- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Kumekuwepo na machapisho kadhaa kwenye mitandao ya kijamii, hususan Facebook, yakimuonesha aliyekuwa mgombea wa urais nchini Uganda, Bobi Wine, akidaiwa kukutana na Rais wa Marekani, Donald Trump. Hata hivyo, ukweli ni kwamba picha hizo zinazosambaa mitandaoni zimetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya akili unde, na si halisi.
Licha ya kwamba mgombea huyo wa urais alikimbilia Marekani baada ya kuhofia usalama wa maisha yake kufuatia matukio yaliyojitokeza wakati wa uchaguzi mkuu nchini Uganda, hakuna ushahidi unaothibitisha kuwa amekutana na Donald Trump kwa mazungumzo rasmi.
Ufuatiliaji uliofanywa kupitia tovuti rasmi za Ikulu ya Marekani haujaonesha taarifa yoyote kuhusu mkutano kati ya viongozi hao wawili.
taarifa hizo za kukutana na raisi wa marekani zinajili mara baada ya Bobi wine kuchapisha taarifa kwenye ukurasa wake wa facebook ukiwa na ujumbe ufuatao"Started my international engagements today with meetings on Capitol Hill, in Washington DC."

- Tunachokijua
- Machi 18, 2026 kupitia ukurasa wake wa X (Zamani Twitter) Robert Kyagulanyi (Bobi Wine) aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Urais Uganda 2026 aliandika kuwa ameanza vikao vya kimataifa nakwa siku hiyo alikuwa Capitol Hill, in Washington DC.
"Started my international engagements today with meetings on Capitol Hill, in Washington DC."
Madai
Kuanzia Machi 21 kumekuwa na picha inayosambaa kupitia mitandao ya kijamii ikimuonesha Bobi Wine akiwa ameketi na Rais wa Marekani Donald Trump, huku walioichapisha picha hiyo wakipongeza. Tazama hapa na hapa.
Uhalisia picha hiyo ni upi?
Ufuatiliaji kwa njia ya mtandao umebaini kuwa hakuna chanzo chochote cha kuaminika kilichochapisha taarifa hiyo kuhusu mkutano ama kukutana kwa Bobi pamoja na Rais Trump kwa tarehe hizo.
Licha ya kuwa Bobi Wine yupo nchini Marekani na ameweka wazi lengo la yeye kuwa huko lakini hakuna mahali alipochapisha katika mtandao wake huo kuelezea kama amekutana na Rais Trump ukizingatia na ukubwa wa tukio husika.
Kwa kutumia Nyenzo za kidigitali ikiwemo Hive Moderation JamiiCheck imejiriridhisha kuwa picha hiyo si halisi bali imetengenezwa kwa teknolojia ya Akili Unde.
Google reverse image search kupitia kipengele cha "about this image" kinabainisha kuwa picha hiyo imetengenezwa kwa Teknolojia ya Akili Unde ya Google amapo pia Hive Moderation imeitaka "Gemini3"
Taarifa za Rais Trump kumulika Bobi Wine nchini Marekani kwa kumtambua kama Rais wa Ugana
Awali kulikuwa na Taarifa pia zinazoeleza kuwa Rais Trump amemualika Bobi Wine nchini Markani kama Rais mpya wa Uganda ili waweze kujadili kuhusu mustkabali wa Uganda kwa ukubwa wake kulingana na uongozi wao ambapo taarifa hizo pia hazikuwa za kweli.
Msingi wa haya yote ni upi?
Haya yanajiri mara baada ya Bobi Wine kushindwa katika uchaguzi wa Urais uliofanyika January 15, 2026 nchini Uganda na Rais Yoweri Museveni kuchaguliwa tena kwa awamu ya saba kuliongoza taifa hilo.