Bodaboda ni kifo

Bodaboda ni kifo

Juzi nilikua nawahisha mzigo flani uende mkoani, kutokoea k.koo,
Kuulizia Konda akaniambia ndio tunatoka ubungo, ikabidi nichukue boda niiwahi Basi mwenge,
Sipendagi kuharakisha hawa watu ila sikua na jinsi wakati anaufunga ule mzigo nikamwambi Uharakishe tuna mda mfupi sanaa gari inapita,

Sijapata ona aisee, Ile boda ilipigwa mguu, Tunafika Junction pale mwenge hata hakuangalia, ye kaona Gap pale kati kavuka,
Tulipishana na Semi Ubavu kwa ubavu,
Ninaposema hivi namaanisha Shati langu lilichafuliwa kabisa na bodi ya ile semi, na mzigo ukapigwa push kdg.

Mimi niliamini tayari, maana yenyewe ilikua inakata kona na sisi tunanyooka, kufuata zile tairi 6 za nyuma, kushtuka tushavuka, Na basi hio hapo, konda ndio akafungua mzigo kwenye boda mana jamaa naye kapata wenge kakaa kwenye kadaraja ka mbao Kwenye mtaro kainama kashika kichwa,

Ana zinduka tuu ananiuliza
"Tunarudi k.koo"?
Nikamwambia Baba rudi tu mwenyewe.
Dah pole sana, abiria pia tunachangia kama mdau hapa unasema akimbie lazima akukimbize, ila naonaga ni kama hawa vijana hawamejitoa ufahamu, unawezaje kukatisha kwenye eneo hatari hivyo bila kuangalia pembeni yako
 
Kabla hajakatisha danger everything looks shwaaaari. Ndiyo maana unaambiwa: Stop!
 
Elimu zaidi inahitajika kutolewa kwa hao bodaboda maana imeajiri wengi na watu wanalea familia zao kupitia bodaboda wakiaacha watafanya shughuli gani? Au warudi kuwa wezi?
Ukiwa na familia inabidi uwe makini zaidi ili baada ya kazi urudi kwako ukiwa na chochote vivyo hivyo kwa ajili ya abiria wako.
Lkn boda boda wanavyoendesha na kuenenda barabarani utadhani wote hawana familia na hawajali maisha yao, ya wateja wao au hata ya watumiaji wengine wa barabara. Wanaendesha km watu ambao wanatamani kifo kiwapate au watu ambao hawajali km kifo kitatokea au haiktatokea.
 
Aiseee! Got it
 
Dah pole sana, abiria pia tunachangia kama mdau hapa unasema akimbie lazima akukimbize, ila naonaga ni kama hawa vijana hawamejitoa ufahamu, unawezaje kukatisha kwenye eneo hatari hivyo bila kuangalia pembeni yako
Kitu wanachojidanganya ni
Uzoefu, akili za kijinga sana kuleta mazoea na chombo cha moto, mimi nilikua sipandi Boda ila kuna mda nalazimika..

Nishapoteza rafiki zangu 3 kwa ajali za boda,
 
Acha kuharibia biashara za vijana wanaojiajiri. Ajali husababishwa na kutozingatia sheria na alama za barabarani. Waache vijana wajiajiri
Ni sawa kabisa Mkuu. Lakini! Daaa!! Hizo mbio bwana ni balaa! Kama ulivyosema, asilimia 99 ya waendesha bodaboda ni vijana. Tatizo si sheria za barabarani, ni "ujana"
 
Ewe mama/ baba unaempakia mwanao au wanao wawili kwenye boda boda kupelekwa shule acha ufala, upumbavu na uvivu. Boda boda ni kifo!

Ewe mdada wa chuo unaependa urembo wako na uzuri wako, boda boda ni kifo.

Ewe boda boda tafuta kazi ya nyingine ya kufanya achana na huo upumbavu wa boda boda!

Kumekucha
 
Mbona kilimo kinalipa sana,wende kwenye kilimo.Ukilima mahindi,pilipili,nyanya,Bamia,bogaboga.Biashara za kuuza nyanya,mbogamboga,malimau,machungwa,mananasi,maembe nk,inalipa vizuri tu,huku una shamba,umepanda mazao mbalimbali.
Uchumu lazima ugawanyike mjomba kama ni hivyo shughuli nyingine zifungwe pia wote tukalime.
 
Ukiwa na familia inabidi uwe makini zaidi ili baada ya kazi urudi kwako ukiwa na chochote vivyo hivyo kwa ajili ya abiria wako.
Lkn boda boda wanavyoendesha na kuenenda barabarani utadhani wote hawana familia na hawajali maisha yao, ya wateja wao au hata ya watumiaji wengine wa barabara. Wanaendesha km watu ambao wanatamani kifo kiwapate au watu ambao hawajali km kifo kitatokea au haiktatokea.
Wapo boda boda ninawafahamu hawana historia ya ajali tangu waanze kazi zao.
 
Kama bodaboda wa Arusha walivyo na masifa ya kijinga kuna wakati nikipishana nao nasema bora wafe tu. Yani anavunja sheria alafu anakutukana
 
Back
Top Bottom