokaribia.

Ripoti hiyo iliyoandikwa na Danja Bergman na Stefan Reith, iliyotolewa tangu mwezi uliopita, inazungumzia matukio mbalimbali yaliyolikumba taifa la Tanzania kwa siku za karibuni, huku suala la bomu la Arusha lililolipuliwa katika mkutano wa CHADEMA likionekana kulitia doa taifa la Tanzania katika medani za kimataifa.
Hata hivyo, wachunguzi hao wana maoni kuwa ongezeko la matumizi ya mabavu kutoka kwa vyombo vya dola dhidi ya maandamano halali na ukosoaji, ni dalili tu ya mambo makubwa zaidi yanayoweza kutokea katika kipindi cha miaka miwili ijayo, wakati uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika.
Ripoti hiyo pia inasema, kwa kadiri ya hali ilivyo kila aina ya vitisho, udanganyifu na matumizi ya mabavu vitakuwa vikibadilishwa badilishwa na kutokea katika sura tofauti ikiwemo vurugu ili kupotosha umma, huku watuhumiwa wa vurugu hizo wakishindwa kutambuliwa, na wale wanaotambuliwa watafichwa au kutochukuliwa hatua zozote za kisheria na mamlaka husika.

Limeenda mbali zaidi na kusema kuwa hata pale vyombo vya dola vinapohusishwa na mauaji, kwa ushahidi wa wazi, watuhumiwa wamekuwa wakilindwa na kuendelea kutesa mitaani bila kuchukuliwa hatua zozote za kisheria, badala yake wahanga wa matukio hayo wamekuwa wakishitakiwa kwa kesi mbalimbali za kubambikiza, zikiwemo za uchochezi, ugaidi, na kuhamasisha chuki kati ya wananchi na serikali yao.

Katika uchaguzi mdogo uliofanyika nchini Juni 16 katika kata 22 na Julai 14 katika kata nne za Arusha, vurugu nyingi ziliripotiwa zikiwahusu wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuteka, kujeruhi na kupewa mafunzo ya kijeshi kwa ajili ya kusimamia shughuli za ulinzi katika chama hicho kikongwe nchini.

Wachunguzi wa masuala ya siasa wanaona matokeo ya uchaguzi uliofanyika hivi karibuni yanaonyesha kuwa Chama kikuu cha upinzani nchini (CHADEMA) kinapata ustawi wa kasi kubwa, hivyo kuwa tishio katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2014 na Uchaguzi Mkuu wa 2015, jambo ambalo linakiogopesha chama kinachotawala.
Ripoti hiyo inasema upinzani umefanikiwa kujiweka kama serikali mbadala inayoonekana katika chaguzi tangu 2010, hivyo kuna wasiwasi kuwa watawala watatumia kila walichonacho mikononi mwao kuzuia mabadiliko hayo yasitokee.
 
Wakawateke na hawa wajerumani basi ndio tujue kweli Ccm na Polisi mnaweza kuziba midomo ya Dunia..Wapuuzi kabisa Polisi wa Nchi hii mi ndio maana huwa nafurahi nikisikia polisi kamwagwa matumbo na majambazi au hata na maraila tu..mbwa kweli hii mijitu
 
Hii ni tasisi iliyompa slaa upadri wala haina chochote pumzisha akili yako tu acha kusumbuka.

Nchi za Afrika Mashariki zimeitenga Serikali ya CCM kwa sababu ina Udini na Ukabila,Nchi za Ulaya nazo zinaanza Kuamshwa na Taasisi zao kuhusu ukabila na UDINI unaopaliliwa na Viongozi wa CCM.Kweli CCM Majanga.
 
hawa CONRAD wanajua kila kitu. KWA taarifa hii ni wazi kuwa DR SLAA anaumbuka

Nambalapala;

Try to read anything between the lines before uttering your nonsense!

Yawezekana lugha ya Malkia kwako haipandi. Kwa taarifa yako tu kwenye habari hii Dr.Slaa hajatajwa popote. Sasa sijui kaingiaje hapa.

Kama ulikuwa unaogopa umande tafuta mtu anayejua kizungu akupe tafsiri sahihi ya habari hii. Briefly ni kwamba hii habari inaivua nguo serikali yako ya CCM kabsaaa. Milipuko yote ya Mabomu Arusha pale Olasiti kanisani na Soweto kwenye mkutano wa CHADEMA vidole vyote vitano vinaelekeza CCM,Polisi na Serikali yake. Sitaki kufafanua zaidi lakini ninachokushauri tafuta mtu akupe tafsiri sahihi ya habari hii,huo muda mie sina.

