Hizi ndizo akaunti 50 za kufuata unapokuwa Twitter, JamiiForums haikuachwa

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,434
7,055
Kama wewe ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii, bila shaka unatumia na mtandao wa Twitter pia. Au kama hutumii basi bila shaka unaufahamu. Tabia za wanachama wa Twitter hazitofautiani sana na za wanachama wa mtandao huu wa JamiiForums, kuna wale wanachama watiifu na wanaopendwa sana kutokana na mabandiko yao...

Sasa habari mpya kutoka jarida maarufu la habari mbalimbali za ndani na nje ya nchi, Swahili Times, limechapisha taarifa kuhusu akaunti 50 za Twitter zenye ushawishi zaidi hapa Bongo. Humo zimetajwa akaunti za wasanii, wanasiasa, taasisi, wanaharakati na watu muhimu 50 ambao ukiwafuata ni lazima utafaidika kwa namna moja ama nyingine kutokana na mabandiko yao..

Mtandao wa JamiiForums umetajwa pia kama mtandao unaoaminika kutoa taarifa za uhakika za nyanja zote ktk jamii. Hivyo umependekezwa kama mtandao muhimu wa kuufuata huko Twitter.

Chapisho la Swahili Times nimeliweka hapa chini.

50 TANZANIANS TO FOLLOW ON TWITTER

YBGgi9BO-512x334.png

1. Jakaya Mrisho Kikwete- @jmkikwete

Rais Mstaafu yeye amejikita kwenye masuala ya kijamii, huelimisha na kuhabarisha zaidi mwanzo kuhusu kazi zake akiwa Rais lakini sasa kama Mwenyekiti wa CCM na mwanadiplomasia wa Kimataifa.

2. Maria Sarungi- @MariaSTsehai
Maria huzungumzia zaidi siasa, akiwa na lengo la kuwaelimisha watu. Katika mbio za Urais wa Marekani 2016 anaonyesha kuwa shabiki wa Bernie Sanders. Pia huzungumzia masuala mbali mbali yanayoikumba jamii amekuwa ni mshiriki wa karibu. Ni mwepesi wa kushiriki mijadala au kutumia nafasi ya wingi wa watu wanaomfuata (followers) kusaidia watu kufikisha ujumbe kwa hadhira kubwa zaidi.

3. Zitto Zuberi Kabwe- @zittokabwe
Kiongozi wa chama za ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, yeye hupenda kujadili masuala ya siasa hasa kuikosoa serikali na kuonyesha njia mbadala za kutafuta suluhu ya matatizo. Zitto pia ni shabiki wa Liverpool na huonyesha hisia zake waziwazi wakati timu yake ikiwa na mechi mbalimbali.

4. Emanuel Mgaya- mkandamizaji
Mchekeshaji lakini pia ni Mchungaji na mjasiriamali. Yeye huzungumzia zaidi mambo ya kijamii na staili za maisha. Vitu vingi ambavyo huwa anavifanya ni kuchekeza mashabiki zake. Mara chace hu-tweet vitu serious.

5. Millard Ayo- @millardayo
Mtangazaji wa Clouds FM. Ni mtu anayejituma sana, yeye huhabarisha umma kwa habari mbalimbali zinazotokea nje na ndani ya nchi.

6. East Africa Tv- @eastafricatv
Hiki ni kituo cha habari katika kampuni ya IPP Media. Kwa masuala ya muziki hawa ndiyo kazi yao lakini pia huwa wanaandika kuhusu kuelimisha jamii.

7. East Africa Radio- @earadiofm
Hiki ni kituo pacha na East Africa Tv, kama ilivyokuwa kwa Tv na hawa ndio hivyo hivyo, burudani ndio kwa wingi lakini pia kuelimisha jamii kupitia baadhi ya vipindi vyao.

8. ITV- @ITVTANZANIA
Kutoka IPP Media, wao huhabarisha sana umma kuhusu taarifa katika Nyanja zote za jamii kuanzia kwenye siasa, uchumi, michezo.

