Boarding Schools 1970s-2000: Kambi za watu katili, wanaopenda masomo, mateso, ukakamavu, walokole na wazinzi

Naona umejifanya "Stering wa picha" , wewe ndio ulikuwa mjanja na wenzako wajinga, umehadithia wenzio walivyodhalilishwa huku ukificha yaliyokukuta
Hata uwe mjanja lazima ugongwe siku Moja anyway jamaa kasimulia vizuri na hawezi kujisimulia negatively mwenyewe
 
Kuna maeneo na majina sitoyataja kwa makusudi ili kuficha walioathirika na matukio yaliyotokea ambao kwa sasa wengine ni watu wakubwa na vyeo vyao serikalini na vyombo vya dola.

Ilikuwa siku ya jumamosi mida ya saa 9 ndo naingia eneo la shule. Ni mkoa wenye baridi sana. Nawaona watu mbalimbali wenyeji wakiwa wamevaa nguo nzito kiasi flan wamekusanyika maeneo mbalimbali wakiota moto na kuchoma mahindi.

Tunapotembea mimi na watu wengine wawili mimi nikiwa na bag langu kubwa la mgongoni na sanduku la bati ngumu (trunker) amenibebea mwnakijiji mmoja ambaye ni mbeba mizigo. Pia juu yake limefungwa godoro la futi nne kwa sita nchi 6.nawaona wenzangu wengine wawili nao na mabegi,godoro na hayo masanduku.

Wanatokea watu watatu wanakuja kumpokea mmoja ya wale wanafunzi. Mimi nlikuwa na bro mmoja ambaye tunatoka naye mtaa mmoja dar so alikuwa kama kaka yangu. Na wenzake wawili. Wale wanafunzi wenzangu wapya mmoja wao akapokelewa na mtu mmoja mkubwa kiasi na amekomaa. Alikuwa amevaa viatu kama vya jeshi vyeusi na surual ya jeans imepauka inambana imemlegea kidogo kiunoni.alimfuata yule mgen mwenzangu na kumpokea mzigo na ghafla akaanza kulia kwa sauti huku anaomba apewe bag abebe. Yule mwanafunzi ambaye nlikuja kumfaham kwa jina la sunday akagoma kwanza lakini alipoona jamaa anasisitiza akampa.jamaa akabeba ule mzigo huku akilia na kuongoza njia.cha ajabu wenzake aliokuja nao wala hawakusema kitu zaidi ya kutembea kama vile wapo kwenye majonzi.

Wakiwa wanatembea akaja mwingine huyu alikuja na furaha sana akicheka na kuonesha furaha akampokea mwingine nliyekuja kumfaham kuwa anaitwa shaban.akamkumbatia.shaban(jina bandia kwa sasa huyu ni XXXXXXXXXXX hapa nchini) akashtuka kidogo jamaa akaomba ampokee na kumakaribisha kwa bashasha kubwa sana. Naye akabeba mzigo akaongoza kuelekea barabara moja ambayo kuna kibao kimeandikwa shule ya sekondar XXX.

Tukaelekea huko hapakuwa mbali sana.kwa kweli nlikuwa nasikia baridi mpaka meno yanagongana nikawa nmajikumbatia pamoja na kuvaa coat zito halikufua dafu.

Ilifika jioni baada ya kila mtu kuwa ameoneshwa sehem ya kuishi.kulikuwa na mabweni makubwa manne. Ila mimi na hawa kaka zangu mmoja tukiwa tumetoka naye dar tulienda kukaa nyumba moja ambayo ilikuwa zaman ya mwalimu ila ikabadilishwa kuwa bweni kwa viongozi.huyu bro alikuwa kaka mkuu, mwenzake mmoja alikuwa waziri mkuu na mwingine waziri wa chakula.

Usiku kama saa mbili mlango ukaja kugongwa... Akatoka bro( hivi sasa ni mtumishi wa Mungu) wakaongea maneno kadhaa akaja kunambia wenzangu wananiita niende prepo(masomo ya jion) nikamwambia sina cha kwenda kusoma na nmechoka.kule mlangoni jamaa akasisitiza basi hata nikawasalimu.

