Bodi ya Mikopo inawaibia Watanzania

Jamaaan eeh mlipe tu na watoto wa wengine tusome miulize mm nasoma kozi ngumu bila boom ni shida tu wakati wenzangu wananunua nguo na simu za bei kwa boom tu wanamageto yao mimi nakaa hostel. Mlipe deni.
 
Kuna mambo yanatia hasira hii nchi basi tu.
 
Ukichukuwa deni la milioni 30, halafu kila mwaka ukawa unalipunguza kwa lakhi 4, maana yake ni kuwa utachukuwa tarikbani miaka 75 kulipa deni lote (30,000,000/400,000 = 75)! Na wakati huo utakuwa umetumia zaidi ya mil 100 kulipa milioni 30. Huu ni sawa na ujambazi ambao Bodi imehalalishwa kufanya. Ni ndoa ya kinyonyaji kabisa. Yaani ni sawa na kuapa kuwa utakufa na kuzikana na Bodi ya Mikopo!
Kwahiyo ukichukua mil 28 +1.6m=29.6 tofauti ya laki nne tu, sasa hapo unakuwa unalipa deni au una maktaimu?
 
NAOMBA MODS,WAUNGANISHE NYUZI ZOTE ZINAZOHUSIANA NA MALALAMIKO YA BODI YA MIKOPO KISHA WAUFANYE UWE STRICKLY.

HILI SUALA NI ZITO NA PANA MNO KWA MASLAHI YA VIJANA WANYONGE WALIOANZA KUPIGANA NA KUJIKWAMUA KIMAISHA

BINAFSI,HATA MIMI NI MHANGA MKUBWA TU WA HILI SUALA...NGOJA NIKAE VIZURI HALAFU NAMIMI NIELEZE VITUKO NILIVYOVIKUTA KWA HAWA JAMAA THEY SO CALLED HELSB

N.B. (DAWA YA DENI NI KULIPA TU,LAKINI SIO KWA HUU UTARATIBU KANDAMIZI ULIOPO SASA)
 
Mwaka kesho wanaondoka na hizi sheria zao mbovu. Mikopo ya nini ya kukandamiza watoto wa wengine, nao yafaa warejeshe zile pesa walizowasomeshewa. Very hopeless indeed.
 
Mkuu hizi habari za kusema utulie kwanza sjui ukae vizuri unazitoa wapi?? Huu uzi hauna cha kusubiri mwagika kila kitu hapa tunataka mambo yote yawekwe adharani kuhusu upupu wa hawa jamaa
 
Bodies imekuwa zaidi ya TRA inavyonyanyasa watu. Hivi MTU gani mwenyeakili timamu atajipeleka akakatwe kiasi cha kukomoana? Kuna watu has a walimu wamebakiwa na mshahara wa lakimoja kisa heslb. Wameshindwa kukata kidogo kidogo isiumize watu ili wajitokeze wengi au mpaka raisi ajisikie kuwaambia na kuwatumbua ndipo watagutuka?
Taasisi yoyote ya kitanzania chini ya serikali haipaswi kufanya maisha ya watu kuwa magumu
 
Nimeona kiji-barua toka bodi ya mikopo wakijaribu kujieleza nini maana ya sheria ya mikopo kwa wanafunzi. Kwa ujumla kama hayo ndo maelezo toka kwa wataalamu wa bodi hiyo basi, tuseme tu kwamba tuna watu wasio na uwezo ndani ya taasisi za serikali. Kama kuna makosa au ugumu wa utekelezaji wa sheria mpya, bodi hii ndo ilistahili kutoa mapendekezo ya jinsi ya kuboresha sheria lakini, maelezo yao ni kama umemuuliza mtoto wa kindergarten.

Sihitaji kuwasaidia jinsi ya kuangalia matatizo yao, nionacho ni wizi na ufisadi wao wa siku zote wanaojaribu kuziba pengo la wizi wao. Waligawa pesa vyuoni hata pasipo na wanafunzi. Wakalipia wanafunzi hewa kwa makusudi. Sasa wanawaibia wakopaji wa kweli. Taasisi hii inahitaji watu makini ktk mfumo wa elimu na jamii na siyo kuweka muhasibu tena akitoka kwenye NGO ndogo kabisa, eti awasidie wakopaji wa nchi hii.
 
