Ningependa kukujibu kuwa, nani kasema kuwa wanaume hawana cha kufanya hadi waanzishe na kumiliki blog zao? Mpoki aliwahi kuhojiwa majuzi na kusema kuwa kwa kweli ni kazi kuendesha blog na kufanya kazi za kiandishi. Naye angesema kuwa yuko bize, na mwingine, na mwingine je?
Ninakubaliana na Mpoki kwamba kuendesha Blog na kuifanya iwe active inahitaji muda wa kutosha na kujitoa. Michuzi akihojiwa na Bongo Celebrity Blog alisema kwamba huwa analala baada ya saa saba usiku kila siku na kuna siku nyingine huwa anakuwa macho mpaka saa tisa za usiku ili angalau aweke taswira alizonazo na kupitia comments za wadau. Je, akina mama walio na responsibilities za kazi, familia, watoto na mengineyo wana nafasi hiyo? Ukisema waende 50/50, maana yake na responsibility za ndani nazo ziwe 50/50 of which hakuna mwanaume ambaye yuko tayari kwa hilo.
Nimesema hapo awali, wanawake wanapenda kufanya yale yaliyo karibu nao. Hivyo bado changamoto ziko pale pale. Suala si kuwatetea eti wako bize na mambo yao mengine kiasi cha kuwaachia kina Dina kuvurunda.
Hata wanaume nao wanafanya yale yaliyo karibu nao, na ndiyo maana nikasema tuangalie background za bloggers, elimu na malengo ya kuanzisha blogs. Michuzi, Mjengwa, Mroky, MichuziJr, Mpoki na wengineo wa jamii hiyo walianzisha blogs za picha kwa kuwa kupiga picha ni sehemu ya fani/hobby/ajira yao. So hizo picha ni mojawapo ya vitu vilivyo karibu nao. Wachangiaji kwenye hizo blogs ndiyo wameongeza mijadala ya uchumi, jamii, na mengineyo.
Mfano, siku Liverpool ikishinda ama Man U wakishindwa, immediately after the match utakuta taswira na matokeo ya game pale kwa michuzi, lakini siku Liverpool wakishindwa ama Man U akishinda utakutana na taswira kesho yake ama usione kabisa mpaka watu wamtumie e-mail za vijembe. Ni swala la interest na mazingira ya kazi. Hivi ulishaona kwa Michuzi kuna mada/comments za kukandia CCM ama serikali? Hujiulizi ni kwanini huwa hata comments za kukandia serikali huwa hazionekani? Mazingira ya kazi ndugu yangu.
The rest of bloggers wa kiume wengi wao ni waandishi wa habari by profession na wanachokiweka huko ni news wanazokutana nazo ama makala wanazoandaa ama wanaanzisha mijadala ili kupata maoni na mwelekeo wa wachangiaji na hivyo kuwapa nafasi ya kuandika makala ambazo ziko balanced.
Kwa hiyo hata wanaume nao wanafanya kile ambacho kilicho karibu nao, hakuna blogger ataanzisha blog ya fani ambayo siyo yake. Mchumi ataweka blog ya uchumi na ndicho kilicho karibu yake. Politician atakuwa na blog ya siasa ili kuangalia joto la siasa na mwelekeo ukoje. Kwa hiyo wenye blogs wengi wanaweka vitu ambavyo viko kwenye anga zao ama ambavyo ni sehemu ya maisha yao. Na ndiyo maana nikasema angalia BACKGROUND ya blogger, it tells a lot.
Sasa kama akina Kalonga and the likes wamekulia kwenye mazingira ya mashindano ya mavazi na mitoko, marafiki wa aina gani, mavazi ya aina gani na kwamba anam-date nani na wa class gani, what do you expect from them?
Ukienda kwa Mjengwa utakuta picha za Iringa na kama siyo Iringa basi ni Dar, hususani Kariakoo na Kinondoni Biafra au Bagamoyo, au vijijini iwapo atakuwa na safari za vijijini na hizo picha ndiyo ziko karibu na yeye. Picha nyingine tofauti zinakuwa zimetoka kwa wadau ambao hutuma kwenye hizo blogs na bloggers hutoa maelezo kwamba picha imetumwa na mdau.
Nao wajitoe kama wanaume. Si wanataka 50/50?
Kwa wale walio kwenye ndoa wanaweza kujitoa iwapo mfumo dume utawaruhusu kufanya hivyo. Mfumo dume bado ni kikwazo kwa akina mama kufikia hiyo 50/50 unayosema ndugu yangu.
Nimalizie kwa kusema kitu kimoja, tunaposema akina mama/dada makini nao waanzishe blogs zao za ku-discuss mambo muhimu lazima tuelewe priorities zao, access ya mtandao na pia fursa ya kufanya hivyo. Hao walio na blogs unaweza kuta ama wako nje ya nchi au wako Bongo. Walio nje ya nchi wana access ya mtandao 24/7, na walio bongo wanaweza kuwa na access ya mtandao wakiwa ofisini na ndipo wanakofanya vitu vyao. Kwa hiyo kuna mengi sana ambayo yanaweza kuwa vikwazo kwao kuliko jinsi tunavyofikiria na inawezekana wana mambo mengine muhimu ambayo wanafanya ambayo ni mazito/makubwa na yana tija kuliko hata kuwa na blog ambayo inakuwa accessed na wale walio na mtandao tu.
Mfano Mama Hellen Kijjo-Bisimba ambaye ana kituo haki za binadam na amekuwa akifanya makubwa sana na outreach yake ni kubwa zaidi kuliko hata blog. Kuna wana harakati kibao ambao wana NGOs zao ambazo zimekuwa zikisaidia jamii na ziko karibu na watu kwa kuwa zinatoa msaada unaonekana. Mfano ni yule aliyekuwa house girl wa Mahita anatetewa na Kituo cha Mama Bisimba na si ajabu akapata haki yake. Mpaka sasa Mzee mzima Mahita ameingia mitini amegoma kwenda kufanyiwa DNA, sijui mahakama itaamua nini. Kwa hiyo kila mama anaangalia afanye kipi na kile kilicho ndani ya uwezo wake. Tusitumie hao wachache ambao walianzisha blogs bila kujua wanafanya nini na wakaishia kuzifanya ziwe za mipasho badala ya kuwa visima vya mijadala na maoni yenye kuleta maendeleo kwa jamii.