Nikaona isiwe shida sababu ya mazingira ya kule nlikuwa nikaenda room nikavaa combat, coat zito na boots nikafika mlangon nikamwona jamaa siyo friendly ila analazimisha kuonesha yupo friendly na wenzake kwa nyuma ule ukimya wao ulinishtua. Nikawaambia subiri nikarudi ndani. Nikaenda kubadilisha mkanda nikavaa mkanda wa mzee ambao alikuwa anautumia zaman alipokuwa mwnajesh.

Walikuwa jamaa watatu wakanichukua wakanambia twende wazee wakakusalimu. Kulikuwa na giza shulen tulikuwa tunatumia taa za solar sabab umeme ulikuwa bado kufika. So njia nzima ilikuwa giza kunasikika tu sauti ya wadudu na wanaonekana wale wadudu wanaotoa mwanga wanaruka ruka.sikuwah kuwaona mwanzo nlikuwa nawaogopa nikidhan wanaweza niunguza.nlipoona wenzangu wanakaza mwendo sikujali nikapiga moyo konde. Mbele nikasikia sauti ya kilio na jamaa wakifoka "salimia wazee" kulikuwa na kimto maringo ile sehemu hakikuwa kinakauka miaka yote.maji yalikuwa ya baridi sana. Nikaona mtu analazimishwa akae chini ya maji akiibuka anachapwa viboko maji machafu yenye matope...anazama akiibuka anachapwa anarud kwenye maji.

Nikaingiza mkoni chin ya coat nikalegeza mkanda. Yule jamaa kule eiendelea kumpa kipigo wakiwa walikuwa watu wawili waliojifunika usoni.mimi nikapata wazo hali si nzuri hasa baada ya kuona jamaa nliokuwa bao kama wanataka kunitanguliza basi nikawa makini. Jamaa mmoja alinisukuma ili nianguke kumbe mwenzie nlikuwa standby nikaenda mbele kwa kasi sikuanguka nikawa tayar nmeshachomoa mkanda na kumpiga nao aliyenisukuma alipiga kelele "jichoooooooo" kile chuma cha mkanda kilimpasua jicho. Tayari mimi nlikuwa nmeshapandisha mori. Nawaambia asogee mwngne.kile kilio kiliwafnya jamaa wasije mmoja akasoge nikampiga na mkanda kichwan akachanika mwingne akakimbia na hawa wakakimbia nami nikawa nakimbia kurud bwenini kwangu sasa. Nao wakidhan nawakimbiza mpaka walipotokomea kwnye miti mi nikarud bwenini.nahema sana nina mkanda mkono na damu imenirukia.

Wale mabro kuniona wakaniuliza umeumizwa na nini sikujibu kitu nikavua lile coat...mmoja akatoka kasi kuelekea kwenye mabweni ya jumla.kufika kule anasema likumkuta mwanafunz mmoja kapasuka jicho lote na mwingine kachanika kichwan.

Akarud kuuliza ilikuwaje.nikamweleza.yule wa jicho haraka akapelekwa dispensary na alichanika hapakuwa pakubwa sana akagoma kwenda.ikawa usiku mzito ambao sikulala kwa amani maana nlikiwa nawaza nini next.

Jumapili mapema nliamka nikawa nje nasubiria nini kinafuta pale kwenye kabwen ketu walikuja watu weng kiasi wanaoneshana vidole vikinielekea mimi.wakawa na mengi ya kuongea.

Yule jamaa alichukuliwa na gari la misheni kupelekwa mjini kwa matibabu.jumapili tete ikapita.jumatatu asub assembly tukakaribishwa na yakatolewa matangazo ya matukio makubwa mawili moja la form one mmoja(njuka) kuteswa mpaka kuamua kuondoka kurudi home na lingine form two wawili kujeruhiwa.mwalim akataka wahusika wapite mbele.wote wakanyamaza.wale waliokuja kuniita pia hawakujitokeza..... Huo ulikuwa tu mwanzo wa maisha ya kisasi,ubabe na masomo shuleni hapo. Ulikuwa mwanzo wa kuanza kuishi kwa matumaini, looking over the shoulders na kwa umakini kila hatua. Yalikuwa maisha yaliyojaa hofu isiyo na woga na ujasiri wenye wendawazimu.

