Bob Marley vs Lucky Dube

Bob Marley vs Lucky Dube

Victor Bravo

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2016
Posts
264
Reaction score
241
Ivi lucky dube na bob marley nani alikua mkali na alitamba sana enzi za muziki wake, Binafsi Wakati nakua nilikua namsikiliza sana lucky dube, lakini walionitangulia wanasema hajawahi tokea kama bob marley.. Nini maoni yako nani mkali kati ya hawa jamaa wawili. Kwangu lucky dube ni bora sauti mashairi mpka ujumbe wa nyimbo zake.
 
Lucky Dube ana mziki mzuri kuliko Bob Marley.
 
Ivi lucky dube na bob marley nani alikua mkali na alitamba sana enzi za muziki wake, Binafsi Wakati nakua nilikua namsikiliza sana lucky dube, lakini walionitangulia wanasema hajawahi tokea kama bob marley.. Nini maoni yako nani mkali kati ya hawa jamaa wawili. Kwangu lucky dube ni bora sauti mashairi mpka ujumbe wa nyimbo zake.

Mkuu reggae ni nyimbo zinazoishi.ni nyimbo unaweza ukakaa na baba yako watoto wako na mabinti zako na mama yako mkasikiliza bila kuoneana aibu,Ila sasa weka bongo flavour uone msipokimbizana.Kimsingi all in all siyo vitu vyote ni vya kushindanishwa
 
Hawa wawili huwezi kuwangalinganisha, kwa sababu kila mmoja ana ubora wake kwa staili yake na wanatofautiana zama. Kila mmoja anasimama kama Legend wa reggae. Kuna Ma-Legend wengi kwenye reggae, ambao huwezi kuwafananisha. Mimi ni mpenzi mno wa reggae, lakini hata siku moja siwezi kupata jibu kikiwashindanisha Peter Tosh, Bob Marley na Bunny Wailer, kwa sababu kila mmoja ana radha yake ya kipekee. Hitimisho ni kwamba Bob huwezi kumshindanisha na Luck Dube hutapata jibu sahihi.
 
Reggae ni nziki wa style, na kila mwanamziki wa reggae and staili yake. Kwa hiyo ukiipenda style flani basi utampenda huyo mwanamziki. Bob anastaili yake
Luck Dube ana staili yake
Alfa Blondy, Culture, UB40, Gregory Isaac na wengine wengi wana stlye zao.
Kwa kweli sitamuelewa mtu atakayesema mwanamziki flani wa reggae yuko juu ya mwenzake. kwanza nitamuona hajui mziki wa reggae.
kwangu hata mtanzania Justine Kalikawe ana mziki mkali zaidi ya Bob. Hata hivyo na Bob nae anemambo yake makali ambayo Kalikawe hana.
Mziki wa reggae ni mziki wa ujumbe, sala-imani na burudani. mwanamziki mingine anaweza changanya yote hayo au akaweka kipengere kimpja tu.
tena kuna aina mbalimbali za reggae, mfano roots, sweet reggae, reggae maffin nk.
Pia kuna mwingine atapenda live perfomance, mwingine atapenda mashairi zaidi, mwingine atapenda kuchanganya kila chombo cha mziki, mwingine atapenda baadhi tu ya vyombo ya mziki.
kwanza kwa wana reggae wa ukweli hakuna atakayeanza kulinganisha mziki wa mtu na mtu mwingine. huo ni utengano na ni uchochezi.
Tulinganishe miziki mingine tu... Reggae tuachane nayo
 
Back
Top Bottom