Mr.Junior
JF-Expert Member
- Sep 8, 2013
- 12,984
- 11,794
Hapo ndio hawa wenetu wananiacha hoi kabisa.Bodaboda anaamini honi ndio breki
Hapo ndio hawa wenetu wananiacha hoi kabisa.Bodaboda anaamini honi ndio breki
Ni hatari kwa Taifa. Mimi ninadhani pikipiki zipandishiwe ushuru mara nne ili ziwe ghali kama bajaji au zaidi ili kupunguza madhara kwa jamii.Hawa watoto wengi wao bangi haziwapendi kabisa. Mtaa ninaoishi wanasumbua mpaka basi. Yaani muda wote ni kelele, na kupita kwa mwendo kasi!!
Na wanakufa kweli kutokana na huu ujinga wao!! Lakini hata hawajali.
Kiukweli kuna bodaboda wachache sana wenye akili timamu.
Tatizo na serikali yenyewe ndiyo inapata unafuu kwa kiasi fulani. Maana hawa watoto wasingekuwa na shughuli za kufanya, wengi wao wangekuwa ni vibaka na wezi mtaani.Ni hatari kwa Taifa. Mimi ninadhani pikipiki zipandishiwe ushuru mara nne ili ziwe ghali kama bajaji au zaidi ili kupunguza madhara kwa jamii.
Kabla ya Mchina kumwaga pikipiki nchini Mjapani ndiye alikuwa anaongoza kwa kuuza Yamaha kwa bei sawa na gari ndogo na kipindi hicho usafiri wa pikipiki uliheshimika kama wa gari.
Tatizo na serikali yenyewe ndiyo inapata unafuu kwa kiasi fulani. Maana hawa watoto wasingekuwa na shughuli za kufanya, wengi wao wangekuwa ni vibaka na wezi mtaani.
Mimi nashauri wangepewa semina za mara kwa mara ili wajitambue. Maana wengi wao wakishapata tu hesabu yao ya siku; basi kinachofuatia kuanzia hapo ni kuchezea tu mafuta, kunywa pombe na kuvuta bangi.
Ni bodaboda wachache sana ndiyo wana malengo. The rest ni vurugu tu mtaani.
Unajua maana ya kishandu?
Na hata akipona hawez kuwa sawa maisha yake yoteMara nyingi si rahisi kupona
Mr Devil 😂Kuna mmoja kagonga mtoto juzi kwa speed za kipumbavu kwenye barabara ya vumbi ni mbovu lakini ana pita speed, tume piga makofi hadi akawa mwekundu nazani ali hadithia wenzake.
Na wana penda kupita njia za waenda kwa mguu wana acha lami. Hawa sha sema nki mfuma ana nipigia honi kwa nyuma ni makofi tu ..pale ubungo Riverside sha piga makofi mmoja ali nipigia honi kidogo moyo uchomoke
Unayeamini waganga wanaweza kukupakua usiku na mimi nayejua 100% hakuna watu kama hao hapa duniani ni nani mjinga?Wewe mwenyewe hujui kwamba kamati ya waganga wanakupakua kila usiku
Pia taa ya nyuma wanatoa wanaweka kidogo.
Usukani wanaupindisha unakua kama koleo la kung'olea meno.
Bure kabisa!



HahaKuna mmoja kagonga mtoto juzi kwa speed za kipumbavu kwenye barabara ya vumbi ni mbovu lakini ana pita speed, tume piga makofi hadi akawa mwekundu nazani ali hadithia wenzake.
Na wana penda kupita njia za waenda kwa mguu wana acha lami. Hawa sha sema nki mfuma ana nipigia honi kwa nyuma ni makofi tu ..pale ubungo Riverside sha piga makofi mmoja ali nipigia honi kidogo moyo uchomoke
Kwaiyo wewe huna usamaria wema uongo? Uliona kupakia huo mzoga kwenye hicho ki rahum chako kwamba kingeisha mafuta au unakuja kueleza unoko hapa,hata picha hujaweka....
Tatizo la bodaboda kule kupatia mara moja wanafikiri mara zote wataendelea kupatiaLeo kwa mara ya kwanza nimeshuhudia mtu anakata roho.
Ajali ya bodaboda na gari ndogo imetokea maeneo ya Kange kituoni mkoani Tanga majira ya saa tisa alasiri.
Bodaboda ame-overtake upande wa kushoto wakati gari ndogo ilikua inakunja kutoka barabara kuu kuelekea barabara ya vumbi huku dereva wa gari dogo akiwa amechukua tahadhari zote ikiwemo kuwasha indicator.
Bodaboda katoka na speed zote upande wa kushoto bila kujua kuna gari tayari inakunja kona mbele yake. Kijana akalivaa gari ubavuni upande wa mbele, akatupwa mbali na boda yake na kutua mzimamzima pembezoni mwa barabara.
Kwakua niilikua nyuma ya gari hilo dogo wakati ajali inatokea eneo, nilisogea mbele na kupaki pembeni kisha nikashuka kwenda kumtazama muhanga wa ajali ile. Damu zilikua zinamtoka kwa nyingi sana puani, mdomoni na masikioni.
Alikua katika mwendo wa kasi mno (takribani 80-100km/her) na mbaya zaidi hakua na helmet kichwani.
Shukrani zimuendee msamalia mwema mwenye gari zenye namba T*** EBN ambaye alijitolea kumkimbiza hospitali. Lakini kwa hali ilivyokua ni wazi kijana alikua amekwishakata roho.
Chondechonde vijana wa Bodaboda kuweni makini tafadhali.
Sie tunamfahamu huyo mwamba kwa post za majigambo na spika alizonazo,hawezi kukusaidia asijitangaze/asikutangazeUnajuaje labda huyo msamaria mwema ni yeye ila hakupenda kujianika utambulisho wake?
Umeona kaficha namba ya gari?