Lakini kwa watu makini(GT) madai ya Viongozi wa Chama Twawala CCM na Serikali baada ya mlipuko huo yamedhihirika kuwa ni ya UONGO ULIOPINDUKIA BAADA YA MATOKEO YA CHAGUZI NDOGO ZA UDIWANI KWENYE KATA 4 ZA ARUSHA MJINI!
CHADEMA hawajashinda kwa bahati mbaya au kuonewa huruma kama walivodai kina Lukuvi,Mwigulu,Nnape na wapuuzi wengine wa chama Tawala. Lile Bomu hata kama lisingepigwa hiyo tarehe 15/06/2013 bado ushindi ulikuwa ni wa CHADEMA tu! Kwa hiyo matokeo haya ya ushindi wa CHADEMA ni mrejesho wa Bomu la Soweto kwamba KUMBE CCM NDIYO WALIOPANGA KUVURUGA UCHAGUZI BAADA YA KUONA KWAMBA HAWAKUWA NA NAMNA YOYOTE YA KUSHINDA UCHAGUZI HUO!

Wasalaam.

Na bado tutaona Aljazira, CNN na SkY News karibuni...CCM wanadhani dunia haijui
 
MAGAMBA yanaanza kuwekwa uchi kwa ushenzi wao wanaowafanyia Wananchi wao bila ya kuwa na hatia yoyote
 
mkuu, si ipo ujerumani tu bali wana ofisi hapa Dar es salaam na ndo wafadhili wakubwa wa chadema. usitegemee kuwa wataandika taarifa za kuisafisha serikali na kuichafua chadema

hivi kuna sehemu hao jamaa wamesema uongo?
 
images
images
​
​
MATUKIO ya utekaji, kupiga na hata kuuawa kwa viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani, hususan CHADEMA, yamechukua sura mpya baada ya shirika moja la Kijerumani kutoa ripoti iliyoanika hadharani ukatili huo. Ripoti hiyo ambayo inadaiwa kusambazwa ndani na nje ya nchi, imeshutumu vikali matukio hiyo, huku ikisukuma lawama kwa vyombo vya dola kwa kushindwa kuchukua hatua madhubuti dhidi ya watu wanaodaiwa kuhusika na ukatili huo.

Shirika la Konrad Adenauer Stiftung la Ujerumani linalojihusisha na utafiti wa siasa nchini limetoa ripoti hiyo, huku likitahadharisha kuwepo kwa uwezekano mkubwa zaidi wa vitendo vya kikatili kwa viongozi wa vyama vya upinzani, wanaharakati na wakosoaji wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete kadiri chaguzi zinavyokaribia.

Ripoti hiyo iliyoandikwa na Danja Bergman na Stefan Reith, iliyotolewa tangu mwezi uliopita, inazungumzia matukio mbalimbali yaliyolikumba taifa la Tanzania kwa siku za karibuni, huku suala la bomu la Arusha lililolipuliwa katika mkutano wa CHADEMA likionekana kulitia doa taifa la Tanzania katika medani za kimataifa.
Hata hivyo, wachunguzi hao wana maoni kuwa ongezeko la matumizi ya mabavu kutoka kwa vyombo vya dola dhidi ya maandamano halali na ukosoaji, ni dalili tu ya mambo makubwa zaidi yanayoweza kutokea katika kipindi cha miaka miwili ijayo, wakati uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika.
Ripoti hiyo pia inasema, kwa kadiri ya hali ilivyo kila aina ya vitisho, udanganyifu na matumizi ya mabavu vitakuwa vikibadilishwa badilishwa na kutokea katika sura tofauti ikiwemo vurugu ili kupotosha umma, huku watuhumiwa wa vurugu hizo wakishindwa kutambuliwa, na wale wanaotambuliwa watafichwa au kutochukuliwa hatua zozote za kisheria na mamlaka husika.

Limeenda mbali zaidi na kusema kuwa hata pale vyombo vya dola vinapohusishwa na mauaji, kwa ushahidi wa wazi, watuhumiwa wamekuwa wakilindwa na kuendelea kutesa mitaani bila kuchukuliwa hatua zozote za kisheria, badala yake wahanga wa matukio hayo wamekuwa wakishitakiwa kwa kesi mbalimbali za kubambikiza, zikiwemo za uchochezi, ugaidi, na kuhamasisha chuki kati ya wananchi na serikali yao.

Katika uchaguzi mdogo uliofanyika nchini Juni 16 katika kata 22 na Julai 14 katika kata nne za Arusha, vurugu nyingi ziliripotiwa zikiwahusu wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuteka, kujeruhi na kupewa mafunzo ya kijeshi kwa ajili ya kusimamia shughuli za ulinzi katika chama hicho kikongwe nchini.

Wachunguzi wa masuala ya siasa wanaona matokeo ya uchaguzi uliofanyika hivi karibuni yanaonyesha kuwa Chama kikuu cha upinzani nchini (CHADEMA) kinapata ustawi wa kasi kubwa, hivyo kuwa tishio katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2014 na Uchaguzi Mkuu wa 2015, jambo ambalo linakiogopesha chama kinachotawala.
Ripoti hiyo inasema upinzani umefanikiwa kujiweka kama serikali mbadala inayoonekana katika chaguzi tangu 2010, hivyo kuna wasiwasi kuwa watawala watatumia kila walichonacho mikononi mwao kuzuia mabadiliko hayo yasitokee.
Matatizo yetu yameanzia mbali sana.
 
Back
Top Bottom