Lukwangule
Senior Member
- May 25, 2009
- 157
- 2
MFANYAKAZI wa Shirika la Magazeti ya Serikali (TSN) Muhidin Issa Michuzi ameondoka jana kuelekea London, Uingereza, kuhudhuria kongamano la pili la Watanzania wanaoishi nchi za nje (Diaspora 2 conference) akiwa kama bloga.
Michuzi, ambaye ametoa mchango mkubwa katika kupromoti habari za jamii mtandaoni kupitia blogu yake ya issamichuzi.blogspot.com, amealikwa na ubalozi wetu Uingereza.
Akiwa katika mkutano huo atatoa mada inayohusu umuhimu wa habari za jamii mtandaoni katika kujenga daraja kwa walio ndani na nje ya nchi.
Akizungumza jana amesema amefarijika sana kuona kuna wanaotambua mchango mkubwa unaoletwa na vyombo vya habari za jamii mtandaoni, hasa blogu.
Alisema anajisikia mwenye furaha sana kuona azma yake ya kuifanya tasnia hii ya kupashana habari kwa njia ya intaneti unatambulika na kukubalika na kupewa heshima stahili nyumbani kama ilivyo kwa vyombo vya kawaida kama vile magazeti, redio na luninga.
Michuzi, anayeweka rekodi ya kuwa bloga wa kwanza nchini kualikwa kama bloga kwenye mkutano muhimu kama huo, aliushukuru ubalozi nchini Uingereza kwa kuutambua hadharani mchango wa wanahabari za jamii mtandaoni kwa kutoa mwaliko huo.
"Dunia imezidi kuwa kijiji kimoja kidogo kwa teknohama hii ambayo hata Rais Jakaya kikwete yuko mstari wa mbele kutaka iendelezwe mijini na vijijini ili kuwezesha wananchi wawe na habari za uhakika, za haraka na zenye kutoa fursa ya wasomaji kuchangia maoni" alisema Michuzi.
Blogu ya issamichuzi.blogspot.com ilianza rasmi Septemba 8,2005 katika jiji la Helsinki, Finland, ambako alikwenda kuhudhuria mkutano wa Helsinki Conference akiwa kama mwandishi na mpiga picha wa gazeti la Daily News.
Alikuwa ni bloga wa siku nyingi aliyekuwa anaishi Marekani wakati huo,Ndesanjo Macha, aliyemshawishi Michuzi kufungua blogu yake na kuwa bloga wa kwanza wa Tanzania kuupasha ulimwengu ya kila linalojiri nchini.
Blogu hiyo kwa sasa imefikisha wasomaji milioni 8, kati ya hao asilimia 30 wakiwa ni wasomaji wa Tanzania.