NB: NITAPUNGUZA BAADHI YA DETAILS HASA BAADA YA JAMAA MMOJA NLIYESOMA NAYE KUNIPIGIA SIMU AKIHISI KABISA NI MIMI NMEMZUNGUMZIA YEYE. NA LENGO LANGU NI KUBAKI MTU ASIYEJULIKANA. HIVYO NTAONDOA BAADHI YA DETAILS ILI WAHUSIKA WASIJE WAKAFAHAMIKA. SI LENGO LANGU KUWA EXPOSE. WENGI WANA NAFASI MUHIMU KITAIFA. KASORO MIMI TU.

INAENDELEA....................................................................................................

aliyepelekwa town kutibiwa hakurudi tena shuleni sijui ila wazaz wake walikuja shule kukawa na kikao na walimu.wanafunzi pamoja na kubanwa sana hakuna ambaye alikuwa na ushahidi kamili kuwa mtendaji ni nani kwa kuwa wahusika wakuu waligoma wakisema kuwa ilikuwa usiku na aliyewafanyia hivyo hawakumuona vizuri. ile issue ikawa imewashtua sana wanafunzi. ndo nikaja kupata kisa cha sunday ambaye ndiye aliyekuwa siku ile usiku akizamishwa kwenye maji yenye matope akiibuka anachapwa viboko. inasemekana alirudi usiku bwenini akiwa ameloana na mmoja wa wahusika alikuwa ni yule ambaye alimfuata kumpokea akilia.

kumbe alikuwa akilia akimwonea huruma jinsi atakavyomtesa. ilipofika jioni alimfuata na kumwambia ampatie tsh 100 ya kwenda kununulia ganja. yule bwana mdogo alimjibu kihuni tu kuwa aachane naye ye si baba yake na ukichukulia ametoka town basi sunday alikuwa anajichukulia ye mhuni wa town wasingemweleza kitu kule bush.kumbe maskini "jogoo la mjini pia haliwiki shamba" jamaa aliponyimwa ile pesa alilia sana...alilia akajigaragaza chini wenzake wakawa wanambembeleza kuwa basi anyamaze hayo mambo yana mwisho aliyemnyima yeye ndo aliyempa sunday.

wakamwondoa huku akilia sana. kumbe ndo alikuwa namlilia sunday. basi jioni ndo wakamfuata sunday bwenini kuwa kuna mgonjwa wakasaidiane kumpeleka hosp bweni la wanawake. sunday tena kusikia bweni la mademu akajua ndo nafasi ya kwenda kujitambulisha usiku huo...ndo safari yao ikaishi kwenye kijito..mto maringo. kesho yake asubuh aliondoka na bus la kwanza la kwanza kwenda town.akawa ameacha na shule.

nakumbuka siku hiyo tumetoka kula jamaa mmoja kidato cha pili akanifuata kunambia kuwa ye hajashiba anahitaj chakula changu.nikampa kile chakula akachukua akamwaga akaondoka.sikujibu kitu.ilikuwa mchana watu waliona kile kitendo. jamaa tena msosi wa jioni alinifuata wakati nakula kwenye meza yangu akaweka mikono yake michafu kwenye bakuli langu la maharage ambayo mimi nlikuwa nimeyaunga na blue band yamenawiri.

halafu akaondoka.. wenzie wakacheka sana... kidato cha nne. yule bro wangu alikuwa ameshaniambia niyaache yale mambo yapite alikuwa ananifaham kuwa nlikuwa mkorofi sana ingawa sura yangu ilikuwa ya upole na ukichukulia nina rangi nyeupe walikuwa wananiona kama mtoto wa mama sana.nikamwaga yale maharage nikaenda kuosha bakuli na sahani nikaenda zangu bwenini.siku hiyo sikuweza kulala nilikuwa nageuka geuka tu kitandani. asubuh mapema nikaamka nikaenda uwanjani kufanya mazoezi nlishaona kuwa sasa natakiwa kugangamaa ile mbaya.

