Bodi ya Mikopo inawaibia Watanzania

Bodi ya Mikopo inawaibia Watanzania

Tabutupu

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2010
Posts
13,262
Reaction score
18,702
Uwepo wa bodi ya mikopo ni dalili tosha kwamba tumedhamiria kuwakandamiza watoto wa maskini kwa nguvu zote.

Pili bodi ya mikopo nafanya kazi kwa kubahatisha sana kiasi cha kuwavambikia hawa maskini madeni ambayo hata siyo yao kwa sababu wanajua kwa umaskini wao hawataweza kwenda mahakamani.

Tatu wafanyakazi wa bodi ya mikopo ni moja ya watumishi wenye lugha za hovyo sana utadhani tumewalazimisha ajira.

Ni bora tungekua tunakopa kwenye banks kuliko huu ujanja ujanja wa serikali wakagi pesa ni zetu .. sisi ndio tunaolipa kodi.

Mapendekezo
1. Serikali iangalie upya swala la marejesho isizidi 5%

2. Retention fee isizidi 1%

3. Bodi ya mikopo ijipange .. Isiumize wachache ambao wamejitolea kulipa kufikia malengo ya 80% ambao bodi imeshindwa kuwafikia.

4. Ili kuboresha urudishaji wa madeni basi kila anayeomba sharti awe na kitambulisjo cha taifa .

Tunatengeneza taifa maskini kwa mikono yetu.

Kuna nchi nyingi sana zinasomesha vyuo vikuu bure.. kwanini isiwe Tanzania.
 
Bodi ya mkopo inabambikiza madeni, unaenda kuomba kulipa deni wanaanza kukuta kwa miezi mitatu hivi wanaacha, hafu baada ya mienzi mitatu wanaanza upya kula kuconsider marejesho ambayo ni tayari
 
Bodi ya mikopo inakaba sana. Kumbuka waokopa bodi ni watoto wa maskini. Bodi imesababisha elimu ya juu kubinafsishwa kwa walio inunua. Hivyo kupunguza uzalendo. Inauma sana kukatwa asilimia 15 tena kutoka kwenye vimshara viduchu vya serikalini.
Uzalendo nchini bado sana kama watoto wa nchi wanalazimishwa kujisomesha badala ya serikali kwa kisingizio cha mikopo

Landson
 
ukishawalipa deni lao wao wanaendelea kukata tu ,ukifanikiwa kustopisha makato ,tabu inakuja kwenye ishu ya kurudishiwa makato yaliyozidi . Utasikia andika barua after 3months malipo yatakuwa tayari lkn wapiii? Ni zaidi miezi 8 sasa watu hawajalipwa madeni yao yanayotokana Na makato yaliyozidi.

Sijui walalamike wapiii
 
Bodi ya mikopo inakaba sana. Kumbuka waokopa bodi ni watoto wa maskini. Bodi imesababisha elimu ya juu kubinafsishwa kwa walio inunua. Hivyo kupunguza uzalendo. Inauma sana kukatwa asilimia 15 tena kutoka kwenye vimshara viduchu vya serikalini.
Uzalendo nchini bado sana kama watoto wa nchi wanalazimishwa kujisomesha badala ya serikali kwa kisingizio cha mikopo

