Blogs sio email inabidi ukumbuke hilo, sasa kama kila mtu ana blog yake na content ni zilezile za kucopy na kupaste hata kama ni biashara kama wengine mnavodai, kiukweli wanaofanya blogs na wanapata hela ni wachacha sana, na honestly kampuni ambayo ina-advertise kwenye baadhi ya blogs inaonyesha jinsi gani hata kichwani si wazima, najua watanzania wengine watasema ati wanasaidia watanzania, sawa lakini Unavoweka matangazo kumi na tano kwenye header ya blog yako, mfano pitia michuzi ambaye ana matangazo mengi sana, unakuta matangazo kama kumi na tano yamepangana juu kabla ya habari ya yenyewe, kati ya watu 100 honestly ni wangapi hua wanapitia tangazo moja moja na kusoma?? Honestly tu, wengi hukimbilia kwenye habari, labda wengi wataona tangazo lililoko juu tu, sasa mtu kama una kampuni na kweli unasema unajua business hasa advertising, kwa nini uweke advert yako katikati ya adverts kama hizi huku unajua kabisa halitofikia wateja?? Najaribu kuonyesha mistakes za watu na sio kwamba ninabif na wenye blogs, ila google au yahoo sio wajinga kuweka advert zao kwenye dimensions flani zikifanyiwa animation, wao nao wanafikiri wanajua ni jinsi gani mtu atakaa asiboreke na matangazo, Mfano mwingine angalia layout ya JamiiForums, kwa juu kabisa kuna googleads ambazo ni kadogo tu ila kanatosha kabisa kwa mtu kuona matangazo na still asiboreke kubrowse page, sasa yangekua yamepangana matangazo 20 kabla hujafika kwenye forums unajua ingepoteza wateja? wapo watu wanao-criticize hata hilo, inaonyesha jinsi gani mtu ni unprofessional, na kingine blogs nyingi layouts zote zinafanana, kwa nini? zinafanana alafu chafu, graphics mbaya, za kupachikwa tu, tumefika kipindi tusiseme ati "ili mradi mtu anasoma tu" uwezo wa kutengeneza something clean upo. Ukisema hadi upate hela mbona Michuzi ana matangazo mengi ya kumwezesha kufungua site nzuri ambayo akaweka content zake katika mpangilio, au unataka uniambie hana hela?? zile ads zote angekua ashafungua blog nzuri yenye layout safi, kama hawezi basi atafute designer amrahisishie kazi, ndiyo maana watu wanasomea haya mambo tanzania, kama kila kitu unataka ufanye mwenyewe hata kama huwezi aliyesomea afe njaa au? mlipe akufanyie kazi safi ili kazi yako nayo ikue na kukua... i like JF na nahisi ni moja ya sites zenye view nyingi sana per day kwa Tanzania, ni muda wa bongo kuamka na sio kufanya vitu kama watoto wadogo, akili ipo sio tunakaa na kupiga kelele ati hatuwezi...