Bodi ya Mikopo mna shida gani maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao?

Kayombo Tips

JF-Expert Member
Jun 19, 2020
574
490
Ni zaidi ya wiki tatu sasa natuma maombi ya mikopo kwenye bodi ya mikopo kwa njia ya mtandao. Lakini muda wote ninaotuma maombi hayo matatizo mawili yanajitokeza.

Tatizo la kwanza napata ujumbe huu "A User With Tha UserName Already Exists". Napata ujumbe huu baada ya kulipia gharama za maombi ya mkopo na kuendelea kutengeneza akaunti yangu. Tatizo hili lilikuwapo kwenye mfumo huo kwa zaidi ya wiki mbili.

Lakini baadae tatizo hilo likaondolewa na likaja tatizo la kiunganishi cha loan application kutokufunguka. Hili tatizo la kitufe cha kuanza kuomba mkopo limedumu kwa zaidi ya wiki nalo lakini leo nimejaribu tatizo la kiunganishi cha kuomba mkopo limeondolewa na limerudi tatizo la ""A User With Tha UserName Already Exists".

Matatizo haya mawili yanajitokeza kwa zaidi ya watu wanne waliokuja kuomba niwafanyie kazi ya kutuma maombi ya mkopo. Sasa najiuliza ina maana watu wote wanne wameshajiandikisha ilhali hawajawahi kujiandikisha?

Na kwanini tatizo la ""A User With Tha UserName Already Exists" linajitokeza baada ya kufanya malipo ya kuomba mkopo? Nadhani bodi ya mikopo watakuja kutoa maelezo kuhusiana na hili. Lakini inavyoonekana tatizo ni kiufundi zaidi. Yaani mfumo wa wao unashida ya kuchakata taarifa.

Sasa najiuliza inakuwaje mfumo muhimu kama huo wa kuomba mkopo unakuwa na shida ndogo kama hii na shida hiyo inadumu zaidi ya wiki mbili mpaka wiki tatu. Wataalamu wa software wanafanya kazi gani ikiwa mfumo muhimu kama huu unashindwa kufanya kazi kwa usahihi katika kipindi muhimu cha kutuma maombi ya mkopo?

Bodi ya mikopo kuna shida gani hapo na mnafanya kazi gani hapo ofisini ikiwa matatizo kama haya yanadumu kwa zaidi ya wiki mbili? Watu mnaowahudumia watapataje huduma kutoka kwenu kwa mwendo huu?

Nimewapigia simu zaidi ya mara 4 naona hampokei simu. Mnafanya kazi gani hapo?

IMG_20230920_153856_674.jpg
 
Back
Top Bottom