Bob Amsterdam ni Mamluki; Watanzania tuweni macho sana

Pulchra Animo

JF-Expert Member
Jun 16, 2016
3,398
2,990
Watanzania wenzangu, napenda kutoa angalizo muhimu sana. A political mercenary is a gun for hire!

Tufanyeni makosa mengine yote tunayoweza kufanya, lakini shime shime tusije tukaingia kwenye mtego wa kuruhusu matumizi ya mamluki kwenye chaguzi zetu!

Ni kawaida ya mamluki yeyote kukosa utiifu kwa nchi alikokodiwa kuendesha shughuli zake za mamluki. Yeye hasimamii maslahi ya nchi husika. Utiifu wa mamluki ni kwa mteja wake. Period.

Ukiingia kwenye mtego wa kuruhusu matumizi ya mamluki, umeingia kwenye shimo refu na lenye utelezi mbaya. Kumbuka, Robert Amsterdam sio political mercenary pekee aliyepo duniani. Wapo wengi.

Let’s assume nchi imeingia kwenye huu mtego na Bob Amsterdam amefanikiwa kumueka mteja wake madarakani. Huu sio mwisho wa ngoma ya aina hii. Ni ngoma ya watu wazima; inakesha! Huu utamaduni ukishajengeka, baadaye mwingine mwenye uchu wa madaraka, kama yule wa kwanza, naye atatafuta mamluki wake na before we know it, we’re back to the drawing board. Je, huu ndio utamaduni tunaotaka kuujenga? Tutakuwa nchi ya aina gani hiyo?

Utamaduni wa kukubali matumizi ya political mercenaries ni utamaduni unaopaswa kuogopwa kama ukoma. Tusije tukadhani mwaka jana U.S. Congress ilipochukua hatua ya kumuondoa madarakani Bwana Trump kwa makosa mawili, likiwemo la kuwatumia Urusi ili ashinde uchaguzi, ilifanya hivyo kujifurahisha. Wanatambua risk kubwa ya kuruhusu matumizi ya foreign powers kwenye chaguzi zao!
 
Bila wewe kwenda Dodoma na Bashite kumpiga risasi Tundu Lissu angefikaje Belgium? angejuanaje na Amsterdam? huona kuwa wewe ndiyo chanzo cha kila kitu? na pia ni kwa nini umeubaka kuulawiti kuunajisi uchaguzi mkuu?

Tume huru ya uchaguzi ni muhimu kwa sasa kuliko hata chakula kwani ushetani wa NEC, Tume, wakurugenzi, na Polisi umepora haki za wapiga kwa kuisimika CCM ikulu kienyeji pasipo idhini baraka za wapiga kura.
 
Bila wewe kwenda Dodoma na Bashite kumpiga risasi Tundu lisu angefikaje Belgium? angejuanaje na Amsterdam? huona kuwa wewe ndiyo chanzo cha kila kitu? na pia ni kwa nini umeubaka kuulawiti kuunajisi uchaguzi mkuu? Tume huru ya uchaguzi ni muhimu kwa sasa kuliko hata chakula kwani ushetani wa NECCCM Tumeccm wakurugenziccm na Polisiccm umepora haki za wapiga kwa kuisimika CCM ikulu kienyeji pasipo idhini baraka za wapiga kura.
Akijibu nistue
 
Nchi ina miaka 59 hakuna maendeleo licha ya kuwa na rasilimali nyingi kuliko mataifa mengi Duniani cha ajabu mtu akija na pesa cash nyingi Airport anaporwa na akipitishia Bank zikionekana BOT nao wanampora kisha kumtishia kesi za utakatishaji fedha.

Nchi inakosa pesa Akiba ya pesa za kigeni imeshuka mno, wafanyabiashara wakubwa wote sasa wanatumia mabenk ya Uganda, Kenya na Zambia ambao wapo busy kuinua uchumi hawana time kupora wafanyabiashara pesa zao kisha kuwabambikia kesi za uhujumu uchumi ama kuwapa vitisho vya kesi kesi zingine, CCM inaporomosha uchumi kwa visheria vyake vya unyanyasaji kwa wafanyabiashara
 
Bila wewe kwenda Dodoma na Bashite kumpiga risasi Tundu lisu angefikaje Belgium? angejuanaje na Amsterdam? huona kuwa wewe ndiyo chanzo cha kila kitu? na pia ni kwa nini umeubaka kuulawiti kuunajisi uchaguzi mkuu? Tume huru ya uchaguzi ni muhimu kwa sasa kuliko hata chakula kwani ushetani wa NECCCM Tumeccm wakurugenziccm na Polisiccm umepora haki za wapiga kwa kuisimika CCM ikulu kienyeji pasipo idhini baraka za wapiga kura.

Nadhani the right thing for me to do is to ignore you. Hujui unachokiongelea!
 
CCM wanatumia pesa nyingi kwa mambo yasiyo na tija kwa Taifa, pesa inayotumika kudidimiza demokrasia kuwahujumu kuwadhoofisha CHADEMA ni pesa nyingi mno ni pesa ambazo zingeweza kujenga viwanda kila kata Nchi nzima.

Hosptal za rufaa kubwa kila mkoa na kuajiri madaktari Bingwa tokea India, Cuba na sehemu zingine Duniani, kujenga vyuo vikuu kila wilaya, kujenga daraja toka DSM mpaka Zanzibar na Pemba mengineyo muhimu, vitu kama hivyo vingeweza kuwapa kura CCM kiwepesi kuliko kwenda kupora kuiba uchakachuaji kama walivyofanya sasa wamempora Nchi kwa njia haramu za kishetani, hawataki kuleta maendeleo na hata kukiwa na vimaendeleo kidogo navyo hujaa ufisadi mwingi kama uliopo sasa kwenye SGR flyover bwawa la umeme na miradi yote mikubwa.
 
Msituingize Watanzania wote kwenye matatizo ya kujitakia, unyama wa watu binafsi. Tunajali nchi sio matumbo binafsi ya watu kwa kupitia chama.

Mercenary tangu lini akapigania maslahi ya nchi badala ya maslahi ya mteja wake?
 
Nchi ina miaka 59 hakuna maendeleo licha ya kuwa na rasilimali nyingi kuliko mataifa mengi Duniani cha ajabu mtu akija na pesa cash nyingi Airport anaporwa na akipitishia Bank zikionekana BOT nao wanamora kisha kumtishia kesi za utakatishaji fedha, Nchi inakosa pesa Akiba ya pesa za kigeni imeshuka mno, wafanyabiashara wakubwa wote sasa wanatumia mabenk ya Uganda, kenya Zambia ambao wapo busy kuinua uchumi hawana time kupora wafanyabiashara pesa zao kisha kuwabambikia kesi za uhujumu uchumi ama kuwapa vitisho vya kesi kesi zingine, CCM inaporomosha uchumi kwa visheria vyake vya unyanyasaji kwa wafanyabiashara

Sera za ujamaa wanataka kuujenga kwa kizazi cha sasa.
 
Yaani ukiona viongozi wa upinzani wanaojinasibu wanataka kuchukua nchi halafu hawana backup ya wananchi ujue ni wahuni wachache wanaleta chokochoko.
 
Back
Top Bottom