Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,770
- 1,173
Bodaboda ni Nguzo Muhimu ya Uchumi, Si Chombo cha Maandamano
Katika jamii yetu ya sasa, waendesha bodaboda wamekuwa mhimili mkubwa wa usafirishaji, ajira, na ustawi wa kiuchumi kwa mamilioni ya Watanzania. Wakiwa na mchango mkubwa katika kutoa huduma ya usafiri mijini na vijijini, sekta hii imepunguza ukosefu wa ajira kwa vijana, kuongeza pato la mtu mmoja mmoja na kuchangia uchumi wa taifa. Serikali ya Awamu ya Sita imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha bodaboda wanatambuliwa, wanasaidiwa kwa mafunzo, mikopo, na mifumo rasmi ya usimamizi ili kuwafanya kuwa sehemu ya mfumo rasmi wa maendeleo.
Hata hivyo, ni jambo la kusikitisha kuona baadhi ya viongozi wa kisiasa kutoka chama cha Chadema, akiwemo Godbless Lema na John Heche, wakijaribu kuwahusisha waendesha bodaboda na ajenda za maandamano na vurugu. Kauli ya Heche inayodaiwa kuwahimiza bodaboda kushinikiza mahakama kuhusu kesi ya Tundu Lissu ni mfano wa wazi wa matumizi mabaya ya vijana kwa maslahi binafsi ya kisiasa. Aidha, kauli ya Lema inayowadharau bodaboda kuwa kazi yao ni "ajira ya laana" ni dhihirisho la dharau na chuki dhidi ya juhudi za vijana wanaojitafutia riziki halali kwa njia ya heshima.
Ni wazi kuwa kauli hizi ni za kichochezi, hazilengi ustawi wa taifa bali ni mbinu za kuzua taharuki na kupotosha jamii. Mahakama ni taasisi huru ambayo haipaswi kushinikizwa kwa maandamano au presha ya mtaani. Juhudi yoyote ya kuchochea fujo wakati wa mwenendo wa kesi ni uvunjifu wa sheria na ni jambo linalopaswa kulaaniwa kwa nguvu zote.
Tunatoa wito kwa bodaboda kote nchini kuendelea kufanya kazi zao kwa amani na kujiepusha na siasa chafu zinazotaka kuwafanya kuwa vyombo vya machafuko. Serikali inawatambua, inawathamini, na itaendelea kuwaunga mkono kwa sera na mipango thabiti ya kuwaendeleza.