Mkuu hivi njnaweza kupata laptop yenye uwezo wa graphic design na video editing kwa chini ya 700,000 ??
Nafaka
Dah umenipa ugumu kidogo kwa bajeti hiyo, kiukweli utapata ila utatakiwa ku upgrade RAM kama itakuwa chini ya 8gb size, ili uwe na speed kwenye design & editing.
Atleast Tafuta hizi model, kama utaweza pata refublished kwa bei hiyo ila sizani kama zitakuwa chini ya laki 7 labda bahatisha
HP ProBook 450 g7
HP ProBook 655b
HP Elitebook x360
May be hizi hapa utapata Refublished kwa bei hiyo ama chini, ila hakikisha zina RAM ya 8GB na kuendelea, core i5 gen ya 4 na kuendelea.
HP Elitebook 820 g3 au 840 g1.
HP ProBook 450 g2
HP ProBook 450 g5
Kama utatumia w10 os huwa inakula RAM mpaka 3 GB hivi, hapo kama RAM ni 8gb inabaki space kubwa.
CASE STUDY:
Mkuu nimewahi fanya video editing maeneo flani nilikuwa natumia hp notebook 840 g1 na nilikuwa natumia premiere Pro cc17 na after effect cc17, kwenye kurender/encoding media encoder ilichukua muda japokuwa kuna kuna ku optimize bit-rate, ila ilitumia masaa mawili hadi matatu, ulefu wa video ninayo edit ni 30min ukijoin vipande, text, logo ama lower3rd.
RAM ilikuwa 4gb, mkuu but after upgrading to 8gb ilikuwa very smooth.
Asikudanganye mtu hatakama utatumia wondershare filmora, movavi, power director, davinci resolve bado unahitaji mfumo kaka.
Render Render Render Render Render Render Render Render Render Render inakela.
Wadau wengine watakuja kukupa ushauuri kulingana na ujuzi wao, anyway kuna gaming pc ziko vizuri pia. Kama utataka desktop itakua poa kwa bajeti hiyo.