Bodaboda mnawahi wapi?

Bodaboda mnawahi wapi?

Inna Lillah wainna ilaih rajioun, ila ile sehemu ya kuingia na kutoka Kange tahadhari muhimu sana
 
Bila shaka gari ilikuwa inatokea Tanga Mjini na ilikunja kuelekea njia ya vumbi iendayo Kange Kasera na boda alikuwa ananyoosha kwenda Kange Stendi, Kituo Kikuu cha Mabasi, Tanga.

Hawa vijana wa bodaboda walishashindikana. Pikipiki mpya washaondoa side mirrors na kutoboa exhost ili ipige kelele.

Vijana wameshindikana nchi nzima hakuna wa kuwagusa.

Kwenye taa nyekundu wanapita, hawakai foleni.

Boda boda ni laana
Wanaita kona ya jeshini. Vijana wa boda wanaisha pale.
 
Kuna mmoja kagonga mtoto juzi kwa speed za kipumbavu kwenye barabara ya vumbi ni mbovu lakini ana pita speed, tume piga makofi hadi akawa mwekundu nazani ali hadithia wenzake.

Na wana penda kupita njia za waenda kwa mguu wana acha lami. Hawa sha sema nki mfuma ana nipigia honi kwa nyuma ni makofi tu ..pale ubungo Riverside sha piga makofi mmoja ali nipigia honi kidogo moyo uchomoke
 
Leo leo tena asubuhi. Maeneo ya Jet karibu na vingunguti Dar es salaam. Boda boda imepata ajali na abiria alikuwa mdada amefariki

Hii nimeisikia, nasikia bodaboda tairi ya daladala imempita kichwani. Maskini mdada wa watu sijui alikuwa anatoka sokoni.
 
Kizimkazi
Screenshot_20240112-215827.jpg
 
Juzi kuna wawili walikuwa wanafukuzana wakaanguka wakaumia , boss kapata taarifa kachukua mali yake.
Wana ujinga ujinga mwingi sana.
 
Mungu wa mbinguni namwomba aniepushie mm hii kazi na uzao wangu wote
 
Boda boda Wana shida kubwa...na shida yao ni ya malezi. Hawana uvumilivu/ustahmilivu.

Hawana mpango binafsi na mpango wa pamoja. Kila mtu kugombania ndiko kunakowafabya wawe na haraka zisizokuwa na maana. Bodaboda hana mpango maalumu, yaani hajui ili siku yake iwe successful anatakiwa abebe abiria wangapi ni kama tumbo lisiloshiba kila akiona chakula lazima ale.

Na shida ya tatu no inherent kwa watanzania wote na namna tulivyokuzwa kama umma wa taifa hili. Kwenye bongo zetu nyuma kabisa Kuna namna tunaamini uhai wetu ni expendable. Na hii inatokana na kuondolewa utu wetu wakati wa ukoloni nadhani.

Mtanzania kufa sio issue saaana..ndio maana ukitoka care ya routine inayoonekana ...kutoka kwa watu na viongozi... huwa hakuna genuine care Mtanzania anapokufa. Na sisi tunapelekana hivyo hivyo. Kufa in pursuit for money sio issue we kufa tuu ni kawaida. Ni kitu kibaya sana.

Tusizoee vifo. Ni mbaya sana..
 
Leo kwa mara ya kwanza nimeshuhudia mtu anakata roho.

Ajali ya bodaboda na gari ndogo imetokea maeneo ya Kange kituoni mkoani Tanga majira ya saa tisa alasiri.

Bodaboda ame-overtake upande wa kushoto wakati gari ndogo ilikua inakunja kutoka barabara kuu kuelekea barabara ya vumbi huku dereva wa gari dogo akiwa amechukua tahadhari zote ikiwemo kuwasha indicator.

Bodaboda katoka na speed zote upande wa kushoto bila kujua kuna gari tayari inakunja kona mbele yake. Kijana akalivaa gari ubavuni upande wa mbele, akatupwa mbali na boda yake na kutua mzimamzima pembezoni mwa barabara.

Kwakua niilikua nyuma ya gari hilo dogo wakati ajali inatokea eneo, nilisogea mbele na kupaki pembeni kisha nikashuka kwenda kumtazama muhanga wa ajali ile. Damu zilikua zinamtoka kwa nyingi sana puani, mdomoni na masikioni.

Alikua katika mwendo wa kasi mno (takribani 80-100km/her) na mbaya zaidi hakua na helmet kichwani.

Shukrani zimuendee msamalia mwema mwenye gari zenye namba T*** EBN ambaye alijitolea kumkimbiza hospitali. Lakini kwa hali ilivyokua ni wazi kijana alikua amekwishakata roho.

Chondechonde vijana wa Bodaboda kuweni makini tafadhali.
Wakati umefika wa kudhibiti idadi ya boda boda. Mitaa imefurika pamoja na fujo
Hata moja kati yao havai helmet naa polisi wanaona kweupe
 
Back
Top Bottom