Bobi Wine: Katiba Mpya pekee si suluhisho

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
7,217
12,914
Wakati hoja ya Katiba Mpya ikitawala mijadala na hotuba za viongozi mbalimbali katika Baraza Kuu la CHADEMA, mwanasiasa wa upinzani kutoka nchini Uganda ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye baraza hilo amesema katiba mpya pekee haiwezi kuwa mwarobaini wa matatizo.

Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine ambaye ni kiongozi wa chama cha National Unity Platform amesema ni wazo zuri kuwa na katiba mpya, lakini isichukuliwe kama ndio itamaliza matatizo yote kwenye nchi husika.

Uganda tuna katiba nzuri sana, naweza kusema moja ya katiba bora zaidi duniani licha ya kuwa Jenerali [Rais YowerilMuseveni amebadili katiba mara nyingi sana. Katiba yetuhaiheshimiwi, sheria nchini Uganda ni nzuri tu kama ilivyokwenye karatasi ilimoandikwa" ameeleza.

Akitoa mbadala wa hayo amesema kuwa ni lazima kuwajengea uwezo wananchi waweze kuisimamia katiba ambayowanakusudia kuwa nayo.

Ametoa wito kwa CHADEMA kuwashawishi vijana zaidi kushiriki kwenye shughuli za kisiasa kwani Afrika ni bara changa, na hivyo hatma ya Afrika ipo mikononi mwao, kwa wao kujua ni wapi wanakusudia kwenda.

************†**********†************†*****************†
Dkt Slaa alituambia tusije tukawaaminishi wananchi kuwa Katiba Mpya ndiyo kila kitu.

400.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
FACT: Hakuna aliyesema kuwa katiba mpya ndiyo kila kitu! FACT: Katiba mpya ni msingi bora wa kujenga mfumo na uongozi bora. FACT: Katiba mpya inahitajika ili kuwa na viongozi na mfumo bora.

Tukishakuwa na viongozi na mfumo mzuri basi inabidi tutumie nguvu zetu kuboresha mambo mengine ya kujiletea maendeleo. Je, wewe unapojenga nyumba huwa unasema msingi bora ndiyo kila kitu?

Bila shaka msingí ukiwa bora unakuwa hujafanya kila kitu bali unakuwa umebakiwa na kazi kubwa ya kujenga nyumba! Msingi unakuwa umekuwezesha kujenga nyumba imara na nzuri! Upotoshaji hautawasaidia! Tatizo kubwa wengi wenu ni ma-clowns na problem moja kubwa ya ma-clowns ni kuto-realize their limitations!
 
Ni nini kitakachosababisha Katiba Mpya isiheshimiwe endapo itapatikana?

Kwa mtazamo wangu, Katiba Mpya haitaheshimiwa kama bado patakuwepo na mabaki ya utawala kandamizi kwenye vyombo vya kutunga sheria, na kuzisimamia.

Nitolee mfano wa hapa kwetu, Katiba Mpya inaweza isiheshimiwe endapo bungeni wabunge wengi wakiendelea kuwa wa CCM, hawa wataendelea kumlinda mwenyekiti wao ambaye ndie Rais hata kama akivunja sheria.

Au mahakamani; majaji na mahakimu wengi wataendelea kumheshimu/ogopa aliyewateua hata kama atakuwa anavunja sheria.
 
Hotuba ya Mgeni Rasmi imebeba mawazo ya hekma ya Freeman bin Aikael bin Mbowe

Kamanda Freeman Mbowe namfananisha na Nyerere kwa uwezo wake wa kisiasa

anashauri watu wasibeze hoja ya ACT kuhusu Tume huru ya Uchaguzi kwa kusema mambo haya yanapaswa kwenda pamoja

ukisikiliza Hotuba ya Kamanda Mbowe na Hotuba ya Mgeni rasmi unagundua Freeman ameanza kutambua Siasa za kina Lema na Lissu za uanaharakati zitakimaliza haraka sana

amekitaja kabisa ACT kwa jina na akiwakemea Viongozi wanaoshinda mitandaoni kukitukana

ametaka tuache tabia ya kuamini kila anaewaza tofauti na mawazo ya Chadema ni mtu mbaya

Hongera sana Kamanda

Hongera sana Wazalendo wa Nchi hii msiolala ili sisi tulale kwa kazi yenu isiyomithilika
 
Ni nini kitachosababisha Katiba Mpya isiheshimiwe endapo itapatikana?

