Bodaboda hawana Haki

Ajali ni ajali tu mkuu tho sometimes bodaboda wanajisabibishi vifo wenyewe kizembe...... sjui ni bangi au nini??
 
Mwendokasi vituo vipo karibu karibu sama,pia barabarq zetu zebra kila mahari,ndio maana watu wanagongwa
 
Sio DIT kabisa ni nyuma kidogo pale kwenye mataa ambapo kuna barabara ya kwenda Lumumba kama sijakosea.. Muda mwingine madereva wa mwendokasi wanadharau mataa.

Kama ni hapo basi kweli bodaboda kwa asilimia 99 ndiye aliyejimiksi....

Huwa wanagongwa sana kwenye hayo mataa hasa wale wanaotoka Morogoro Road kukatiza kuelekea Lumumba Road...

Maderava wa pikipiki huwa hawana subira na wengi ni weupe sana wa sheria za barabarani...
 
Mi kinachonipa hasira ni madereva wa magari wanapowapigia honi waendesha pikipiki wapishwe ili wapite. Wakati hivyo vyombo vyote vina hadhi sawa barabarani.

Gari na pikipiki havina hadhi sawa barabarani tafadhali mkuu, ingawa vyote ni vyombo vya moto...

Kisheria mtu wa pikipiki anapaswa aendeshe upande wa kushoto wa barabara na sio katikati au kulia mwa barabara...

Kuna sheria ya mwendokai pia, "dereva azingatie ukomo wa mwendo (speed limit) na wakati wote asizidi mwendo wa kilometa hamsini kwa saa (50kph)"...

Sasa katika haya mawili, kwa nini usipigiwe honi na gari ambalo kwa kawaida speed limit kwenye maeneo huru ni 80kph?
 
Boda wanavunja sana Sheria ! Na wanakera sana. Wameshazuiwa kutumia Barabara za Mwendo kasi muda tu awasikii! Uwezi risk maisha ya watu zaidi ya 100 waliopo kwenye bus kwa ajili ya mpumbavu mmoja- unakula kichwa tu hii ndo dawa- ajali ya jana ni miongoni mwa makumi ya ajali za Boda na Bus za mwendo kasi. Inatakiwa bodas wapewe mafunzo ya Driving na pia ije kuwa boda akipata ajali ya kutokana na uzembe afutiwe leseni milele hapo ndo watakuja kuwa na adabu
 
Kwamba Mwendokasi dereva alikuwa kalewa?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Mwache huyo anaongea, binafsi npo napambania afya hapa wiki ya pili siendi kazini kisa kichaa Moja alikua anaendesha gari Kwa speed kubwa na hayupo site yake kubalance mambo ikabidi aforce kupenya akaniparamia
Mkuu pole sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…