9. Salim Alkhasas- @Salim_alkhasas
Yeye hujiita Papa Mchoyo, akiandika tweet yake basi ni sawa na jiwe gizani, ujue kuna mtu anarekebishwa. Mara nyingi amekua akikosoa yale ambayo yamekua hayaendi sawa kwenye jamii papo hapo. Mara kadhaa naye hutupia tweets za siasa.

10. Mpoki- @Mpokimjuni
Yeye ni mchekesheaji, mara zote anapo tweet basi jiandae kuchecha maana unaweza jiuliza huwa anawaza nini.

11. Dani Nkurlu- @RevKishoka
Kishoka hupenda siasa sana. Karibia mara zote huzungumzia siasa akikosoa na kusifia pale panapostahili.

12. Uncle Fafi- Tanganyikan
Fafi hupenda sana Basketball. Taarifa zote za NBA ukiamka pitia TL yake. Mpaka mida ya saa tisa za usiku huwa anatweet kuhusu NBA. Lakin pia masuala ya burudani naye yumo. Pia ni mmoja wa watanzania pekee wenye followers wengi mtandaoni licha ya kwamba wao sio celebrities katika medani za siasa, soka, biashara au sanaa.

13. Nasib Abdul- @diamondplatnumz
Ni mwanamuziki maarufu, yeye huzungumzia sana masuala ya burudani. Hutweet kuhusu show zake, nyimbo mpya na mara chache kuhusu familia yake.

14. Ambwene Yesaya- @AyTanzania
Ay wengi humuita ZEE au Legend. Mara nyingi yeye huzungumzia burudani sana lakini ni shabiki wa Barcelona hivyo mara kadhaa hujadili mpira.

15. Hamis Mwinjuma- @MwanaFA
Choirmaster yeye hupendele kujadili masuala ya burudani kwa sana, lakini pia ni shabiki wa Manchester United, utamkuta siku ya mpira basi anasumbua sana.

16. Mwananchi- @mwananchinews
Hii ni kampuni ambayo huchapisha magazeti lakini pia huandika habari mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii. Hivyo huhabarisha kuhusu masuala yote ndani ya jamii.

17. Swahili Times- @swahilitimes Hii ni media house pia, tofauti na nyingine hii ni mpya, imejikita kwenye kuhabarisha jamii kuhusu masuala yanayotokea kote ulimwenguni. Inakua kwa kasi siku hadi siku.

18. Given Edward- @Givenality
Yupo sana kwenye mambo ya kijamii, ni mtu anayependa kuona jamii inakuwa moja. Pamoja na mambo mengi anayozungumzia ila ya kijamii yana nafasi kubwa.

19. Evarist Chahali- @Chahali
Ni mtanzania anayeishi Uskochi barani ulaya, hupenda kuzungumzia mambo makubwa mawili, kwanza ni siasa na mambo ya usalama (Security). Na pia mwandishi wa vitabu.

20. Salama Jabir- @EceJay
Tv Personality. Mtangazaji kwenye kipindi cha Mkasi lakini pia anapenda mpira, shabiki wa Man Utd. Mara nyingi hapepesi na huelezea mitazamo yake wazi wazi kuhusu jambo.

21. Makirita Amani- @MakiritaAmani
Yeye hujadili sana masuala ya jamii. Hupenda kuweka Makala zinazokuelimisha mfano namna ya kuongeza ushawishi kwa wengine n.k

22. John Pombe Magufuli- @MagufuliJP
Rais wa Tanzania, huandika kuhusu mambo yanayoendelea nchini. Ni vizuri kumfuata maana yeye ni kama baba wa familia, mfano siku akiamua kutweet leo hakuna mtu kutweet uweze kuona tweet yake mapema. Muhimu kuwa naye kwenye TL yako.

23. Idris Sultan- @IdrisSultan
Mshindi wa BBA 2014. Yeye ni mchekeshaji, vitu vingi anavyoandika ni ili kuwafurahisha wale wote wanaomfuata. Pia hutumia Twitter kuelezea struggles za maisha yake.

24. Carol Ndosi- CarolNdosi
Hupenda kujadili masuala ya burudani na huendesha Tamasha la Nyama Choma. Amekuwa mstari wa mbele kuandika kuhusu kutatua kero au kusaidia wenye uhitaji katika jamii.