Kwa mtazamo wangu, Katiba Mpya haitaheshimiwa kama bado patakuwepo na mabaki ya utawala kandamizi kwenye vyombo vya kutunga sheria na kuzisimamia.

Nitolee mfano wa hapa kwetu, Katiba Mpya inaweza isiheshimiwe endapo bungeni wabunge wengi wakiendelea kuwa wa CCM, wataendelea kumlinda mwenyekiti wao ambaye ndie Rais hata kama akivunja sheria.

Au mahakamani, majaji na mahakimu wengi wataendelea kumheshimu/ogopa aliyewateua hata kama atakuwa amevunja sheria.
facts
 
Je inawezaka kuitwa katiba bora kama haijaweka misingi ya kuwa na taasisi imara za kusimamia utekelezaji wa katiba hiyo?
Misingi kwenye Katiba Mpya itakuwepo, lakini misingi hiyo kwanza itaandikwa kwenye makaratasi [non effective] ila ili ije kuwa active kwenye utekelezaji wake...

Hapa naona lazima pawepo na chombo huru cha kusimamia upatikanaji wa wajumbe na viongozi wake, ili tuepuke kuwaweka masalia wa serikali dhalimu.

Kinachowaponza waganda naamini baada ya wao kuipata Katiba Mpya, bado yule aliyewapa hiyo Katiba ana watu wake karibia kwenye kila idara muhimu, ndio maana Bobi Wine analalamika.

Na hili linasababishwa na aina ya serikali waliyonayo, ile sio ya kidemokrasia japo Museveni hushinda kwa kupigiwa kura, yale ni maigizo tu kama haya yanayotokea hapa kwetu ya CCM na Tume ya uchaguzi.
 
Namna ya kuiweka hii misingi ili ije kuwa effective baada ya kuipata Katiba Mpya ndipo mtihani ulipo.

Kwani misingi hiyo kwanza itaandikwa kwenye makaratasi, lakini ili ije kuwa active kwenye utekelezaji wake, naona lazima pawepo na chombo cha kuisimamia upatikanaji wa wajumbe na viongozi wake, ili tuepuke kuwaweka masalia wa serikali dhalimu.
It takes time , it’s not an overnight thing. It is a process that will materialize with time.
Once the constitution is in place then with time you will know its shortcomings and you will rectify them accordingly.
 
Huu ndio ukweli. Mfano zipo sheria nzuri nyingi tu lakini hazifuatwi. Kuna sheria inayotaka vyama kuitaarifu Polisi kabla ya mikutano yao? Lakini hii imekuwa fimbo ya kudumu kwa wapinzani na wameshindwa hadi sasa kupinga hilo hata kimahakama.
 
Watu wengi wanaopayuka Katiba Mpya Katiba Mpya. Hawajui hata chochote.

Wamejaa fantasies tu na Mambo ambayo labda yanapatikana peponi tu.
 
It takes time , it’s not an overnight thing. It is a process that will materialize with time.
Yes, I agree with you 100% especially kwenye namna ya kuwapata hao wajumbe watakaohusika kusimamia mchakato wa uteuzi wa hao viongozi kama majaji na mahakimu.
 
Yupo sahihi, ni kweli hata kama Nchi ikiwa na Katiba nzuri Bado inaweza isiheshimiwe na Viongozi wetu.
 
Je inawezaka kuitwa katiba bora kama haijaweka misingi ya kuwa na taasisi imara za kusimamia utekelezaji wa katiba hiyo?
Bob wine ni mpinzani wa kweli anajua tatizoliko wapi

Sawa Chadema watamtukana whatever lakin ana hoja

Katiba pekee sio kila kitu
 
Back
Top Bottom