Benjamini Netanyahu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2014
- 102,675
- 126,912
Kazi kwao
Habari zilizonifikia ni kuwa Menejimenti ya Shirika la Ndege ATCL imevunjwa ili kukidhi vigezo na haja za Shirika hilo na malengo yaliyowekwa kwa miezi 8.
Imeamuliwa Wakurugenzi Wote na baadhi ya Mameneja waondolewe mara moja (Isipokuwa Mtendaji Mkuu aliyeajiriwa hivi karibuni) hatua hiyo imechukuliwa kwa sababu mbalimbali ikiwemo utendaji dhaifu, viwango hafifu vya elimu kinyume na matakwa ya nafasi hizo na uadilifu.
Aidha wakurugenzi na Mameneja waliokuwa wakikaimu nafasi mbalimbali imeamriwa warudishwe kwenye ngazi zao za chini.
Bodi imemuagiza Mtendaji Mkuu atangaze nafasi za Wakurugenzi, Mameneja na nafasi nyingine atakazoona zinafaa kutafutiwa wafanyakazi wapya.
=======
UPDATE
Hata hivyo hatua zaidi zitachukuliwa kwa mawakala wa kukatisha tiketi kwakuwa utaratibu uliokuwepo hakuangalia maslahi ya shirika na ikithibitika hakuna ulazima wa kuwatumia mawakala basi kutakuwa na zoezi la kubatilisha mikataba ya mawakala na kuwatumia wafanyakazi wa Shirika.
Mwenyekiti wa bodi ATCL amedai shirika lilikuwa linakopa sana zamani na sasa wachofanya ni kulipa madeni ya zamani
Wamesema wamepunguza sana matumizi yasiyo ya lazima na wana mpango wa kuongeza safari za ndani za Kilimanjaro na Mtwara, pia wamefanikiwa kuongeza mapato ya ndani yatokanayo na mizigo iliyozidi
Pia wanadhibiti utolewaji wa tiketi za bure unaotolewa kwa wafanyakazi wa shirika ambao unaonekana kutumiwa vibaya na wafanyakazi
sasa walioondolewa ni chadema? akili zote umeacha lumumba umebaki mtupu tuChadema watanyooka tu, Safari hii, kila kona kibano
Sana....kuna jamaa alikuwaga meya smbdy londa....alikuwa kitengo cha Fedha jamaa kapiga hela sanaaaa kipindi hichoShirika limeliwa hili !
Mimi nafikir sio elimu watu wamechoka serikali wali isusa shirika na tusifikirie shirika la ndege linataka madigrii hapana sita.iosa.icao ni elimu ambayo inajitegemea kwenye airlines sasa kwa tz itakuwa ngumu ndo maana airlines kama Qatar air. Emirates Na hao rwanda air kuna wageni wahindi wazungu Na kila mwenye ujuzi ili kuensesha shirika sisi watz tuna usiasa ndani so kufanikiwa ni kugumu sana bil qualified staff Na sisi tz hatuna watu hao waliokuwepo ni watu wazima mfano engineering mtu wa chini ana miaka 60 watu waliosoma airlines education wachache leo tz ukitaka manager airline quality uwezi kumpata nje ya hao wazee sasa wacheni siasa tafuteni watu wa maana tuanze biashara!!!!
Usiseme safari sema Kirikuuudah nimeona chupa ya safari lager hapo pembeni.
Muda wa kazi umeisha...dah nimeona chupa ya safari lager hapo pembeni.
eeh vinaitwa kirikuu............nilikuwa sijui.Usiseme safari sema Kirikuuu
Ndio hivyoooeeh vinaitwa kirikuu............nilikuwa sijui.