Bodi ya mkopo naona ipo serious

RGforever

JF-Expert Member
Apr 3, 2011
6,878
5,424
010334a0bb3c383d072dddb3b07c49e9.jpg


UPDATE

9a38029341bc3aecb13f06cb5dfc3739.jpg


Elimu ya Juu:
Edson Mwakyombe analia. Analia kwa uchungu na huzuni mkubwa. Analia kwa sababu ndoto zake zimekutana na kikwazo. Sisemi kwamba hazitatimia kwa sababu hatujui Mungu ana mipango gani nae.
Ila Mungu sio wa kuachiwa kila jambo. Mungu hatoi mikopo ya Elimu ya Juu. Ameshatupa serikali. Na ndio maana Raisi huwa anatusihi sana TUMUOMBEE. Je Edson Mwakyombe hajamuombea? Sidhani.
Katika maumivu na huzuni yake Edson Mwakyombe anaweza kujikuta akijiuliza 'yuko wapi Mungu wangu' au 'yuko wapi Raisi wangu'. Huko ndiko lilipo tegemeo lake.

Edson Mwakyombe analelewa na mama yake baada ya baba yake kufariki. Amefaulu kwa kupata Divisheni 1.8. Na kwa kuingalia picha hii Edson Mwakyombe hakai Masaki wala Mikocheni. Kwa wale mliosoma Jiographia somo la "kutafsiri picha" mtajua kwa nini.
Kinachoumiza Edson Mwakyombe hayuko peke yake. Wapo wengi wanatamani sana kupata elimu ya juu lakini hawana uwezo. Elimu ni msingi imara wa kila kitu. Maendeleo yetu yanategemea ELIMU kuliko BARABARA, NDEGE au VIWANDA.
Bila Elimu unapanda ndege kwenda wapi? Kufanya nini?

Bila Elimu utafanya kazi gani kiwandani? Utaajiriwa kama mfagizi tu?

Bila Elimu utasafiri kutoka kijijini kukimbilia mjini kutafuta ajira kwa kutumia barabara na ajira hutapata! Utaongeza idadi ya wasio na kazi mjini!! Binafsi sioni sababu ya kukejeli serikali kwa kutumia msemo 'tunaisoma namba' au kukumbusha ahadi kuhusu mikopo ya juu. Katika hili tusaidiane. Nini kifanyike?

Mwanzoni kabisa Raisi alielekeza fedha zinazookolewa kwa kubana matumizi zijenge barabara au matumizi mengine muhimu. Namuomba tubane matumizi sehemu yoyote ile Edson Mwakyombe na wenzake wapate elimu ya juu. Hata kama ni kufuta kikao kimoja cha bunge afute tu!!! It is that deep. Ikiwezekana afute kila aina ya posho mpaka fedha zipatikane vijana wetu waende chuoni!! Namuomba Raisi katika hili asikae kimya. Binafsi siwezi kumkumbuka kwa barabara, ndege au viwanda kama bado tutaendelea kuwa WAZALISHAJI wakubwa wa vijana wasio na elimu. Hapana. Tutakuwa kiwanda kikubwa Afrika cha kuzalisha UJINGA, WASIO NA AJIRA na MASIKINI
Naomba Raisi ukirudi kutoka Kenya useme neno lolote kuhusu hili. Na neno liwe kheri kwa Edson na wenzake-#albertomsando
 
Kinachonishangaza ni neno mwombaji kutumiwa wakati sisi si waombaji wapya je mkopo wa umefutwa ili neno mwombaji linapotumika
 
weka link tuione maana picha zinasambaa but link kila mtu hana au mmetengeneza nn ili kuwapa presha vijana maana walishaaanza kulia tayari
 
Back
Top Bottom