Landson
Huku ikiwa ulichukua mkopo kwa makubaliano ya Aslimia 10℅
 
. Kwako *Dr.John Pombe Magufuli*

Bodi ya Mikopo imewanufaisha watanzania wengi sana ikiwa ni pamoja na kuwajengea watanzania misingi ya kielimu kwa ajili ya future katika maisha yao . Aidha, Asilimia 80 ya wanufaika wa mikopo ya bodi ni wale kina KAYUMBA Yaani watoto wa maskini.
Sheria ya mwaka 2016 ya bodi ya mikopo iliyofanyiwa marekebisho ni sheria *ANGAMIZI* kwa watoto maskini.
*Sheria imeweka wazi ( Watz wengi hawana tabia ya kujisomea) kuwa marejesho ya mkopo yatakuwa ni kwa 15%, na deni hilo litakuwa linaongezeka kila mwaka wa fedha kwa asilimia 6% ya deni halisi la mwanzo.*
Kwa mfano.
*Daktari ambae amesomeshwa na bodi, asilimia kubwa deni lao huwa kati ya mil 25 mpaka 30.*
Basic salary yake ni 1.5 Mil
Makato ya mshahara wake ni kama ifuatavyo
Helsb 225, 000 TSH
PAYE 295,090 TSH
NHIF 42,420 TSH
Pension. 80, 000
Total deduction 642, 510 TSH
take home yake ni 857,590 TSH —ana watoto na anasomesha!
-----------------------------
Kwa sheria ya bodi ya mikopo, huyu bwana kwa mwaka ataweza kulipa 2.7Mil ( 225,000X12)
Hivyo katika deni lake la 30Mil , atakuwa amepunguza deni lake hadi 27, 300,000TSH ikifika mwisho wa mwaka wa fedha.
Mtu huyu atapaswa kuanza mwaka wa fedha mpya akiwa na deni la 27, 300, 000 TSH.
Lakini sheria ya bodi inasema hapana, unatakiwa kuongezewa 6% ya 30 mil ambayo ni 1.8 Mil
Hivyo deni analopaswa kuanza nalo ni 27,300,000+ 1.8 Mil sawa na 29, 100, 000 TSH.
Kwa mwaka unaofuata tena, atafanikiwa kuipunguza hiyo 29,100,000 Mil hadi 26,400,000 Mil na ndiyo ni kianzio cha deni lake kwa mwaka mpya uliofuata.
Sheria ya bodi itasema hapana, hii 26,400,000 lazima iwekwe 6% ya 30Mil ambaye ni 1.8
Hivyo 26,400,000+ 1.8 mil
Deni jipya kwa mwaka mpya uliofuata itakuwa ni 28,200,000Mil badala ya 26,400,000 and the list goes on.
Yaani utakuwa unakwenda mbele na kurudi nyuma mpaka unastaafu.
Sheria ya mwaka 2016, inazidi kusema kuwa, ikiwa muhusika mpaka anastaafu, hajafanikiwa kumaliza deni lake, basi pension yake itafidiwa.
Yaani, Ikiwa una pension ya 15 Mil , na deni lako lilibaki 20 Mil , Bodi itakula zote 15 Mil na itakudai 5 Mil na hiyo 5 mil itazidi kuongezeka kadiri miaka inavyokwenda mbele, ni hatari sana na mbaya zaidi watumishi wengi hawajui hii sheria.
Ikitokea pension yako imeliwa yote na bodi,maana yake unazeeka ukiwa huna kitu.
I just can't figure it out , ni sheria kandamizi dhidi ya mtoto maskini iliyopitishwa na wabunge wetu tukufu.
Ni kwamba mtoto wa maskini hatoweza kumaliza hili deni , ni deni la maisha hasa waliosoma makozi ya sayansi kama udaktari, Nesi, famasi , na injinia na wale waliosoma nje ya nchi.hawa wote madeni yao si chini ya 25Mil or so. It is a detrimental to these poor people, and Unfair.
Mapendekezo
1. Serikali ipitie upya hii sheria, na ifutilie mbali hiyo incremental ya 6% kwa kila mwaka, it is not even practical, watu wengi wanakufa na hayo madeni tena bado yakiwa makubwa mno.
2. Irudishwe asilimia 8% au 10% badala ya 15% ya makato ya bodi, kwa sababu watumishi wa umma ndiyo wanufaika na hii mikopo, na wengi wanaangamia hali zao malikiti sokoni.
3. Bodi ya Mikopo itoe elimu maredioni juu ya utaratibu wa urejeshwaji wa haya makato WaTZ wengi haijui kitu kuhusu mambo ya sheria.
4. Sheria ya kuchukua pension ya watumishi walioitumikia serikali hadi kustaafu itolewe kwa Sababu ni mateso makubwa yatakuwa kwa hawa watu na hii ni jamii yetu inayoitumikia serikali ya Jamhuri miaka nenda rudi.
Watumishi wa umma wengi wanastaafu wakiwa maskini na fukara, uwachukulie tena hizo pesa za pension, kweli ? Doh tutapata laana katika nchi.
USHAURI.
1. Kwa wazazi ambao wanajiweza, achaneni na mambo ya kuwasukumizia watoto wenu kwenye mikopo mpaka muelewe vyema sheria ya marekebisho, hiki ni kilema cha maisha kwa wale ambao deni lao ni above 20Mil.
2. Pia wahusika hakikisheni mnaipitia hii sheria na muelewe marejesho yake, you need to take precaution. Kama huelewi mtafute Mwanasheria akuelewesheni ni hatari sana fuatilieni haya mambo.
Rais JPM tunaomba ufanyie kazi hayo mapendekezo kwa heshima na taadhima .

*Wako Raia Mwema.*
 
Post hii imekaa vizuri sana, tafadhali mods tuiweke kama sticky thread
Cc. Zitto
Moderator
@invicible
pascal mayalla
 
Kwa nguvu ya mtandao naomba tusaidiane kupaza sauti juu ya udhalimu na unyanyasaji wa kupindukia kwa watu maskini unaofanywa na bodi ya mikopo juu ya wanufaika wa mikopo hiyo.
 
