Bodi ya Mikopo(HESLB) waachia majina ya wadaiwa sugu kuanzia mwaka 1994 hadi 2014

Mr.Junior

JF-Expert Member
Sep 8, 2013
11,773
9,967
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inatangaza orodha ya majina ya Wadaiwa Sugu ambao wamehitimu katika Vyuo mbalimbali vya Elimu ya Juu kuanzia mwaka wa masomo 1994/1995.

Wasugu hao wanapewa siku 30 kulipa madeni yao ndani ya muda huo kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa na wahusika kulazimika kulipia gharama za kuwasaka na kuendesha kesi.

Chanzo: Tovuti ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu..

Habari hii imetumika kwenye Kipindi cha JamiiLeo kinachorushwa kila siku jioni katika Channel ya JamiiForums kwenye mtandao wa YouTube.

Kuona kipindi hicho angalia video ifuatayo, acha maoni yako na kisha Subscribe kwenye Channel ya JamiiForums.

Attachments

  • ORODHA_YA_WASUGU_1.pdf
    9.5 MB · Views: 2,019
  • ORODHA_YA_WASUGU_2.pdf
    9.6 MB · Views: 1,986
  • ORODHA_YA_WASUGU_3.pdf
    9.6 MB · Views: 1,680
  • ORODHA_YA_WASUGU_4.pdf
    9.6 MB · Views: 1,787
  • ORODHA_YA_WASUGU_5.pdf
    9.4 MB · Views: 1,838
Kuna waliofariki dunia, kuna wasio na ajira na kuna ambao kwa sababu zisizojulikana hawajawahi kukatwa hayo madeni na pia ikumbukwe kuwa kuna hewa humo humo.

Kuweka list bila kujua uzima wa wadaiwa pia kujua wangapi wana ajira ni ukosefu wa mawazo ya kujiongeza haswa kwenye suala nyeti kama hili. Hiyo siyo bodi yenye maarifa.
 
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inatangaza orodha ya majina ya Wadaiwa Sugu ambao wamehitimu katika Vyuo mbalimbali vya Elimu ya Juu kuanzia mwaka wa masomo 1994/1995.

Wasugu hao wanapewa siku 30 kulipa madeni yao ndani ya muda huo kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa na wahusika kulazimika kulipia gharama za kuwasaka na kuendesha kesi.

Chanzo: Tovuti ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu..

ngoja tujionee
 
maajabu haya utayaona Tanzania pekee...
mtu alishindwa kulipa ada ya chuo, akamaliza, hajaajiliwa, kamaliza hajakaa hata miaka miwili eti ni mdaiwa sugu!!
kamaliza 2013/2014 anakuaje sugu, huo usugu maana yake ni nini sasa??
haa haa kwel noma sana...
 
Back
Top Bottom