basi muda si mrefu jamaa akashuka chini pia uwanjani ye alikuwa anacheza mpira siku hiyo ilikuwa jumamos so akawa anakuja kufanya mazoezi...akapiga mpira ukaja kunigonga upande ambao nlikuwepo akanambia nimpe nikamrushia.akaurudisha kwangu kuwa nina kiburi nimpelekee...nikaushikilia ule mpira. akaamua kunifuata alipofika karibu nilimpiga nao usoni nikamvamia akaanguka chini.nlikuwa tayari mapepo yamenipanda nlikaanza kumpiga kikatili sana. jamaa wengine wakawa wamepigwa na butwaa... jamaa akawa kama amepoteza faham nikaanza kumburuza huku nikipiga makelele namburuza kuelekea bwenini... watu waliogopa sana kwa kile kitendo. waliniona kama nimepagawa.... kumbe kuna ambao walikimbia kwenda kumwambia yule bro kuwa mdogo wako anaua uwanjani.

bro alikuja anakimbia kuniona alishtuka sana... akaanza kukemea..jamaa alikuwa mtu wa dini...akanishika kichwani huku watu wamenishika mikono jamaa yule wakawa wamemchukua mimi nlipelekwa bwenini yule bro na wenzie wakawa wamebaki nami...hawaelewi.ile issue ikawa imesambaa shule nzima. mimi akili zikaanza kunirudia. nikawa nawaza nlikuwa nafanya nini....nikijiangalia nimechafuka ile mbaya. nlianza kuliakwa sauti kubwa ...ndo wale ma bro kunituliza nikaenda kuoga nikaudi kulala.sikuweza kula nikawa kama mgonjwa.

ile shule ilifika kwa walimu jumatatu asubuh wakaka wakajadili saa nne nilikuja kuitwa na yule jamaa alikuwa ameshatolewa hosp amevimba sana usoni. wakaitwa mashahidi kuelezea kisa kizima.walimu wakawa wanachanganyikiwa.ikaamuliwa wote tuadhibiwe kwa kupewa adhabu ya kuchimbua visiki.

shabani yule ambaye likuja kupokelewa kwa nderemo,hoi hoi na vifijo kuna jamaa moja likawa kumbe linamfanya kama ni mke wake. shaban hakuwa mshali alikuwa akitumwa kitu naenda anafanya.kumbe wale waliotumwa kumpokea ndo waliambiwa wakamchagulie jamaa mke. jamaa alikuwa anavuta bhangi masaaa 24x7 ni form 2 lakini utadhani form 6 alikuwa amekomaa sana.siku hiyo nimekaa naye tunatunishiana misuli ananambia dogo mi ntakuondoa duniani. nlimwambia "mi nshakufa mara nyingi sana hawezi kuniua tena" nikampiga beat sana mbele za watu kuwa kama vipi uchorwe mstari....."nlimwambia mimi ukichaa wangu sihitaji kuvuta bhangi"... mama yangu alIshavuta bhangi nikiwa tumboni so ipo kwenye mishipa yangu tayari" jamaa aligwaya... na alikuwa ameshaambiwa matukio yangu nadhan akaona mi si mtu wa kawaida.maana sikuwa nikiongea sana.

shaban pesa zake za matumiz alikuwa anatumia na lile jamaa...(siku hizi nimeambiwa lipo mkoa flan linafanya biashara za mazao) shaban alikonda sana.... kulikuwa na malalamiko ambayo walimu walikuwa kama hawayasikilizi. maana yalikuwa hayafanyiwi kazi. nakumbuka form one mmoja alipoambiwa akapige simu chooni wakati huo kuna jamaa wapo wanajisaidia.yule form one kainamishwa kichwa chake karibu na eneo la choo kuwa awaambie wazaz wake wamtumie pesa. yule bwana mdogo aliinama mi naingia chooni ndo namwona anamalizia kuongea ameinuka...niliumia sana. yule bwana mdogo uso wake ulianza kupatwa na ugonjwa nadhan sabab ya lile joto la chooni...