Matunda ya serikali sikivu ya awamu yatano hayo .Toka link ccm wakawa na nia zuri na hii nchi wao ni kupiga noti ,ufisadi ,kujinufaisha wao na familia zao tu ,hawazijui shida za watanzania hata moja .
Hapa nitatofautiana na wewe. Ni vizuri kujikita kwenye hoja husika. Eleza shida iko wapi? Kisha toa mapendekezo yako ya nini kifanyike ili kutatua changamoto ulizobainisha. Binafsi nianze kutoa hoja kwa kuanza pia kukinzana na kichwa cha mjadala. Naomba kisomeke "Tunaomba Serikali Imulike Upya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu" Baada ya kusomeka hivyo basi niungane na mchangiaji ndugu "Elitwege" hapo juu kuwa kile alichokieleza ni ukweli tosha kuwa ndiyo rangi halisi tunayoifahamu wengi wetu.Jambo moja lenye kutia faraja ni kuwa wengi wetu tuna Imani kubwa sana na serikali ya awamu ya tano katika utendaji wa kazi yake. Hii ni akisi dhamira halisi aliyokuwa nayo Baba wa Taifa mwl. Julius K. Nyerere. Hivyo basi, kutokana na Imani hiyo tunaiomba serikali ifuatilie maoni haya ya wanufaikaji. Hongera Rais wetu, hongera sana.
 
Bodi ya mikopo wanapaswa kuweka kuweka link/utaratibu kwenye mtandao kuonyesha mtiririko au mwenendo wa ulipaji mikopo kwa kila mdaiwa, yaani ionyeshe kiwango anachodaiwa, malipo anayofanya kila hatua na kiasi kilichobaki. Tofauti na utaratibu wa sasa, ambapo ukitaka kujua kiasi kilichobaki kama deni au umelipa kiasi gani ni hadi uende ofisi za bodi za kanda.

Pia utaratibu huu utatusaidia hata sie tulioko sekta binafsi kupata uhakika kama mwajiri anawasilisha kweli makato yote anayotukata kila mwezi?
 
Awali swala la mikopo lilikuja ili kuridhisha IMF wakati wa program ya mageuzi ambayo wenye lugha yao waliita structural Adjustment Program (SAP). Wakati huo Tanzania ilikubali kwa shingo upande ikichelea kukoseshwa misaada. Tulokuwa vyuoni wakati hule tukapatiwa boom na ule mpango wa vyuo vikuu kulisha wanafunzi ukasitishwa na wanafunzi wakawa wananunua wenyewe vyakula. Hii kwa kiasi iliathiri wanafunzi wakati hule. Nitalingumzia baadae hili. Ghafla Serikali ikaona kumbe kuna kauchumi katika hili na ikaanza kuwataka wafaidika wa mikopo kuanza kulipa. Ikumbukwe kuwa wakati hule wanafunzu hawakuingia mkataba na Serikali bali walipewa tu fedha hizo. Kuna watu walikuwa wanadaiwa si zaidi ya shilingi laki tano za Kitanzania, Utamu wa kiuchumi na huenda ikawa shauku ya kuhakikisha watoto wengi wanasoma, Serikali ikarekebisha sheria mwaka 2016. Ni bahati mbaya sheria ile imekuwa mwiba kwa watoto wa Watanzania wengine. Huenda pia matatizo haya ya madeni kuongezeka sana yakawa yanasababishwa na watendaji wasio waaminifu wa bodi ya mikopo. Ni wakati sasa kwa serikali kuipitia upya sheria ile na kufanya marekebisho. Aidha, ni wakati wa bodi yenyewe kuwachunguza kwa karibu watendaji wake ambao miongoni mwao huenda wakawa sio waaminifu. Mkurugenzi wa sasa wa Bodi huenda naye alikuwa ni miongoni mwa waliopata mikopo ile ya awali ambayo madeni yalikuwa sio zaidi ya laki tano. Ikitokea kuwa hivyo ataona umuhimu wa haya tunayoyazungumza.
 
Niungane na Ntinje kukuomba Tabutupu kubadili kichwa cha thread kiwe bodi ya mikopo elimu ya juu imulikwe upya, pia nimewaomba mods waifanye iwe sticky thread
 
Ukimaliza mkopo kwenye salary slip yako Ukienda kuulizia utaambiwa una 3M
Value of Money.

Nimebakisha kana laki4 nimalize
 
Back
Top Bottom