CC Mk54
 
Hesabu unajua wewe?
Miaka 75 inatoka wapi? Iyo 75÷12= Miaka 6 na miezi 3
Kama maesabu yanakushinda usingechukua mkopo
 
Utakuwa ngwini wewe. Unadaiwa 30,000,000 na kila mwaka unatoa 400,000 tu. Hata wakikukata vipi, bado deni linasogea palepale.... Hesabu zako zingekuwa na maan kama ungelikuwa unalipa lakh 4 kila mwezi. Hapa ni Lakh 4 kila mwaka. Ngwini mkubwa wewe...
Hesabu unajua wewe?
Miaka 75 inatoka wapi? Iyo 75÷12= Miaka 6 na miezi 3
Kama maesabu yanakushinda usingechukua mkopo
 
Utakuwa ngwini wewe. Unadaiwa 30,000,000 na kila mwaka unatoa 400,000 tu. Hata wakikukata vipi, bado deni linasogea palepale.... Hesabu zako zingekuwa na maan kama ungelikuwa unalipa lakh 4 kila mwezi. Hapa ni Lakh 4 kila mwaka. Ngwini mkubwa wewe...
Hayo maesabu unajipangia wewe unapeleka laki 4. Kama unaenda kulipia Kodi ya nyumba. Ndio maaana wamewatageti watu wanaopata mshahara wanakata kwa asilimia. Na mikopo waliopata ni watu wa degree ambao mshahara wao unaanzia 750,000 na kuendelea na kama ni asilimia 15 wanakata kwa mshahara ujue ni 1,350,000/- kwa mwaka apo na ujue mshahara kila baada ya miaka 2 mshahara unapanda ivi vitu vinahesabika, sema watu wengi wanaingiza kwy mkopo Mambo ambayo ukuwa nayo wakati wa mkopo. Mfano umu vyuoni wakati unapata mkopo unajiingiza kwy matumizi yasiyoendana na mkopo uliosainiwa kama kusomesha wadogo zako, kwenda kutafutia mademu, kuolea na kuongea mpaka unamaliza chuo unajikuta una mke na watoto 2 unaanza kazi tayari una wategemezi kitu ambacho mkataba wa mkopo hautambui wategemezi hao, mkopo unakutambua wewe na mzazi aliyekuwa referees wako. Tujifunze kuishi kwa bajeti sio kulalamika tuuuu.
 
Hi Hivi rais wa wanyonge anasomaga uzi mzuri kama huu,bodi ya mikopo ni kirusi kinachowatafunna watoto wa maskin,na mbaya zaid hali si shwali kwa waliosoma sayansi,ukiangalia salary slip zao utasikitika,utakuta mtu anadaiwa mpaka milion 30,ikute una penalty hadi milion 40,na makato hayako fixed.
 
Bodi ya mikopo ni majizi kama sio jipu jingine tanzania, wameanza kukata wafanyakazi wenye diploma wakati sio wanufaika wa bodi hiyo.
 
Kusomesha chuo kikuu bure utakua unaota
 
Mkuu wewe ndo mburula sasa ona umepata aibu ya hovyo hesabu ndogo kama hiyo imekushinda,,,

Siku nyingine kabla hujatoa povu tafakari "When you are dead you don't know you are dead,it is only painful for others.The same applies when your stupid"
Hesabu unajua wewe?
Miaka 75 inatoka wapi? Iyo 75÷12= Miaka 6 na miezi 3
Kama maesabu yanakushinda usingechukua mkopo
 
Kuna kampuni niliwahi kufanya kazi,wakawa wananikata huo mkopo lakini walikuwa hawapeleki huko bodi for almost two years. Nimekuja kwenda kuangalia balance,duuh nimekuta deni limepanda from 4mil to 10 mil.nimebaki sijui naanzia wap ila risit zangu zote(salary slips) kwa muda huo wote niliokatwa ninazo.kibaya hiyo kampuni ni kama imekufa,hivyo sina wa kumfuata.Lakini najiuliza,kama bodi ilimpa mandatory hiyo kampuni inikate na iwapelekee na hawakupeleka japo wamenikata,ni nani anapaswa kuwajibika?kwa nini waendelee kunidai Mimi?
 
Natamani rais aitishe mkutano Wa wanachuo watoe dukuduku lao kama walivyofanya wafanyabiashara
Imagine mwanafunzi kabaliza karudi mtaa, na bodi inadai interest kila mwaka na huyu mtu hana kazi. Bodi haioni kama inamtwisha mzigo asioweza kuubeba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…