Tatizo kubwa ni ufahamu sahihi wa matumizi ya barabara. Tukitegemea wafuate elimu ya matumizi ya barabara kwa njia za kawaida (formal); tutaendelea kuwapoteza na kupoteza nguvu kazi na ustawi wa jamii kwa ujumla wake.
Napendekeza serikali iunde team ya kuwapatia elimu ya matumizi sahihi ya barabara; iwapitie vijiweni kwao, iwe karibu na viongozi wao wa vijiweni kwa kuwaelimisha wao ili nao wakawaelimishe wanachama wao(wapya na wazamani), kuwe na toolbox talk( kukumbushana usalama) angalau kila siku. Viifaa vyao vya usalama (helmet) zisitozwe kodi ili vipatikane kwa urahisi zaidi na kwa bei nafuu, wakipata elimu watatumia tu.
Police waondoe uadui nao kwani boda wengi ukimbia police (tigo) bila kuzingatia usalama wao.
Bodaboda ni, wadogo zetu, watoto zetu, majirani zetu,rafiki zetu, binadamu wenzetu etc, tunawahitaji kwa ustawi wa jamii, wanahitaji msaada, wasaidiwe