kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,263
- 17,560
Anachofanyiwa Bobi Wine sio Uganda tu. Vitendo vya viongozi wa kiafrika Kwa wananchi wao kinawatia hamu na kuwapatia sababu wakoni wetu kurudi tena Afrika. Wamegundua kuwa waliondoka kimakosa kabla ya wakati. Waliondoka bila kutengeneza viongozi wanaojuwa thamani ya mwananchi mmoja mmoja, umma, na taifa.
Leo hii kama wakoloni wakirudi kulichukua tena bara hili hawatapata taabu kama ile waliyoipata kwa vizazi vile vya akina Mkwawa, Rumanyika, Mirambo, Isike, Bin Batuta, Bunyoro na Baganga. Kutokana na ukatili, hila, unyanyasaji, wizi wa mali za umma na ufisadi wananchi wengi wanaweza kuwa tayari kuungana na majeshi ya wakoloni katika harakati za kulichukua tena bara hili linalotawaliwa na viongozi wanaotaka kubaki madarakani Kwa nguvu na kutesa waafrika wenzao kwa sababu za kijinga kabisa.