Bodi ya Mikopo pelekeni fedha vyuoni wahitimu wa 2015/2016 wapewe vyeti vyao

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,694
149,917
Kuna chuo/vyuo vimeamua kutokuwapa wahitimu wa mwaka wa masomo 2015/2016 vyeti vyao kutokana na Bodi ya Mikopo kutolipa ada za wanafunzi kwa wakati na hivyo kupelekea vyuo kuzuia vyeti vya wahitimu katika vyuo husika.

Serikali hii imeshindwa kuajiri hivyo ni bora basi ikalipa hata ada hizi ili vijana hawa wapate vyeti vyao wakajitafutia ajira wanakoweza.

Mambo kama haya na mengineyo bila shaka ndio yamemfanya Tambwe Hiza leo hii kupitia Star tv katika kipindi cha "tuongee asubuhi" aseme hii serikali inajali zaidi maendeleo ya vitu na si watu.

Badilikeni tumechoka.

Wapinzani tunaomba muhoji jambo hili nje ya Bunge na katika Bunge linalooanza mwezi huu mwishoni(tarehe 31/01/2017).
 
Kuna chuo/vyuo vimeamua kutokuwapa wahitimu wa mwaka wa masomo 2015/2016 vyeti vyao kutokana na Bodi ya Mikopo kutolipa ada za wanafunzi kwa wakati na hivyo kupelekea vyuo kuzuia vyeti vya wahitimu katika vyuo husika.

Serikali hii imeshindwa kuajiri hivyo ni bora basi ikalipa hata ada hizi ili vijana hawa wapate vyeti vyao wakajitafutia ajira wanakoweza.

Mambo kama haya na mengineyo bila shaka ndio yamemfanya Tambwe Hiza leo hii kupitia Star tv katika kipindi cha "tuongee asubuhi" aseme hii serikali inajali zaidi maendeleo ya vitu na si watu.

Badilikeni tumechoka.
Tambwe hizza ndio role model wako!ulitakiwa upigie debe pesa ziende kwanza kulipa posho na ada za wanafunzi unataka watu walipiwe cheti,waombe kazi kwa kutumia muhtasari wa matokeo inakubalika kamanda
 
Uko sahihi kabisa ususani vyuo vya private ata transcript wanagoma kutoa.
 
n
Tambwe hizza ndio role model wako!ulitakiwa upigie debe pesa ziende kwanza kulipa posho na ada za wanafunzi unataka watu walipiwe cheti,waombe kazi kwa kutumia muhtasari wa matokeo inakubalika kamanda
ndugu yangu baadhi ya maeneo wanakataa kutumia muhtasari wanataka waone matokeo halisi na jinsi ushindan ulivyo mkubwa hakuna aye hangaika na muhtasari wako
 
Habari zenu wana jamvi

Kumekuwa na sintofahamu kwa wahitimu wa chuo cha uhasibu dar es salaam ngazi ya shahada waliokuwa wakifadhiliwa na board ya mikopo,yapata mwezi na masiku kadhaa tangu chuo kiahidi kuwa kitatoa vyeti kwa wahitimu wenye sifa,cha kushangaza hali imekua tofauti kwa wahitimu waliokuwa wanalipiwa na board ya mikopo chuo kinasema hakitatoa vyeti wala transcript hadi watakapolipwa pesa za ada za wanufaika kutoka loan board,yawezekana mimi ndiye sina uelewa juu ya hili naomba wana jamvi nisaidieni Haya maswali;

01;Hivi yawezekana chuo(taasisi) haiiamini serikali yake ambayo iliingia mkataba wa kuwalipia ada wanafunzi wake?

02;Je,ni sahihi chuo kuzuia matokeo na vyeti kwa mwanafunzi ikiwa alishatimiza sehemu yake? Hapa naomba nitolee ufafanuzi kidogo kwa asilimia kubwa kwenye non-priority course huwa board ya mikopo haitoi asilimia mia hapa inategemea bahati ya mnufaika,kwa maana hyo kama board watakulipia 75% ya ada hzo 25% inabidi zilipwe na mwanafunzi mwenyewe na hapa tumeona chuo wanakua wachungu mwanafunzi haruhusiwi kufanya mitihani akiwa na hilo deni hiyo ndio sehemu ya mwanafunzi ambayo anatakiwa aitimize,sasa Leo iweje nihukumiwe mimi kwa kosa lisilo langu?

03;hakuna namna loan board na chuo wakawa na mawasiliano na makubaliano ili kuepusha haya matatizo kwa wanafunzi,inauma sana mtu umepata kibarua unaambiwa upeleke japo transcript lakini chuo kinakatalia na wanatoa majibu mabovu huku wakizunguka kwenye viti "kama kazi ni yako sisi tunachotaka ada yetu" jamani tumefikia huku? Hata mkuu wa chuo anadariki kusema hilo suala liko nje ya uwezo wake,,so sad napoteza kazi hivi hivi

Nawasilisha!
 
Kama ni kweli huo nao ni ujinga mwingine. Kila moja afanye wajibu wake Bodi nayo kama inadaiwa ikilipe chuo/au wakubaliane ili wahitimu wakaajiriwe waweza kulipa deni lao bodi
 
Yakheri ninyi mnaruhusiwa kufanya graduation. Vyuo vingine hawakubali hata ufanye mahafali.
Ref; SAUT na MWECAU.

Pili, hiyo njia tu ya kuishinikiza Serikali itoe pesa. La sivyo taasisi itaendelea kupigwa danadana mpaka ishindwe kujiendesha.

Cha tatu na swali la Msingi ambalo ungeuliza
"Ni kwa nini HESLB mpaka leo haijapeleka fedha za Wanafunzi waliomaliza?" Yaani wewe umalize na useme kuwa umemaliza lakini hela yako haijafika chuoni.
Hilo deni ni lako, siyo la HESLB. Loanboard ni sehemu yako tu katika kukufanikishia hilo. Ndo maana chuo wanawafundisha ninyi, siyo HESLB.
 
Hata mimi mdogo wangu alienda chukua matokeo UDOM kumbe bodi ya mikopo haikuwalipia tuition fee wakiwa mwaka wa kwanza ilibidi walipe wenyewe au urudi nyumbani.
Na ajabu wakianza kuwakata watawakata hata ela ambayo hawakulipiwa
 
Kama ni kweli huo nao ni ujinga mwingine. Kila moja afanye wajibu wake Bodi nayo kama inadaiwa ikilipe chuo/au wakubaliane ili wahitimu wakaajiriwe waweza kulipa deni lao bodi
Mkuu,huu ndio ukweli watu wananyimwa vyeti kwasababu Bodi haijapeleka vyeti.

Tatizo Wapinzani hawahoji na hata Waandishi wa habari nao wako kimya juu ya hili jambo.
 
Back
Top Bottom