Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 1,576
- 2,071
Habarini za mchana.
Ninaleta uzi kidogo kuhusu ishu ya black magic, kwani katika soma soma ya vitabu nimepata vitu kidogo vya kuwashirikisha, karibuni.
Tuanze nini maana ya Black Magic: huu ni Uchawi ambao unatumika katika mila nyingi pamoja na tamaduni kadhaa katika jaribio la ushawishi wa kimwili kupitia njia zisizo za kawaida. Hii ni tofauti na White Magic ambao inalenga katika nyanja ya ushawishi ulio mwema katika imani hasa hasa katika kuponya magonjwa pamoja na kutengeneza dawa. Black Magic inahusika hasa katika kuumiza nafsi ya mtu au mnyama.
Black magic au uchawi mweusi unafanyika kupitia vitendo kama vile; kutengeneza mwanasesere kupitia imani ya Voodoo, Hirizi, alama pamoja na ishara za kichawi, laana na mikosi pamoja na ndumba mbalimbali.
Black magic inatumika ili:
1. Kumuwekea mtu laana au mikosi katika maisha yake.
2. Kumlazimisha mtu kufanya jambo bila ridhaa yake. Mfano: kulima shamba kubwa akiwa usingizini.
3. Kuita uwepo wa mashetani pamoja na mapepo.
4. Kufufua wafu.
5. Pamoja na kutafuta maisha marefu kupitia nguvu za kishetani.
Je ni kina nani haswa wanajihusisha na uchawi huu:
1. Jamii ya Wicca nchini Uingereza wapo watu wanaofanya uchawi wa namna hii. Kuanzia karne ya 20 inaaminika kuwa wanajamii hawa walikuwa wanafanya kazi zinazohusiana na uchawi wa namna hii. Ijapokuwa imani juu ya jamii ya Wicca inasimamia katika kuponya na sio kudhuru nafsi ila asilimia kubwa ya wanajamii wanafanya vitendo vinavyoendana na Black magic.
2. Jamii nyingine ni Santeria, hawa wanapatatikana katika maeneo machache ya Carribean pamoja na Afrika ya Magharibi. Ingawa imani yao inajumuisha baadhi ya vitu kutoka Katika imani ya Wakatoliki, ambayo imewapelekea kuwa sheria kuu moja "Do unto others as you would have done unto you." ambayo imetolewa katika maneno ya Biblia katika kitabu cha Luka mtakatifu 6:31. Hivyo kuidhoofisha imani ya Black magic. Lakini bado kuna wanajamii wanaokiuka sheria hiyo kwa kushiriki katika kufanya matendo ya black magic. Wanafanana kidogo na jamii ya Voodoo (nitawaeleza mbele kidogo).
3. Imani ya Voodoo, hii ni kati ya jamii yenye kusifika kwa kutumia uchawi mweusi katika asilimia zaidi ya 90. Kwani hawa jamaa wana uwezo wa kutengeneza ndumba ya kumdhuru mtu kwa kiasi kidogo sana mpaka kufikia dollar 5 za kimarekani. Ijapokuwa waganga wengi wa Voodoo wanatibu pamoja na kutengeneza tiba Kw kutumia uchawi mweupe bado wana ujuzi mwingi sana wa kutumia black magic. Yaani hata akikupa tiba kwa White magic bado anaweza kutumia black magic kukupa tena hali dhoofu ili urudi apige pesa.
4. Dini za Shetani, kumbuka sio wote waliopo katika dini hizi ni wachawi bali kuna watu ambao wao wanashikilia imani ya kupata maisha au uzima wa milele kupitia njia ya shetani, hivyo kupelekea kutumia black magic katika kuwaita majini, mashetani pamoja na mapepo. Hii ni kupitia kuweka sala za kuabudu shetani na kuweka dawa za kichawi.
Je utajuaje kama umerushiwa uchawi mweusi?
Kwanza inapelekea kuchoka kwa ghafla, ikifuatana na kichwa kuuma na kuwa kizito. Pia kwa wale ambao wapo sensitive sana utaanza kuhisi kitu kisicho cha kawaida mfano, kuhisi haupo peke yako kuzunguka mazingira yako, nywele kusimama ghafla pamoja na kuigiwa na uoga hofu ghafla.
Asante Niishie Hapo kwa sasa
Sent using Infinix hot 4