siku ya jumamosi moja tumekaa tunakunywa uji akatokea jamaa mmoja akamwambia form one mmoja .... we njuka... njoo. akampa tsh 10 akanunua vitumbua 10 awaletee jamaa pale walikuwa wamekaa. wakati kitumbua kimoja ilikuwa tsh 5. yule form one akasema basi ngoja nikachukue pesa.jamaa wakamwambia awaletee wametema mate yakikauka ole wake.yule bwana mdogo alitoka mbio kwenda bwenini akaongeze hela then akawanunulie vitumbua.akawaletea wakam mind mate yamekauka wakampa adhabu ya kuwaletea tena uji watu wale 10 kidato cha pili.

ilikuwa form one akifanya kosa kumkosea kidato cha tatu lawama zinaenda kwa form two kuwa inakuaje wanawalea wale njuka vibaya wanawafanyia kiburi. nikapata msichana mmoja mrembo alikuwa anaitwa rose. rose alikuwa kidato cha 3 mimi cha kwanza.alikuwa mzuri sana yule dada mwenyeji wa ruvuma. alinipenda nami nlimpenda.ile ilikuwa issue ambayo iliwaudhi sana kidato cha pili na cha tatu hata cha nne pia maana yule demu hakuwah kutembea nao wote huko. wakajenga chuki inakuaje kidato cha kwanza anatembea na kidato cha tatu.

jioni ikifika kabla ya taa kuwashwa saa moja kamili tunakuwa tumejibanza sehemu tunapiga story na kunyonyana mate.. yule dada alikolea kiasi kwamba akawa anakuja kusomea darasan mwetu. hadi walimu wakafaham natembea na kidato cha tatu. nakumbuka kuna mwalimu mmoja alikuwa naitwa "ROBOT" huyu alikuwa anaogopawa kwa viboko... ilikuwa akikuita kama ulipelekwa kwake kwa kosa hakuachi hivi hivi.... lazima akuchape. hata ukijitetea vipi ukatoa na ushahidi.anakusikilizaaaaaaa...wala hakukatishi.ukimaliza anakwambia "haya lala chini" anakutandika ndo anakwambia haya nimekusikia nimekuelewa usirudie tena au haya nadhan basi walikosea wao viongozi.ila anakutandika kwanza. akapewa jina la Robot kwa maana ya kwamba maelezo unayompa huwa haelew yeye ni kuchapa tu.

ilitokea siku moja tumecheza mechi na wanakijiji walikuja kwetu.refa alikuwa wao tukacheza ile mechi ilikuwa ngumu sana na refa alionekana kabisa kuwabeba.nao walikuja na washangiliaji wao wa kijijini hapo.tulipiga bao mbili refa akazikataa halafu wao wakapiga bao la kuotea akasema mpira uwekwe kati.ikawa shida sana tukajipa moyo tutarudisha imefika mapumziko mwanafunzi mmoja wa kike akapita maeneo ya wanakijiji nao walikuwa wamedata sana tu.wakamkamata wakamtia vidole..yule dada akapiga kelele wakamwachia.akaja upande wtu analia.haraka waziri wa ulinzi na usalama akateua kamati ya ulinzi na kufuatilia suala lile.

yakapendekezwa majina.jina langu katika form one lilikuwa la kwanza na wengine 3 toka form one kumi toka form 2 na wa 6 toka form 3. form wao walikuwa wnaajiona wameshakuwa ni kaka na dada zetu wao wanajiandaa na mitihani. tukakaa kwa mara ya kwanza tunaongea kwa umoja form one na form 2. mpira ukawa umeanza kipindi cha pili.kilekikao kikaamua kuwa lazima kile kitendo kilipwe.akatafutwa mtunza vifaa huko store akaambiwa kuna madarasa ambayo walipaswa kufyeka nyasi wapewe mafyekeo na majembe.hakujua maskini yule dada akatoa. watu wakachukua majembe wakabaki na mipini na waliochukua mafyekeo nao wakawa standby.

