Blogu ya Michuzi na CDM

Blogu ya Michuzi na CDM

Kama bloga,nisingependa ku-comment lolote kuhusu blogu ya bloga mwenzangu.Hata hivyo,kuna mapungufu makubwa katika namna Chadema inavyoshughulikia habari na kuzisambaza kwa vyombo vya habari hususan blogu.

Mara kadhaa nimelazimika kuchukua picha hapa Jamii Forums (na kuweka shukrani kwenye post husika) baada ya kukosa ushirikiano kutoka kwa jamaa wa Chadema.Ifahamike kuwa wengi wa mabloga wanafanya shughuli hiyo kwa mapenzi yao tu ya kupashana habari (ukiweka kando baadhi ya wenzetu ambao blogu zao zina wadhamini).Sasa kama taasisi haijihangaishi kushirikiana na mabloga kuwezesha matukio au habari inazozihusu kuwekwa hadharani,kuna nyakati inafikia hatua kwa bloga kuamua kuachana na habari hizo.

Tatizo hili lilikuwa sugu zaidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita.Tovuti ya Chadema ina mapungufu lukuki kwenye kuweka habari mpya.Lakini tatizo kubwa zaidi ni kama nilivyosema hapo juu kuwa hawajihangaishi kusambaza habari zao.Gazeti linaweza kujihangaisha kusaka habari kwa vile lenyewe linafanya baishara lakini kwa bloga ni tofauti.Kinachotusukuma wengi wetu ni dhamira tu ya ku-share habari na wanajamii wenzetu.

Kwahiyo,nimalizie kwa kutoa wito kwa Chadema na taasisi nyinginezo kutambua nafasi muhimu ya blogu katika zama hizi za utandawazi zinazotegemea sana teknohama.Pengine badala ya kuwahukumu bloga waifanyie nini Chadema,kuna haja ya kuihoji Chadema ifanye nini kwa mabloga ili habari zake zisambae mtandaoni.Haigharimu chochote ku-upload picha na kusambaza kwa blogu mbalimbali badala ya kutarajia mabloga wajihangaishe kusaka picha husika huku na huko.

Na Chadema ina mengi ya kujifunza katika namna teknohama inavyoweza kuleta mabadiliko tarajiwa,mfano hai ukiwa namna Obama na timu yake ilivyoutumia vilivyo mtandao (wa intaneti) katika kampeni zake za Uchaguzi Mkuu uliopita nchini Marekani.

Ndio,Chadema wanaweza...WAKITAKA!
 
Mkuu asante sana. Bila shaka Chadema watafanyia kazi jambo hili maana bahati nzuri viongozi ni member hapa, na kwa kweli ninavyowajua ni wasikivu sana!
Kwa upande wa michuzi ni haki yake kuandika na kuweka lolote analotaka bila kulazimishwa na mtu. Ukiona hapakufai unasepa tu. Mimi hata anuani yao siifahamu maana niliwahi kuingia huko na sikupafurahia mara huyoooooooo nikaondoka na sikurudi. Sasa nyie mwatafuta nini huko? Mwacheni bwana!
Be Blessed.
 
yeye kwake kinachomatter si proffession but money, aina ya watu hawa ni kama virus maana yu radhi kufanya lolote ikiwa tu kitampatia fedha ya kuhakikisha maisha yake mkewe wa ndani na wale wa nje na tegemezi wote ni mazuri. ila nakuunga mkono magamba watu hatari sanaaaaaaaaaaaaaa
 
misupu anajichimbia kaburi! hana jipya zaidi ya udaku. salam zake
 
Wadau nimeperuzi tena Blogu ya Michuzi na kujiridhisha tena kuwa ana hila na CDM, mpaka sasa haja weka picha za mazishi ya Kiongozi wa CDM Shinyanga, Shilembi ila zingekuwa za CCM haraka zinge kuwa posted as BREAKING NEEWZ

ah,hiyo ni blog yake yeye ndo ana maamuz nayo,lakini hapa jf tunaselebuka yupendavyo,mi sidhan kama kuna sababu ya kuingia huko,ni blog ambayo haipo akilin mwangu
 