25. Photo of Tanzania- @tanzaniaphotos
Akaunti hii huweka picha za Tanzania za zamani na sasa pamoja na za watu au maeneo ambao kupitia picha hizo tunaweza kufahamu mambo yalivyo au yalivyokuwa.

26. Fredrick Boshe- @Rickyboshe
Yeye ni Rais wa ToT 2016. Mara nyingi huandika kuhusu movie lakini pia ni shabiki wa Chelsea hivyo hujadili pia mpira.

27. Jamii Forums- JamiiForums
Akaunti hii huhabarisha umma katika nyanja zote ndani ya jamii. Kwa hiyo ni moja ya akaunti muhimu kupata habari mbali mbali.

28. Bongo5- @bongofive
Akaunit hii huhabarisha umma lakini yenyewe imejikita zaidi kwenye masuala ya burudani.

29. Haki Ngowi- @Hakingowi
Yeye huhabarisha umma kwa habari mbalimbali kuanzia kwenye uchumi hadi kwenye udaku.

30. Clouds Media Group- @CloudsMediaLive
Clouds Media Group ni kuhusu burudani kwa wingi, japo mara kadhaa huandika habari mbalimbali ila wamejikita zaidi kwenye muziki na kizazi kipya.

31. Salim Kikeke- Salym
Kutoka BBC Swahili, habari mbalimbali kutoka kona za dunia lakini pia masuala ya mpira. Mechi ikikupita basi ukienda kwenye akaunti yake utakutana na matokeo.

32. Zuhura Yunusu- @venusnyota
Mtangaziji wa BBC Swahili. Mbali na habari pia amekua akizungumzia siasa za nchi mbali mbali za Afrika.

33. Issa Michuzi- @issamichuzi
Yeye ni mwanahabari na kama tujuavyo mwanahabari hutujuza kuhusu masuala mbalimbali nchini na nje ya nchi. Michuzi ni mmiliki wa moja ya blogu ya Kiswahili inayosomwa zaidi duniani.

34. Radio one- @RadioOneStereo
Akauti hii itakusaidia kufahamu yanayoendelea kwenye Redio One hata kama haupo na redio.

35. TFF Tanzania- @Tanfootball
Akaunti ya shirikisho la soka la Tanzania, wakati wote ni masuala ya mpira na yanayozihusisha timu za mpira kutoka Tanzania

36. Blog Zetu- @blogzetu
Akaunti hii hukusanya taarifa kutoka kwenye blog mbalimbali na kuziweka pamoja. Hii utakurahisishia wewe kupata habari kutoka vyanzo mbalimbali

37. January Makamba- @Jmakamba
Waziri, mara nyingi huzungumzia siasa lakini pia elimu kuhusu mambo mbalimbali kama falsafa na majibu ya maswali ya papo kwa papo.

38. Masoud Kipanya- @masoudkipanya
Mchoraji katuni. Katuni zake nyingi hulenga kutetea watu wa chini kwa kuwachokonoa viongozi wajuu ili wakae sawa. Masoud pia ni mwanafalsafa wa kizazi hiki, huwa na tweets zenye kufikirisha.

39. Mohamed Dewji- @moodewji
Mara nyingi hujadili kuhusu masuala ya biashara na kutimiza ndoto (Inspirational quotes).

40. Pato- @PatNanyaro
Hupenda kujadili sana kuhusu masuala ya kijamii, ni mtu wa kujichanganya na watu na mara kadhaa huwa anazungumzia masuala ya uchumi na siasa.

41. Vanesa Mdee- @VanessaMdee
Unaweza kuita VeeMoney, Ni Msanii wa muziki, hupenda kujadili kuhusu masuala ya muziki na mitindo lakini pia ni Mtangazaji wa Redio.

42. E-FM DSM- @New937
Kituo cha redio cha E-fm. Mara nyingi hutoa burudani ya muziki lakini kama kituo cha redio huhabarisha na kuelimisha jamii pia.

