Bodaboda ni kifo

Bodaboda ni kifo

Ewe mama/ baba unaempakia mwanao au wanao wawili kwenye boda boda kupelekwa shule acha ufala ,upumbavu na uvivu. Boda boda ni kifo!

Ewe mdada wa chuo unaeupenda urembo wako na uzuri wako ,boda boda ni kifo.

Ewe boda boda tafuta kazi ya nyingine kufanya achana na huo upumbavu wa boda boda!
Kifo ni popote hata kama unauza maembe na matikiti unaweza pigwa na radi wakati wa mvua ukafa!! Sio hiyo tu hata kama upo bank kikazi jengo linaweza kuporomoka ukafa hapohapo, haijarishi ni kazi gani, kifo kipo pale pale labda jambo la msingi ni kusisitiza umakini wa dreva na ufahamu juu ya kazi yake, lakini suala la kifo ni popote tu. Kinawafanya boda boda kupata ajali kupelekea kifo ni umakini, wapo careless sana wawapo barabarani na wengine unakuta keshapuliza afu anaendesha chombo cha moto nayo ni changamoto. Wengine akakimbia speed kubwa kwa kutaka sifa yaani ni vitu vya ajabu sana.
 
Kifo ni popote hata kama unauza maembe na matikiti unaweza pigwa na radi wakati wa mvua ukafa!!Sio hiyo tu hata kama upo bank kikazi jengo linaweza kuporomoka ukafa hapohapo,haijarishi ni kazi gani,kifo kipo pale pale labda jambo la msingi ni kusisitiza umakini wa dreva na ufahamu juu ya kazi yake,lkn suala la kifo ni popote tu.Kinawafanya boda boda kupata ajali kupelekea kifo ni umakini,wapo careless sana wawapo barabarani na wengine unakuta keshapuliza afu anaendesha chombo cha moto nayo ni changamoto.Wengine akakimbia speed kubwa kwa kutaka sifa yaani ni vitu vya ajabu sana.
Unajua nini kuhusu risk
Unajua nini kuhusu takwimu
 
Abiria pia unayonafasi kubwa tu ya kumuelewesha Dereva kua over speed ni hatari,sio wakati anakimbiza unachekelea tu ila ikitokea ajali ndio unamlaumu.
 
Ewe mama/ baba unaempakia mwanao au wanao wawili kwenye boda boda kupelekwa shule acha ufala, upumbavu na uvivu. Boda boda ni kifo!

Ewe mdada wa chuo unaependa urembo wako na uzuri wako, boda boda ni kifo.

Ewe boda boda tafuta kazi ya nyingine ya kufanya achana na huo upumbavu wa boda boda!
Umesema maneno ya ukweli kabisa,hata sijui tufanye nini ndugu,marafiki,na watu wetu wa karibu,na wasio wa karibu yetu,watusikie,wasitumie usafiri huu.
 
Elimu zaidi inahitajika kutolewa kwa hao bodaboda maana imeajiri wengi na watu wanalea familia zao kupitia bodaboda wakiaacha watafanya shughuli gani? Au warudi kuwa wezi?
Mbona kilimo kinalipa sana,wende kwenye kilimo.Ukilima mahindi,pilipili,nyanya,Bamia,bogaboga.Biashara za kuuza nyanya,mbogamboga,malimau,machungwa,mananasi,maembe nk,inalipa vizuri tu,huku una shamba,umepanda mazao mbalimbali.
 
Watu hawa usipande boda zao...

Wanyoa vduku..

Wale wa singeli sauti adi mwisho Kwenye bodaboda..

Bodaboda kavaa kibukta au kisuruali kimebana mkimbie kabisa..

Wale wavaa vindala (mikanda miwili)...

Hao watu huwa hawajali usalama wao wala hawajipendi kabsa...kamwe hawawezi kujali usalama wa abiria wake.
 
Ata apo ulipo upo na kifo, hata usipo panda utakufa tu, ngoja niendelee kugonga gia
 
Acha kuharibia biashara za vijana wanaojiajiri. Ajali husababishwa na kutozingatia sheria na alama za barabarani. Waache vijana wajiajiri
Kuna kundi kalitaja hapo hilo kundi la watoto namuunga mkono, huwezi ukampakiza mtoto kwenye boda boda its too risk, labda kama unachukulia poa ila ni hatari, zuio ni bora zaidi ya kutibu
 
Juzi nilikua nawahisha mzigo flani uende mkoani, kutokoea k.koo,
Kuulizia Konda akaniambia ndio tunatoka ubungo, ikabidi nichukue boda niiwahi Basi mwenge,
Sipendagi kuharakisha hawa watu ila sikua na jinsi wakati anaufunga ule mzigo nikamwambi Uharakishe tuna mda mfupi sanaa gari inapita,

Sijapata ona aisee, Ile boda ilipigwa mguu, Tunafika Junction pale mwenge hata hakuangalia, ye kaona Gap pale kati kavuka,
Tulipishana na Semi Ubavu kwa ubavu,
Ninaposema hivi namaanisha Shati langu lilichafuliwa kabisa na bodi ya ile semi, na mzigo ukapigwa push kdg.

Mimi niliamini tayari, maana yenyewe ilikua inakata kona na sisi tunanyooka, kufuata zile tairi 6 za nyuma, kushtuka tushavuka, Na basi hio hapo, konda ndio akafungua mzigo kwenye boda mana jamaa naye kapata wenge kakaa kwenye kadaraja ka mbao Kwenye mtaro kainama kashika kichwa,

Ana zinduka tuu ananiuliza
"Tunarudi k.koo"?
Nikamwambia Baba rudi tu mwenyewe.
 
Back
Top Bottom