Unajua Magamba Watu Wabaya Sana!! Wanaua Proffessionalism za Watu Bila Hata Kuwa Na Huruma, Sijajua Huyu Ndugu walimpa Shilingi Ngapi????? Any way Mchumia Tumbo always Unapomshibisha Husahau Hata Kutumia Akili, Poor Issa Michuzi, Ghafla umejiua Kiproffessional!!

nakubaliana nawe 100%. the man's professionalism is dead. so long as ni tumbo lake mwenyewe limemuua, let him rest in peace. maisha yanaendelea na mwerevu haambiwi tazama!
 
kama unahizo picha mtumie. yule mara nyingi ana post kitu anachotumiwa. usilalamike tu
 
Kama bloga,nisingependa ku-comment lolote kuhusu blogu ya bloga mwenzangu.Hata hivyo,kuna mapungufu makubwa katika namna Chadema inavyoshughulikia habari na kuzisambaza kwa vyombo vya habari hususan blogu.

Mara kadhaa nimelazimika kuchukua picha hapa Jamii Forums (na kuweka shukrani kwenye post husika) baada ya kukosa ushirikiano kutoka kwa jamaa wa Chadema.Ifahamike kuwa wengi wa mabloga wanafanya shughuli hiyo kwa mapenzi yao tu ya kupashana habari (ukiweka kando baadhi ya wenzetu ambao blogu zao zina wadhamini).Sasa kama taasisi haijihangaishi kushirikiana na mabloga kuwezesha matukio au habari inazozihusu kuwekwa hadharani,kuna nyakati inafikia hatua kwa bloga kuamua kuachana na habari hizo.

Tatizo hili lilikuwa sugu zaidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita.Tovuti ya Chadema ina mapungufu lukuki kwenye kuweka habari mpya.Lakini tatizo kubwa zaidi ni kama nilivyosema hapo juu kuwa hawajihangaishi kusambaza habari zao.Gazeti linaweza kujihangaisha kusaka habari kwa vile lenyewe linafanya baishara lakini kwa bloga ni tofauti.Kinachotusukuma wengi wetu ni dhamira tu ya ku-share habari na wanajamii wenzetu.

Kwahiyo,nimalizie kwa kutoa wito kwa Chadema na taasisi nyinginezo kutambua nafasi muhimu ya blogu katika zama hizi za utandawazi zinazotegemea sana teknohama.Pengine badala ya kuwahukumu bloga waifanyie nini Chadema,kuna haja ya kuihoji Chadema ifanye nini kwa mabloga ili habari zake zisambae mtandaoni.Haigharimu chochote ku-upload picha na kusambaza kwa blogu mbalimbali badala ya kutarajia mabloga wajihangaishe kusaka picha husika huku na huko.

Na Chadema ina mengi ya kujifunza katika namna teknohama inavyoweza kuleta mabadiliko tarajiwa,mfano hai ukiwa namna Obama na timu yake ilivyoutumia vilivyo mtandao (wa intaneti) katika kampeni zake za Uchaguzi Mkuu uliopita nchini Marekani.

Ndio,Chadema wanaweza...WAKITAKA!

Mkuu umetoa maelezo mazuri mno. watu wasilalamike tu lazima watimize wajibu kwanza
 
Wadau nimeperuzi tena Blogu ya Michuzi na kujiridhisha tena kuwa ana hila na CDM, mpaka sasa haja weka picha za mazishi ya Kiongozi wa CDM Shinyanga, Shilembi ila zingekuwa za CCM haraka zinge kuwa posted as BREAKING NEEWZ