43. The Citizen Tanzania- @TheCitizenTz
Kama kingereza kinapanda basi hili litakufaa kwa habari mbalimbali. Hili ni gazeti ambalo huandika kwa lugha ya kiingereza.

44. Hamis Kigwangalla- HKigwangalla
Naibu Waziri na Daktari pia. Hujadili sana kuhusu masuala ya afya na siasa. Na pia huwa ni mwepesi wa kujibu swali unapomuuliza.

45. BBC Swahili- @bbcswahili
Kituo hiki cha habari cha kimataifa. Suala kubwa ni kuhabarisha umma kwa kuandika taarifa mbalimbali kwa lugha ya kishwahili

46. Chama cha Mapinduzi- @CCM_Tanzania
Akaunti ya Chama tawala cha Tanzanzia. Kikubwa kinachokuwepo kwenye akaunti hii ni kuhusu chama hiki. Kufahamu jambo lolote kuhusu CCM huu ndio ukurasa wa kufuata

47. CHADEMA Media- @ChademaMedia
Akaunti ya Chama kikuu cha upinzani Tanzania. Kama wewe unapenda siasa za upinzani basi usiache kufuata ukurasa huu

48. Azam Tv- @azamtvtz
Kituo cha television. Kikubwa ni kuhabarisha na kuburudisha umma bila ubaguzi

49. Monica Joseph- @Monifinance
Ni mwanauchumi, mambo yake mengi ni kuhusu uchumi na pia siasa na mambo ya kijamii kwa kiasi.

50. Reginal Mengi- @regmengi
Ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya IPP nchini na vile vile ni miongoni mwa watu wenye fedha sana Afrika. Akaunti yake huzungumzia sana kuhusu masuala ya kijamii na siasa.
 
Hivi EATV huko Twitter ipoje? maana kwenye Facebook page yao ni utumbo mtupu, yaani wanapost vile vitu ambavyo vitazua mijadala kwa vijana wenye IQ ndogo....halafu niwa follow Twiter?
Huyu aliyeziandika kazingatia popularity ya hizo account au point zinazopostiwa na wenye account? maana account nyingine utumbo mtupu
 
No offence ila hizo account zote almost 98% ni mere politics, junk stories and hypocrisy. Huwa nashangaa followers kwenye hizo account what do they actually gain?

Mimi kwenye mtandao wa Twitter nimefollow accounts ambazo mainly ni za watu wa nje. Yaani utashangaa kila tweet ukisoma is about genuine issue. Na kwa sababu nimekuwa selective na account zinazohusu masuala ambayo ndiyo itakuwa career yangu ya baadae imenisaidia sana coz nimejikutanisha na wataalam mbalimbali na nimejifunza mengi.

Sisemi kwamba kila mtu afanye kama mimi. Ila unapokuwa kwenye social media jiangalie coz you are trading your time for information, but if those information are merely politics, junk stories and hypocrisy my friend you are being screwed
 
yeah mkuu, pia internet ina addiction, usipojiangalia vizuri unakuta masaa mengi upo unasoma umbea tu unashindwa hata kuwaza idea nzuri na kufanya shughuli zako
 
Sina neno, kwenye Maria Sarungi ila namba moja, sijui kama nikweli au magumashi maana mzee sioni aki post na akiposti zina buma.
 
yeah mkuu, pia internet ina addiction, usipojiangalia vizuri unakuta masaa mengi upo unasoma umbea tu unashindwa hata kuwaza idea nzuri na kufanya shughuli zako
Addiction ya internet ni mbaya mno kama mtu utatumia kupata info zisizo na manufaa coz ni sawa una trade mda wako halafu hupati chochote. Mi nimefanikiwa kutoka kabisa facebook, instagram na networks nyingine za ajabu. Nipo JF na Twitter tena ni kwa shughuli maalumu kwangu.
 
fb unaweza uka like page za mitandao mbalimbali zikawa zinakupa taarifa muhimu, ila instagram hapana
 
No offence ila hizo account zote almost 98% ni mere politics, junk stories and hypocrisy. Huwa nashangaa followers kwenye hizo account what do they actually gain?

