Bodi ya mikopo ya elimu ya juu (Higher Education Students' Loans Board) Tanzania ilianzishwa mwaka 2005 na Rais wa tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayati Dkt.Benjamini William Mkapa chini ya Wizara ya elimu yenye jukumu la kutoa mikopo Kwa wanafunzi wa elimu ya juu kuanzia shahada ya kwanza Kwa vigezo maalumu vilivyowekwa ,Mkopo inatolewa katika sehemu ya malipo ya ada, kujikimu, mafunzo Kwa vitendo, viandikwa na taaluma maalumu.
Chanzo ;(Bodi ya Mikopo)
Njia za kuimarisha utawala bora katika bodi ya mikopo.
Kutoa mkopo Kwa kuzingatia vigezo walivyoviweka. Bodi ina vigezo maalum ili Mwanafunzi apate mkopo mfano kiwango cha ufaulu,Uhitaji wa mkopo(Yatima, TASAF,Ulemavu ).Vigezo hivi mda mwingine havifwati bali kunakuwa na udanganyifu unaopelekea upendeleo Kwa baadhi ya wanafunzi wasio na vigezo hii ni kutokana na ukilitimba unaofanywa na baadhi ya watumishi wasio waaminifu.Hivyo teknolojia itumike katika uchakataji wa upataji wa mikopo.
Uwepo wa ofisi zote Mahali pamoja zinazohusika na Mikopo.Taasisi kama RITA, Mahakama,Posta,NIDA.Hii itasaidia kuokoa muda na ukamilishwaji wa nyaraka Kwa ufanisi Kwa waombaji. Mfano kuongeza ofisi katika wilaya zote tofauti na sasa ambapo zipo katika ngazi ya mkoa tu.Hii itaongeza uwajibikaji na ufanisi na kupelekea utawala bora.
Kuondoa vipaumbele vya Utoaji wa mikopo katika baadhi ya taaluma. Bodi iondoe kigezo hichi cha kutoa kipaumbele Cha mkopo kwa wanafunzi Waliosoma masomo ya Sayansi tu mfano udaktari, uhandisi,mfano katika"SAMIA SCHOLARSHIPS" ilivyofanya bali ifikirie na masomo ya sanaa mfano,habari,ualimu wa sanaa,utawala,utalii, tafsiri na ukalimami,kwa sababu wengi waliokosa mkopo ni masikini.Hii italeta usawa Kwa wote.
"SAMIA SCHOLARSHIP" ya Mwaka 2022/2023 iboreshwe mwaka huu wa masomo 2023/2024. Miongoni mwa vigezo ni kutoa ufadhili Kwa tahasusi za Sayansi tu, Kama vile (PCB, PCM, PGM, CBG, PMC's) Kwa wavulana wenye daraja la kwanza alama 3-5 na wasichana alama 3-6 ambapo waliopata hizo alama hizo mwaka 2022 matokeo ya kidato Cha Sita ni wanafunzi toka shule za watu binafsi wenye uwezo wa kumudu gharama za chuo na mkopo kwao sio kipaumbele. wachache Sana ni Toka shule za serikali.Hivyo basi serikali ione wajibu na Kwa tahasusi za sanaa waliofanya vizuri ili kuleta usawa Kwa wote.
Chanzo:Wizara ya elimu,Sayansi na teknolojia
Kutoa Fedha za mafunzo Kwa vitendo Kwa wanafunzi wote.Baadhi ya taaluma taaluma wanapata fedha za mafunzo kwa vitendo na wengine kuachwa wakati mwaka wa kwanza wa masomo wanahitajika kwenda kufanya mafunzo Kwa vitndeo mfano wa taaluma ni shahada ya sanaa katika elimu. Hivyo hupata ugumu wakati ukifika wa kwenda kufanya mafunzo Kwa vitendo katika shule za msingi na Sekondari hivyo bodi iwajibike Kwa hilo.
Kuimarisha mifumo ya TEHEMA na Kanzi data.Ili kuongeza ufanisi na ubora katika Utoaji wa mikopo mfano Kanzi data iunganishe Mifumo ya Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) na la Ufundi, Tume ya Vyuo vikuu Tanzania(T.C.U),Posta, RITA, NIDA ili iokoe muda wa umalizikaji wa nyaraka Kwa Kipindi kifupi,Pia Mifumo mda mwingi imekua inasumbua Kwa kutikisika hivyo taarifa kuvurugika, mfano wanufaika wa mikopo kutokupata fedha Kwa wakati , kupata fedha zaidi au pungufu ya kiwango alichopangiwa.Hii itasaidia kupunguza upotevu wa Kwa bodi fedha wakati wa kutoa mikopo.
Kutoa elimu Kwa wanafunzi na Jamii .Elimu inatakiwa itolewe Kwa wanafunzi Kipindi wakiwa shuleni (Kwa kidato Cha Sita) na vyuo vya kati kabla hawajamaliza ili kuandaa mapema mahitaji na nyaraka kabla ya dirisha la mikopo kufunguliwa, mfano cheti cha kuzaliwa, vifo ,namba ya nida,barua ya udhamini wa masomo,uthibitisho wa daktari kutokana na ulemavu,gharama za ada kwenda bodi,muhuri wa wakili,steshenari hii itasaidia kujiandaa mapema tofauti na sasa ambapo elimu inatolewa kidogo mfano katika makambi ya J.K.T Kipindi cha wahitimu wa kidato cha Sita na ualimu wakiwa makambini Kwa mujibu wa Sheria ambapo si wote wanahudhuria .Hii ikifanyika italeta uwajibikaji na Kuongezeka kwa utawala bora.
Kiujumla haya yakifanyika Kwa weredi wa hali ya juu basi itafanya bodi ya mikopo kuwa na uwezo wa kutoa mikopo Kwa wanafunzi Kwa usawa,haki na kuondoa sintofahamu katika jamii.Pia italeta chachu ya wanafunzi kusoma na kuondoa mzigo Kwa wazazi au walezi juu ya gharama na hivo kuongeza kiwango cha elimu na wataalamu wenye tija katika jamii ya Tanzania.