Shiiiiit!!!! umenikumbusha mbali sana kipindi nikiwa na-visit hako kablog, unajua amejiwekea utaratibu wa kuzichuuja coments zoote then anaamua ni ipi aweke, siku moja kulikuwa na mada moja iliyokuwa ina atract mawazo tofautitofauti toka kwa wachangiaji binafsi sikuchangia chochote nikawa nasoma coments za watu wengine nilishangaa sana kuona coment zoote katika mada ile zilikuwa zinasifu CCM, nikahisi pengine inatembelewa zaidi na watu wasiyo ijua vizuri CCM ikabidi nitoe critical coment kuhusiana na udhaifu wa CCM, ni kwamba ile coment haikutoka nikahisi pengine lugha za namna ile hazipendi kwenye blog yake, ili kujiridhisha na hilo nikatumia lugha ileile against CHADEMA na baada ya dakika tano ile coment akaipost, nikashangaa sana kwamba huyo michuzi anataka post zinazoonekana ni zile tuu anazozitaka yeye, basi nikaamua kuacha kupost kitu chochote kwenye blog yake na taratiibu nikajikuta naisahau hiyo blog. Sijafanikiwa kurudi tena kwenye hiyo blog ya mpiga picha wa Daily news gazeti ambalo limewahi kutabiri kwamba Dr Slaa hatoshinda kiti cha urais na ikatokea.
 
umefuata nini huko?mimi huwa sifunguii kabisa nina mwaka sasa,JF tupo juu siku moja nilikuwa na sikiliza BBC kuna mzungu mmoja alikuwa anaisifia jf mpaka raha,achana nao wataanzisha nyingi sana lkn jf kiboko yao,hapa hakuna gamba,magamba wanayo wao huko
 
Mi nazaidi zaidi ya miezi mingi tu tangu niache kuingia kule yaani naona hatatuc poteze muda kum blame
kwanini hajaweka hizo picha hata kama angeweka kuna wasomaji wangapi kule bana !!!yaani Michuzi hata ukiifananisha na jukwaa la vichekesho bado Michuzi inafunikwa sasa kuna haja yakupiga kelele nae? Labda tu kwa ushauri kama JF ikiona yafaa wangeangalia namna ya kuweka sehemu ya matangazo ya misiba kwa kua huu ni mtandao wa jamii na hizo ni huo ndio ukamilifu wetu kijamii au imekaaje wakuu?
Yaani Michuzi ni kilaza kinoma hajui unapokua na blog unahitaji kuweka mahitaji ya jamii husika na sio mahitaji ya washika pembe wako.
Ona jamiiforums ilivyojitosheleza kwa mpangilio makini unadhani mtu akishaingia unadhani atathubutu kutoka humu ni kwa sababu wanaweka mahitaji ya jamii husika.
Tena ukiangalia jinsi wasemavyo wadau inasemekana wamiliki wa jamiiforums ni wanachama hai wa CCM lakini angalia jinsi wanavyoruhusu hoja zote bila bila kupendelea kwa nini michuzi usijifunze kwa hili veve kijana? Ujumbe:_Badilika Michuzi kiblog chako hicho utakua unasoma wewe na demu wako tu.
 
Kuna matangazo ya misiba mingi tu kweny michuzi blog,wanaCDM wangetuma picha na habari za huu msiba ingawa mimi ni mwanachama wa CCM Nningependa pia jamii ijuwe wanasiasa wa vyama mbalimbali .Kwa hiyo,ningependa pia kumjua marehemu na jitihada zake kisiasa.Tumeni tu habari,sidhani kama ataichuja.
Naitakia amani familia ya marehemu.......It can be done,play your part!
 
Michuzi ana benefit na serikali iliyopo madarakani. Huwezi kukata mkono unaokulisha hata siku moja!
 
kwani huku JF members wake wote ni CDM au ni ya wana CDM...basi isemwe mapema, maana kila kikitajwa CCM majority ya watu humu ndani wanalipuka!!! kila mtu ana haki ya kuwa mfuasi wa chama au imani yoyote alimradi havunji sheria za ncji hii...nawasilisha!:A S 39:
 
Back
Top Bottom