Mimi kwenye mtandao wa Twitter nimefollow accounts ambazo mainly ni za watu wa nje. Yaani utashangaa kila tweet ukisoma is about genuine issue. Na kwa sababu nimekuwa selective na account zinazohusu masuala ambayo ndiyo itakuwa career yangu ya baadae imenisaidia sana coz nimejikutanisha na wataalam mbalimbali na nimejifunza mengi.

Sisemi kwamba kila mtu afanye kama mimi. Ila unapokuwa kwenye social media jiangalie coz you are trading your time for information, but if those information are merely politics, junk stories and hypocrisy my friend you are being screwed
Very true, ni upuuzi mtupu na hata hao followers wao sio kwamba wana chochote cha maana na pengine wao wenyewe huwa wana tweet nonsense . Kinachotokea watu wanakawaida ya ku-follow watu wakitarajia retweet as a way of getting mention.

Utakuta mtu anajaza server tu kwa comment tweet za kipuuzi, au ku-tweet kitu/hoja isiyokua na mashiko halafu anam-mention the so called mtu mashuhuri kutafuta approval ya upuuzi wake au retweet na hao so called mashuhuri haraka haraka ame-retweet.

Pia katika hiyo list kuna watu walishatoka tweeter mara baada ya uchaguzi na hawakua na chochote cha maana walichokua waki-tweet kabla ya hapo zaidi upuuzi na kuvunja sheria. Wapo wanaopata followers sio kwasababu wana ushawishi au wana-tweet vitu logic ni kwasababu tu huwa wanaji-patroy kama either wanawajua wakubwa serikalini au ni wajuzi wa mambo but in actual sense it's vice versa as we know they're academic background na kwamba hawana huo weledi so you can understand they're followers are of the same kada.
 
umelenga penyewe kaka sina cha kuongeza. Kuna dada ni rafiki yangu sijui huko kwenye mtandao celebrity gani ali like picha yake. Basi ndo imekuwa story kila mahali. Ni vile ni mwanamke tu nlitaka kumpa za uso maana mi sipendi kabisa mtu aniongeleshe story za kipuuzi. Yaani ujinga mtupu. Vijana wengi wanapoteza mda kwa mambo ya kijinga kabisa. Sad
 
Namuona Papa Mchoyo kwenye account yangu ya twitter. Simfahamu ni nani,sikumbuki kumfollow. Nasema sikumbuki.Maybe I did,maybe I didn't.
 
umelenga penyewe kaka sina cha kuongeza. Kuna dada ni rafiki yangu sijui huko kwenye mtandao celebrity gani ali like picha yake. Basi ndo imekuwa story kila mahali. Ni vile ni mwanamke tu nlitaka kumpa za uso maana mi sipendi kabisa mtu aniongeleshe story za kipuuzi. Yaani ujinga mtupu. Vijana wengi wanapoteza mda kwa mambo ya kijinga kabisa. Sad
Katika wote waliotajwa hapo niliyemfata ni Mzee Mengi na Dewji pekee... Wengine huwa wanajipa moyo eti ni maarufu kwa upuuzi wao huko Twitter..

Kuna hili kundi la CarolNdosi, huyo anayejiita Papaa Mchoyo, Maria Sarungi na wenzao wanaojiona maelite wa twitter Tanzania niliblock kabisa kwa ushenzi wao..
 
Hahahaha... Mimi ni Mengi tu kwa hapa bongo hao wengine sitaki kuskia kabisa. Nnao follow wengine ni wa huko duniani yaani sometime mpaka najikuta kama utamaduni wao unaanza kunivaa. Nimeamua hivo tu hata whatsapp nna kundi langu la watu wa huko duniani yaani unaona kabisa hawa watu wapo serious. Sasa hawa wabongo wenzetu unakuta watu wanajadili mambo ya hovyo tu. Sad
 
Eti Masanja na Mpoki nao ni wa lazima kuwafata teh teh teh teh huu utani huu aiseee... Mimi wabongo ni hao wawili tu na wengine ni ndugu wa karibu na school mates.. Mimi nina group whatsapp la African Young Entrepreneurs and we have the same project ya kila mmoja kuimplement on his nation.. So far we are making some steps
 
Back
Top Bottom