basi mpira unakaribia kwisha akatumwa tena mdada kundi la wale jamaa kuuliza kuwa wakati wanamsonga songa yule dada aliangusha saa inahitajika.jamaa wakamdaka tena kumbe tulikuwa tumeishajipanga.tuliwapa kipigo kibaya sana... wengi walijeruhiwa na wana wake wao tukawakamata na kwenda kuwafungia kwenye darasa moja..walikuwa wakilia na kupiga kelele..wakajisaidia haja ndogo mule ndani.wanaume wakakimbia kwenda kijijini kujipanga. hali ilikuwa mbaya.tulijipanga kulinda mabweni yetu na ya wanawake. mkuu alipopata taarifa haraka sana akaenda kumwita mwenyekiti wa kijiji na wazee kadhaa ambao yeye alikuwa anawasaidia saidia pale kijijini.wanakijiji kule nao wakaenda kuchukua zana za jadi.

ukafanyika usuluhishi kwa mbinde sana na shule ikalazimika kununua mbuzi wawili wachinjwe kutengeneza aman maana tulikuwa tunategemeana sana pale kijijini.ila kiuhalisia sisi ndo tulikuwa na wakat mgumu sana.maana mahitaji yetu yalikuwa yanapatikana pale center ambako tulishapigwa wanted tusionekane.tena ukichukulia ilikuwa haturuhusiw kwenda town bila uniform basi ilikuwa rahis kutung'amua.ile issue ikaisha ingawa wale jamaa ambao tuliwateka wake zao waliapa lazima tuoneshane tena umwamba.ika hatuendi mjini mpaka angalau tuwe watu 5-10.

tarehe 9/9 saa 9 usiku ilikuwa ni siku maalum ya kuwakata mkia form one.baada ya siku ile form one walikuwa wanapunguziwa mateso kwa kiasi kikubwa.maana sasa wanaonekana kuwa wameshakatwa mikia.form one walikuwa wakiitwa Salamander hivyo tarehe hiyo ndo ilikuwa siku maalum ya kuwakata mikia..... siku hii ilikuwa mbaya sana kwa kidato cha kwanza. siku yao ya hukumu.siku ya kilio,mateso,huzuni adha,kilio na kusaga meno.......

ITAENDELEA..........
Eeeheee endeleza uzi
 
Kaka nimesoma kipindi cha second Master aitwaye Sungusungu, akina mwalimu Shebby (mzee wa moshi), Babu Tangalo. Ilikuwa nuksi sana kaka kilichonisaidia kuishi maisha hayo ni upole, heshima na kujishusha. Shule zote za kanda ya ziwa ikiwemo aliyofundisha raisi Magufuli walikuwa wachumba tu.
Unaweza kuwa mwanafunzi wangu ingawa sijafundisha darasa lenu,unaweza kuwa darasa la akina Tumaini Makene,vipi Mr Mahushi bado yupo hapo Geseco?
 
Kaka nimesoma kipindi cha second Master aitwaye Sungusungu, akina mwalimu Shebby (mzee wa moshi), Babu Tangalo. Ilikuwa nuksi sana kaka kilichonisaidia kuishi maisha hayo ni upole, heshima na kujishusha. Shule zote za kanda ya ziwa ikiwemo aliyofundisha raisi Magufuli walikuwa wachumba tu.
Huyu Sungusungu alikuwa nani? Basi itakuwa juzi juzi hapa, mimi nimepita pale enzi za akina Ngussa, akaja Shima second master akiwa Shikome (huyu nimesahau jina la utani tulikuwa tunamwita nani?)
 
Mkuu nashukuru maana nikiwa nimepumzika napitia kisa chako hapa. Nataman nami nije nitoe kisa changu. Mateso ambayo umesimulia nmewah shuhudia nami miaka yangu. Boarding ilikuwa kama jeshini.
 
Back
Top Bottom