Habarindiyohiyo
JF-Expert Member
- Aug 11, 2008
- 263
- 13
Kumezuka tabia ya bloggers wa kitanzania kuendeleza kejeli kwa Rais Kikwete kwa kutumia lugha kali kali ambazo pia zinaleta uchochezi. Kati ya Bloggers washabikia tabia hii yupo Utakapojua Hujui Ndipo Utakapojua, yupo pia huyu JJ. Watu hawa wanashindwa kutofautisha kati ya ukosoaji na udhalilishaji wa hadhi ya Rais aliyechaguliwa kwa asilimia 80 ya watanzania wote. Mamlaka zinazohusika lazima zichukue hatua kukemea hali hii. Kama kuna blogger mwingine mwenye tabia hii atajwe pia hapa ili aweze kufahamika.Bloggers watambue kwamba wanaweza kuhukumiwa kwa maneno yao wanayoandika andika. Kama tunaweza kuikemea theutamu kwanini tuache kuwakemea hawa?
............ndiyohiyo
............ndiyohiyo